ATCL kupeleka ndege Afrika Kusini pamoja na Airhostess walikuwa sahihi, tusichukulie kila jambo ni "ufisadi"

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Kuna wakati unaposikiliza hotuba za Mhe. Rais, zile ambazo amejijengea utaratibu wa kutuhutubia bila kuandika wala kusoma popote, basi unapata picha kuwa kuna baadhi ya wasaidizi wake, ama wanakuwa na ukosefu wa data za jambo fulani au ni vile wanafikisha lolote wanaloliona huko walikopandikizwa kwa sura ya ufisadi.

Wakati wa kumuapisha Balozi Mlowola, Rais kwa hotuba yake ya kusisimua, ameibua mjadala mkubwa sana ndani ya Taifa, mjadala unaochagizwa na kauli yake dhidi ya ATCL na ndege zake, mjadala unaoonyesha licha ya ukali wa Rais, lakini bado watu wanafisadi na kutumia mali za umma vibaya.

Wengi wameshangilia sana maneno yale ya Rais,
na kunogesha mjadala, Rais alitembelea "ATCL hangar" na kujionea jinsi ndege ilivyopakwa rangi kwa milioni 7, na kwa "Uzalendo" wa wapaka rangi, Rais akaongeza 10 ya juu.

Lakini tujiulize, hivi ni kweli katika kipindi hiki cha ukali na ufuatiliaji wa Rais bado kuna watu hawaogopi kiasi cha kutaka kuiba mbele ya macho ya bwana mkubwa? Tena uwizi ndani ya mahali ambapo jicho la Rais lipo saa 24? Maana katika nembo ya mafanikio ya awamu ya tano, basi ni kufufuka kwa ATCL na uwekezaji wa ndege mpya(Kwa hili nipo na JPM mpaka dakika ya mwisho).

Jambo la kufahamu ni kuwa, uwekezaji katika usafiri wa anga unahitaji gharama kubwa, hizo ni pamoja na gharama za malipo kwa nguvu kazi na malipo kwa ukarabati na uendeshaji wa ndege na vile vinavyoambatana navyo, sio kila jambo liangaliwe kwa jicho la "ufisadi" na sio kila jambo lisifiwe kwa jina la "kubana matumizi".

Tukienda na dhana hii, tutaliuwa shirika, tutafanya kazi chini ya viwango na tutapoteza "confidence" ya wataalamu kutushauri kitaalamu maana wanaogopa kuonekana ni sehemu wa mafisadi wanaotaka kujipatia pesa kwa njia ya ukarabati au uendeshaji wa shirika letu. Ifikie mahali, katika haya mambo ya kitaalamu, tuwaachie wataalamu wetu na hao tuliowapandikiza toka "Eagle House" waendelee kufanya kazi zao nyingine ambazo haziingiliani na utaalamu moja kwa moja.

Usafiri wa anga una taratibu zake kwa hatua ya kitaifa na kimataifa, wao wenye fani zao wanaita "Standards And Recommended Practices (SARPs)", ingawa hizi hazina "legal binding force" lakini walau nchi wanachama walioziridhia wanapaswa kuzifuata ili kuweka ule mfanano wa ubora wa viwango katika level ya kidunia.

Suala la upakaji wa rangi katika ndege
Hili bila shaka hata kwa mujibu ya kanuni na sheria za TCAA linadondokea kwenye kipengele cha "Marking and Manner of Affixation (hapa wanasheria watanisahihisha). Aircraft Registration and Markings Regualations zinatoa muongozo wa namna ndege inavyopaswa kupakwa rangi inapobadilika kutoka kwa "Operator" mmoja kwenda kwa mwingine.

Kwa hiyo, ndege aliyoisema Rais, Operator wake alikuwa ni TGFA, na logo pamoja na rangi ya TGFA ni tofauti na rangi na logo ya ATCL. TGFA rangi yake ya kujitambulisha ni nyeupe na blue bahari wakati rangi ya ATCL ni nyeupe na blue, nembo ya TGFA ni bibi na bwana wakati ya ATCL ni twiga. Hivyo ATCL walitaka kuondoa rangi hii yote pamoja na logo, na kwa kweli kwa viwango vya kimataifa (the bitter reality is - Tanzania can not do such kind of a thing).

Kuipaisha ndege kwenda Afrika Kusini ambapo walau watu waliangalia unafuu wa bei kulingana na sera za sasa ilikuwa ni jambo la lazima na la kawaida sana. Sisi hatujafikia viwango hivyo, huo ndio ukweli. Hao waliosifiwa si kwamba wamefanya kile kilichotakiwa kwenda kufanywa Afrika Kusini, ila wamechomeka tu logo kwenye ubavu na sehemu za fusalage, fuel tanks, tail boom na engine cowling.

Hii ni kama Fastjet na rangi ya njano, nyeupe, nyekundu na kasuku na muito wake uliita kama "Gray bird" maana logo yake ilikuwa ni kasuku wa kijivu. South Afrika ni rangi za bendera yao na mnyama jamii ya swala(Springbok) na muito wake popote duniani huitwa kama "Springbok" kwa hiyo huwezi kui-brand South Africa bila uwepo wa hizo rangi zake, na hili ndio ATCL walikusudia kulifanya.

Kwa hiyo, kwa mujibu wa kanuni hizi za usajili, nadhani zinataka marks, design pamoja symbol zishabihiane na operator. Ila kwa sababu labda TCAA, TGFA na ATCL wote ni watoto wa baba mmoja, hili si tatizo, lakini hata kama si tatizo basi isijenge picha kuwa kulikuwa na dalili ya ufisadi kwa watu wa ATCL kumbe wao walikuwa wanafuata Standards tu na ndio maana ukiangalia rangi ya mstari wa ubavuni na ule wa maandishi ya ATCL katika hiyo ndege iliyopakwa rangi, utagundua kuwa zile ni blue mbili zinazotofautiana. Ya ubavuni kwenye mstari ni blue ya TGFA na kwenye neno "Air Tanzania" ni blue ya ATCL.

Na lengo la ATCL lilikuwa ni kukwangua ndege nzima na kupaka rangi na logo za ATCL na kuondoa zile za TGFA, kitu ambacho ni Standards za usafiri wa anga, ila sababu mwenye nazo kaamua wapake rangi juu ya rangi, basi wale walioamua kuipeleka Afrika Kusini isionekane walikuwa wezi. Ila, tuwe tu tayari kwa matokeo ya kupaka rangi juu ya rangi.

Kimsingi ndege zote za ATCL ni za TGFA, na serikali ilifanya hivyo ili tusipokwe na wanaoidai ATCL yetu.

Kuhusu Air Hostess kuwamo ndani ya ndege
Hili la Air Hostage(nadhani alimaanisha air hostess), halo halikuwa la kusemwa hadharani maana ni kama waliomfikishia Rais taarifa hizi wakidhani wameibua ufisadi ni kama tu na wao wamejiabisha.

Ndege ya aina ile inapokuwa na safari ndefu nje ya nchi kama Afrika Kusini, ni lazima ibebe hata Flight Attendants wawili, na hii ndio standard, tunapotaka mambo mazuri basi tukubali na gharama zake.

Flight Attendants ni sehemu ya "Cabin Crew", hawa zaidi ya kutugawia chai na kalimati tunaposafiri, wao pia ni wanahusika na mambo ya safety kwa cockpit crew, ndio watoa huduma ya kwanza kama rubani mmoja ataugua ghafla akiwa angani, hawa wana kazi zaidi ya ile tunayodhania, hawa kusafiri na ndege ikiwa haina abiria a safari ndefu ni moja ya hitaji muhimu la kiusalama angani, na pia hata anaongezeka injinia ambaye anapaswa kuwepo ili kutoa msaada wa tatizo la kiufundi ndege ikiwa angani.

Hivyo hawa kujumuishwa katika safari ni hitaji la kiusalama na sio ufisadi, kama tunataka mambo mazuri basi tukubali na gharama zake. Kuna incidence nyingi ambapo cabin crew wamesaidia marubani wakati wa hatari angani na kuokoa maisha ya marubani.

Hivyo, kuna wakati tusidhani kila kilicho nafuu ni faida, nafuu nyingine ni aghali. Na tusitazame kila jambo kwa mentality ya kuwa tunaibiwa ili tuweze kuwa wa kimataifa na tukidhi viwango ni lazima tukubali pia kutumia gharama.

Yote kwa yote, pongezi zimwendee Mh. Rais kwa jinsi anavyolipa nguvu shirika letu na kutufanya sasa na sisi tupatikane katika rada za usafiri wa anga duniani, naona mpaka walio USA wanatuchungulia kwenye flight radar na kutuombea mabaya. Kwenye hili la ATCL, wengi tupo na JPM mpaka tone la mwisho cha muhimu wale waliopandikizwa, wasiangalie kila jambo kwa jicho la ufisadi, tutaendesha mambo chini ya kiwango.

Zaidi, soma hapa:

 
"Na lengo la ATCL ilikuwa ni kukwangua ndege nzima na kupaka rangi na logo za ATCL na kuondoa zile za TGFA,kitu ambacho ni Standards za usafiri wa anga,ila sababu mwenye nazo kaamua wapake rangi juu ya rangi,basi wale walioamua kuipeleka Afrika Kusini isionekane walikuwa wezi.Ila tuwe tu tayari kwa matokeo ya kupaka rangi juu ya rangi"

Kwenye andiko lako lote ilo eneo limenitafakarisha sana. Natamani sana kama ungeetueleza kidogo madhara yatokanayo na kupaka rangi juu ya rangi.
 
Ili la Air Hostage(nadhani alimaanisha air hostess),nalo halikuwa la kusemwa hadharani,

Hivi alisema air hostage!!! Halafu tukisema Magufuli anatatizo la lugha ya Kiingereza mashabiki wa CCM wanasema sie Chadema. Kutojua kiingereza sio tusi. Mbona mie Kfaransa kinanipa shida sana!

Ila suala la kupaka rangi juu ya rangi hizi kiki za Magufuli zitakuja kuleta madhara. Uzito wa rangi inayopakwa ndege ni jambo linazozingatiwa katika kupaka rangi na ndege ikiwa full board hiyo ni factor kubwa tu katika take off speed!

NIliandika uzi juu ya usalama wa hizi ndogo kwa kuzipaka rangi kwa utashi wa Magufuli


https://www.jamiiforums.com/threads...milioni-ya-fedha.1566081/page-6#post-30910162
 
"Na lengo la ATCL ilikuwa ni kukwangua ndege nzima na kupaka rangi na logo za ATCL na kuondoa zile za TGFA,kitu ambacho ni Standards za usafiri wa anga,ila sababu mwenye nazo kaamua wapake rangi juu ya rangi,basi wale walioamua kuipeleka Afrika Kusini isionekane walikuwa wezi.Ila tuwe tu tayari kwa matokeo ya kupaka rangi juu ya rangi"

Kwenye andiko lako lote ilo eneo limenitafakarisha sana. Natamani sana kama tungeelewa madhara yatoknayo na kupaka rangi juu ya rangi.
wataalam kwanini wasingemshauri rais kwamba kupaka rangi juu ya rangi kuna moja mbili tatu ila wao wakawa wanaforce tu iende nje ili wapate posho ovyo sana wataalamu wetu.

Mnataka kutuambia twiga kuchorwa pale kutaidondosha ndege ile sio.
 
alafu anatuhimiza tuwe wazalendo wakati kesha jenga tabaka mioyoni mwa watu
Ukiwa katili,mbaguzi na muovu,nani atakutakia mema au kukusema kwa mazuri?

Umepandikiza chuki na mgawanyika miongoni mwa watu wako kutokana na matendo yako, sasa utegemee nini kutoka kwa watu hao?

Ukipanda bangi,huwezi vuna mahindi.
 
Kuna wakati unaposikiliza hotuba za Mh.Rais,zile ambazo amejijengea utaratibu wa kutuhutubia bila kuandika wala kusoma popote,basi unapata picha kuwa kuna baadhi ya wasaidizi wake,ama wanakuwa na ukosefu wa data za jambo fulani au ni vile wanafikisha lolote wanaloliona huko walikopandikizwa kwa sura ya ufisadi.

Wakati wa kumuapisha Balozi Mlowola,Rais kwa hotuba yake ya kusisimua,ameibua mjadala mkubwa sana ndani ya Taifa,mjadala unaochagizwa na kauli yake dhidi ya ATCL na ndege zake,mjadala unaoonyesha licha ya ukali wa Rais,lakini bado watu wanafisidi na kutumia mali za umma vibaya.

Wengi wameshangilia sana maneno yale ya Rais,
na kunogesha mjadala,Rais alitembelea "ATCL hangar" na kujionea jinsi ndege ilivyopakwa rangi kwa milioni 7,na kwa "Uzalendo" wa wapaka rangi,Rais akaongeza 10 ya juu.

Lakini tujiulize,hivi ni kweli katika kipindi hiki cha ukali na ufuatiliaji wa Rais bado kuna watu hawaogopi kiasi cha kutaka kuiba mbele ya macho ya bwana mkubwa?Tena uwizi ndani ya mahali ambapo jicho la Rais lipo masaa 24?Maana katika nembo ya mafanikio ya awamu ya tano,basi ni kufufuka kwa ATCL na uwekezaji wa ndege mpya(Kwa hili nipo na JPM mpaka dakika ya mwisho).

Jambo la kufahamu ni kuwa,uwekezaji katika usafiri wa anga unahitaji gharama kubwa,hizo ni pamoja na gharama za malipo kwa nguvu kazi na malipo kwa ukarabati na uendeshaji wa ndege na vile vinavyoambatana navyo,sio kila jambo liangaliwe kwa jicho la "ufisadi" na sio kila jambo lisifiwe kwa jina la "kubana matumizi".

Tukienda na dhana hii,tutaliuwa shirika,tutafanya kazi chini ya viwango na tutapoteza "confidence" ya wataalamu kutushauri kitaalamu maana wanaogopa kuonekana ni sehemu wa mafisadi wanaotaka kujipatia pesa kwa njia ya ukaratabi au uendeshaji wa shirika letu.Ifikie mahali,katika haya mambo ya kitaalamu,tuwaachie wataalamu wetu na hao tuliowapandikiza toka "Eagle House" waendelee kufanya kazi zao zingine ambazo haziingiliani na utaalamu moja kwa moja.

Usafiri wa anga una taratibu zake kwa hatua ya kitaifa na kimataifa,wao wenye fani zao wanaita "Standards And Recommended Practices (SARPs)",ingawa hizi hazina "legal binding force" lakina walau nchi wanachama walioziridhia wanapaswa kuzifuata ili kuweka ule mfanano wa ubora wa viwango katika level ya kidunia.

Suala la upakaji wa rangi katika ndege,hili bila shaka hata kwa mujibu ya kanuni na sheria za TCAA linadondokea kwenye kipengere cha "Marking and Manner of Affixation,(hapa wanasheria watanisahihisha).Aircraft Registration and Markings Regualations zinatoa muongozo wa namn ndege inavyopaswa kupakwa rangi inavyobadilika kutoka kwa "Operator" mmoja kwenda kwa mwingine.

Kwa hiyo,ndege aliyoisema Rais,Operator wake alikuwa ni TGFA,na logo pamoja na rangi ya TGFA ni tofauti na rangi na logo ya ATCL.TGFA rangi yake ya kujitambulisha ni nyeupe na blue bahari wakati rangi ya ATCL ni nyeupe na blue,nembo ya TGFA ni bibi na bwana wakati ya ATCL ni twiga.Hivyo ATCL walitaka kuondoa rangi hii yote pamoja na logo,na kwa kweli kwa viwango vya kimataifa,the bitter reality is,Tanzania can not do such kind of a thing...Kuipaisha ndege kwenda Afrika kusini ambapo walau watu waliangalia unafuu wa bei kulingana na sera za sasa ilikuwa ni jambo la lazima na la kawaida sana.Sisi hatujafikia viwango hivyo,huo ndio ukweli.Hao waliosifiwa si kwamba wamefanya kile kilichotakiwa kwenda kufanywa Afrika Kusini,ila wamechomeka tu logo kwenye ubavu na sehemu za fusalage,fuel tanks,tail boom na engine cowling.

Hii ni kama Fastjet na rangi ya njano,nyeupe,nyekundu na kasuku,na muito wake uliita kama "Gray bird" maana logo yake ilikuwa ni kasuku wa kijivu,South Afrika ni rangi za bendera yao na mnyama jamii ya swala(Springbok) na muito wake popote duniani huitwa kama "Springbok" kwa hiyo huwezi kui-brand South Africa bila uwepo wa hizo rangi zake,na hili ndio ATCL walikusudia kulifanya.

Kwa hiyo,kwa mujibu wa kanuni hizi za usajili,nadhani zinataka marks,design pamoja symbol zishahabiane na operator.Ila kwa sababu labda TCAA,TGFA na ATCL wote ni watoto wa baba mmoja,hili si tatizo,lakini hata kama si tatizo basi isijenge picha kuwa kulikuwa na dalili ya ufisadi kwa watu wa ATCL kumbe wao walikuwa wanafuata Standards tu.Na ndio maana ukiangalia rangi ya mstari wa ubavuni na ule wa maandishi ya ATCL,zile ni blue mbili zinazotofautiana.

Na lengo la ATCL ilikuwa ni kukwangua ndege nzima na kupaka rangi na logo za ATCL na kuondoa zile za TGFA,kitu ambacho ni Standards za usafiri wa anga,ila sababu mwenye nazo kaamua wapake rangi juu ya rangi,basi wale walioamua kuipeleka Afrika Kusini isionekane walikuwa wezi.Ila tuwe tu tayari kwa matokeo ya kupaka rangi juu ya rangi.Kimsingi ndege zote za ATC ni za TGFA,na serikali ilifanya hivyo ili tusipokwe na wanaoidai ATCL yetu.

Ili la Air Hostage(nadhani alimaanisha air hostess),nalo halikuwa la kusemwa hadharani,maana ni kama waliomfikishia Rais taarifa hizi wakidhani wameibua ufisadi ni kama tu na wao wamejiabisha.Ndege ya aina ile inapokuwa na safar ndefu nje ya nchi kama Afrika Kusini,ni lazima ibebe hata Flight Attendants wawili,na hii ndio standard,tunapotaka mambo mazuri basi tukubali na gharama zake.

Flight Attendants ni sehemu ya "Cabin Crew",hawa zaidi ya kutugawia chai na kalimati tunaposafiri,wao pia ni wanahusika na mambo ya safety kwa cockpit crew,ndio watoa huduma ya kwanza kama rubani mmoja ataugua ghafla akiwa angani,hawa wana kazi zaidi ya ile tunayodhania,hawa kusafiri na ndege ikiwa haina abiria a safar ndefu ni moja ya hitaji muhimu la kiusalama angani,na pia hata anaongezeka injinia ambaye anapaswa kuwepo ili kutoa msaada wa tatizo la kiufundi ndege ikiwa angani.

Hivyo hawa kujumuishwa katika safari ni hitaji la kiusalama na sio ufisadi,kama tunataka mambo mazuri basi tukubali na gharama zake.Kuna incidence nyingi ambapo cabin crew wamesaidia marubani wakati wa hatari angani na kuokoa maishaya marubani.

Hivyo,kuna wakati tusidhani kila kilicho nafuu ni faida,nafuu nyingine ni aghali.Na tusitazame kila jambo kwa mentality ya kuwa tunaibiwa,ili tuweze kuwa wa kimataifa na tukidhi viwango ni lazima tukubali pia kutumia gharama.

Yote kwa yote,pongezi zimwendee Mh.Rais kwa jinsi anavyolipa nguvu shirika letu na kutufanya sasa na sisi tupatikane katika rada za usafiri wanga duniania,naona mpaka walio USA wanatuchungulia kwenye flight radar na kutuombea mabaya.Kwenye hili la ATCL,wengi tupo na JPM mpaka tone la mwisho,cha muhimu wale waliopandikizwa,wasiangalie kila jambo kwa jicho la ufisadi,tutaendesha mambo chini ya kiwango.
Ulitafutwa sana juzi mkuu...... Lakini baadae tulipokuona unamalizia kumchora twiga tukaelewa kumbe ulikuwa busy!
 
"Na lengo la ATCL ilikuwa ni kukwangua ndege nzima na kupaka rangi na logo za ATCL na kuondoa zile za TGFA,kitu ambacho ni Standards za usafiri wa anga,ila sababu mwenye nazo kaamua wapake rangi juu ya rangi,basi wale walioamua kuipeleka Afrika Kusini isionekane walikuwa wezi.Ila tuwe tu tayari kwa matokeo ya kupaka rangi juu ya rangi"

Kwenye andiko lako lote ilo eneo limenitafakarisha sana. Natamani sana kama tungeelewa madhara yatoknayo na kupaka rangi juu ya rangi.

1. UZITO UNAKUWA ZAIDI YA ULE ULIOKUSUDIWA.
2. RANGI INAKUWA SIO BORA, HIVYO HAIWEZI KUDUMA WALA KULETA MUONEKANO MZURI.
3. NDEGE INA SENSORS NYINGI SANA, HALI HII INAWEZA KUSABABISHA BAADHI ZIKAFUNIKWA NA RANGI NA KULETA
FAULT NYINGI AMBAZO ZINAWEZA KULETA MADHARA AU KUONGEZA GHARAMA ZA MATENGENEZO.

MENGINE WATAONGEZA WATAALAMU HIYO KUTOKA KWENYE BASIC YA KAWAIDA KABISA KWENYE ENGINEERING.
 
Yaani ndege nzima m5,? du wazalendo kweli kweli hawa na m10 juu.
Kumbe ni rangi juu ya rangi!
Amaa kweli hapa kazi tu.
Mkuu kukwangua rangi ya ndege ili uipake upya inahitaji chemicals na wataalamu wa hiyo kazi. Halafu Magufuli anakuja kupiga kelele za kiki za kisiasa eti ameokoa Tshs 160 walitaka kuzifanyia ufisadi. Hivi analinganisha jinsi hiyo ndege ambavyo imepakwa rangi hapa TZ na jinsi ambavyo ingepakwa rangi nje? Anajisifia kuokoa fedha kwa kuamuru watu wapake rangi juu ya rangi kwa kutumia brashi!
 
Hata muandike kitabu kujitetea ukweli utabaki palepale maelekeze yalikuwa muandike tu air tanzania na mchore twiga hayo mengine iliongeza nyie wenyewe ili mpate pa kupiga.

Acha ubishi mbona jamaa kaelezea kitaalam tu hapo wala hakuna ukakasi wowote.
 
wataalam kwanini wasingemshauri rais kwamba kupaka rangi juu ya rangi kuna moja mbili tatu ila wao wakawa wanaforce tu iende nje ili wapate posho ovyo sana wataalamu wetu.

Mnataka kutuambia twiga kuchorwa pale kutaidondosha ndege ile sio.
Mkuu unaniuliza mimi kweli? Na mimi natamani kujua hizo sababu za kitaalamu kuhusu kupaka rangi juu ya rangi. Kimsingi mimi naona mtoa mda/wataalamu husika wamefunika kombe tu ili...
 
Back
Top Bottom