ATCL kupunguza na kusitisha Safari zake kupisha matengenezo ya Injini

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,029
1,645
IMG_1965.jpg
 
Airbus A220-300,hivi hizi zinasafiri kwenda wapi,maana sidhani kama zinatumika kwa safari za ndani ya nchi...
 
Na hizi mpya zilizonunuliwa na system ya engine hizo hizo ambazo zinahitaji matengenezo na zenyewe zinatengenezwa! Hivi madaraka yanalevya eenhe! unakuwa haupo timamu kabisa
 
Kulifufua hili shirika kulikuwa ni kwa kukurupuka. Ni bora wangewaachia sekta binafsi tu waliendeshe wao wapewe gawio.
Bora wangetumia hayo matrillion ya kifasadi walizonunua hizo ndege kutatua tatizo sugu la maji. Watu wanapanda hizo ndege huku wananuka vikwapa kwasabau hawajaoga.
 

Shirika la ndege Air Tanzania limesema kuwa litapunguza miruko na kufuta baadhi ya safari zao kulingana na idadi ya ndege zilizopo.​

Katika taarifa ya Shirika hilo, imeelezwa kuwa kutokana na changamoto za kiufundi kote duniani za injini aina ya PW1524G-3 zinazotumika katika ndege za Airbus A220-300 kumekuwa na uchaleweshaji wa ndege za shirika hilo wakati changamoto hiyo ikitafutiwa ufumbuzi.

Mkurugezi wa Shirika la ndege, ATCL, Ladislaus Matindi akiongea na BBC amesema Shirika huu ni uamuzi wa muda mfupi ili kutoa muda kwa watengenezaji wa injini za ndege hizo kushughulikia matatizo yaliyopo.
''Injini si kuwa inatengenezwa ina makosa, kuna mengine yanakuja kutokea baada ya matumizi na hawa watengenezaji watawashauri

Amesema kwa kawaida huwa injini zinatolewa kisha huletewa injini nyingine lakini kwa bahati mbaya mahitaji yamekuwa makubwa wamekuwa na ndege nyingi hawana uwezo huo wa kuleta injini kwa ajili ya kurekebisha kwa hiyo lazima zirudishwe kiwandani zikafanyiwe marekebisho.
''Faida tulizonazo sasa hivi kuendelea kufumbia macho hili jambo kutegemea leo tutafanya kazi kesho hatufanyi linaleta matatizo makubwa sana kwa abiria wetu... kwa hiyo ni lazima tuhakikishe kuwa hapa sasa hivi tuna uwezo huu kutokana na tatizo la hizi ndege, kwa hiyo basi tuwe na safari ambazo zinaendana na uwepo wa ndege zilizopo''.

Amesema kwa shirika ni tatizo kwa kuwa wanapoteza mapato, lakini kwa abiria inakuwa vigumu kwao kuwa na uwanda mpana wa kuchagua safari kwa kuwa ratiba nazo zinakuwa zimepungua.
Bado haijajulikana itatengamaa lini lakini Shirika hilo limesema kuwa halitakuwa tatizo la muda mrefu.
''Hatujajua bado, tunaendelea kuzungumza nao lakini nina uhakika halitakuwa tatizo la muda mrefu, ndege zetu zina rekodi nzuri sana kwahiyo tunaposema kuna tatizo, kuna tatizo dogo ambalo linatakiwa kushughulikiwa, lisiende likawa tatizo kubwa ambalo linaweza kuleta ajali, ndiyo maana yetu. Alisema Bw.Matindi
 

Attachments

  • 1668103256812.gif
    1668103256812.gif
    42 bytes · Views: 3
changamoto za kiufundi kote duniani za injini aina ya PW1524G-3 zinazotumikmaa katika ndege za Airbus A220-300 kumekuwa na uchaleweshaji wa ndege za shirika

Maneno mazito , serikali sikivu iyachukue na kuyafanyia kazi



The FAA released an Air Worthiness Directive 2019-19-11 requiring following actions on Pratt & Whitney Models PW1519G, PW1521G, PW1521GA, PW1524G, PW1525G, PW1521G-3, PW1524G-3, PW1525G-3, PW1919G, PW1921G, PW1922G, PW1923G, and PW1923G-A turbofan engines that have accumulated fewer than 300 flight cycles.

The FAA received reports of two recent IFSDs on PW PW1524G-3 model turbofan engines. The first IFSD occurred on July 25, 2019 and the second IFSD occurred on September 16, 2019. These IFSDs were due to failure of the LPC R1, which resulted in the LPC R1 releasing from the LPC case and damaging the engine. LPC rotor failures historically have released high-energy debris that has resulted in damage to engines and airplanes (see Advisory Circular (AC) 39-8, “Continued Airworthiness Assessments of Powerplant and Auxiliary Power Unit Installations of Transport Category Airplanes,”
READ MORE: rgl.faa.gov.
 
Air Tanzania ina jumla ya ndege 4 aina ya airbus a220 ambazo zitaathiriwa na changamoto kama iliyoelezwa na taarifa ya ATCL pamoja na mamlaka ya usafiri wa anga FAA ya Marekani

 
Kulifufua hili shirika kulikuwa ni kwa kukurupuka. Ni bora wangewaachia sekta binafsi tu waliendeshe wao wapewe gawio.
Hee Tena nnchi kubwa bila ndege zake siku wakiambiwa abira kuruka had mwanza milion itakuwa balaa

Magu kafanya vzr tumpongeze
 
Back
Top Bottom