ATCL kupeleka ndege Afrika Kusini pamoja na Airhostess walikuwa sahihi, tusichukulie kila jambo ni "ufisadi"

Kwa uzi wa kiuelewa na ufafanuzi wa namna hii subiria kuitwa majina. Utasikia hoo wakala wa mabeberu, umekosa uzalendo. Ila mkuu haya mambo unayajua na umeelezea kitaalam. Hongera
 
Hoja yangu ni kuwa kwa nini hawa wapiga dili wa bongo kwa kushirikiana na mabeberu wanataka kupeleka ndege ikiwa na "air hostage" badala ya "air hostess"?? Huoni kua hili linafanywa makusudi kukwamisha juhudi za kuelekea uchumi wa vi-wonder unaosimamiwa na serikali tukufu ya chama pendwa cha mapinduzi???Nimelipenda swali lako binti, unaonekana uko upande wa kuunga mkono juhudi!
Asante kwa hoja MFU!
 
Tatizo mnabisha mambo msiyoelewa. Hivi unafikiri kupiga rangi ndege ya abiria ni sawa na kupiga rangi gari? Inawezekana tatizo lako ni lugha au mapenzi yaliyopita kwa Jiwe, au ugonjwa wa Uzalendo Induced Logic Deficiency Syndrome - UIDS.

In-service experience has taught us that even activities performed on the aircraft mainly for cosmetic reasons, like washing or painting, may have an impact on the safety of operations.

The in-service incidents described in this article illustrate the need to care-fully follow the indicated instructions available in the Aircraft Maintenance Manual, Structure Repair Manual as well as Tool and Equipment Manual.
Are you saying we need to send our aircracfts outside Tanzania FOR WASHING so as to avoid "the so called impact on the safety of operations"/' Are you guys SERIOUS?STOP KIDDING!
 
If necessary yes. If we dont have people that know how to wash a passenger plane in a safe manner. Either that or we train our own people.
 
Kuna wakati unaposikiliza hotuba za Mhe. Rais, zile ambazo amejijengea utaratibu wa kutuhutubia bila kuandika wala kusoma popote, basi unapata picha kuwa kuna baadhi ya wasaidizi wake, ama wanakuwa na ukosefu wa data za jambo fulani au ni vile wanafikisha lolote wanaloliona huko walikopandikizwa kwa sura ya ufisadi.

Wakati wa kumuapisha Balozi Mlowola, Rais kwa hotuba yake ya kusisimua, ameibua mjadala mkubwa sana ndani ya Taifa, mjadala unaochagizwa na kauli yake dhidi ya ATCL na ndege zake, mjadala unaoonyesha licha ya ukali wa Rais, lakini bado watu wanafisadi na kutumia mali za umma vibaya.

Wengi wameshangilia sana maneno yale ya Rais,
na kunogesha mjadala, Rais alitembelea "ATCL hangar" na kujionea jinsi ndege ilivyopakwa rangi kwa milioni 7, na kwa "Uzalendo" wa wapaka rangi, Rais akaongeza 10 ya juu.

Lakini tujiulize, hivi ni kweli katika kipindi hiki cha ukali na ufuatiliaji wa Rais bado kuna watu hawaogopi kiasi cha kutaka kuiba mbele ya macho ya bwana mkubwa? Tena uwizi ndani ya mahali ambapo jicho la Rais lipo saa 24? Maana katika nembo ya mafanikio ya awamu ya tano, basi ni kufufuka kwa ATCL na uwekezaji wa ndege mpya(Kwa hili nipo na JPM mpaka dakika ya mwisho).

Jambo la kufahamu ni kuwa, uwekezaji katika usafiri wa anga unahitaji gharama kubwa, hizo ni pamoja na gharama za malipo kwa nguvu kazi na malipo kwa ukarabati na uendeshaji wa ndege na vile vinavyoambatana navyo, sio kila jambo liangaliwe kwa jicho la "ufisadi" na sio kila jambo lisifiwe kwa jina la "kubana matumizi".

Tukienda na dhana hii, tutaliuwa shirika, tutafanya kazi chini ya viwango na tutapoteza "confidence" ya wataalamu kutushauri kitaalamu maana wanaogopa kuonekana ni sehemu wa mafisadi wanaotaka kujipatia pesa kwa njia ya ukarabati au uendeshaji wa shirika letu. Ifikie mahali, katika haya mambo ya kitaalamu, tuwaachie wataalamu wetu na hao tuliowapandikiza toka "Eagle House" waendelee kufanya kazi zao nyingine ambazo haziingiliani na utaalamu moja kwa moja.

Usafiri wa anga una taratibu zake kwa hatua ya kitaifa na kimataifa, wao wenye fani zao wanaita "Standards And Recommended Practices (SARPs)", ingawa hizi hazina "legal binding force" lakini walau nchi wanachama walioziridhia wanapaswa kuzifuata ili kuweka ule mfanano wa ubora wa viwango katika level ya kidunia.

Suala la upakaji wa rangi katika ndege
Hili bila shaka hata kwa mujibu ya kanuni na sheria za TCAA linadondokea kwenye kipengele cha "Marking and Manner of Affixation (hapa wanasheria watanisahihisha). Aircraft Registration and Markings Regualations zinatoa muongozo wa namna ndege inavyopaswa kupakwa rangi inapobadilika kutoka kwa "Operator" mmoja kwenda kwa mwingine.

Kwa hiyo, ndege aliyoisema Rais, Operator wake alikuwa ni TGFA, na logo pamoja na rangi ya TGFA ni tofauti na rangi na logo ya ATCL. TGFA rangi yake ya kujitambulisha ni nyeupe na blue bahari wakati rangi ya ATCL ni nyeupe na blue, nembo ya TGFA ni bibi na bwana wakati ya ATCL ni twiga. Hivyo ATCL walitaka kuondoa rangi hii yote pamoja na logo, na kwa kweli kwa viwango vya kimataifa (the bitter reality is - Tanzania can not do such kind of a thing).

Kuipaisha ndege kwenda Afrika Kusini ambapo walau watu waliangalia unafuu wa bei kulingana na sera za sasa ilikuwa ni jambo la lazima na la kawaida sana. Sisi hatujafikia viwango hivyo, huo ndio ukweli. Hao waliosifiwa si kwamba wamefanya kile kilichotakiwa kwenda kufanywa Afrika Kusini, ila wamechomeka tu logo kwenye ubavu na sehemu za fusalage, fuel tanks, tail boom na engine cowling.

Hii ni kama Fastjet na rangi ya njano, nyeupe, nyekundu na kasuku na muito wake uliita kama "Gray bird" maana logo yake ilikuwa ni kasuku wa kijivu. South Afrika ni rangi za bendera yao na mnyama jamii ya swala(Springbok) na muito wake popote duniani huitwa kama "Springbok" kwa hiyo huwezi kui-brand South Africa bila uwepo wa hizo rangi zake, na hili ndio ATCL walikusudia kulifanya.

Kwa hiyo, kwa mujibu wa kanuni hizi za usajili, nadhani zinataka marks, design pamoja symbol zishabihiane na operator. Ila kwa sababu labda TCAA, TGFA na ATCL wote ni watoto wa baba mmoja, hili si tatizo, lakini hata kama si tatizo basi isijenge picha kuwa kulikuwa na dalili ya ufisadi kwa watu wa ATCL kumbe wao walikuwa wanafuata Standards tu na ndio maana ukiangalia rangi ya mstari wa ubavuni na ule wa maandishi ya ATCL katika hiyo ndege iliyopakwa rangi, utagundua kuwa zile ni blue mbili zinazotofautiana. Ya ubavuni kwenye mstari ni blue ya TGFA na kwenye neno "Air Tanzania" ni blue ya ATCL.

Na lengo la ATCL lilikuwa ni kukwangua ndege nzima na kupaka rangi na logo za ATCL na kuondoa zile za TGFA, kitu ambacho ni Standards za usafiri wa anga, ila sababu mwenye nazo kaamua wapake rangi juu ya rangi, basi wale walioamua kuipeleka Afrika Kusini isionekane walikuwa wezi. Ila, tuwe tu tayari kwa matokeo ya kupaka rangi juu ya rangi.

Kimsingi ndege zote za ATCL ni za TGFA, na serikali ilifanya hivyo ili tusipokwe na wanaoidai ATCL yetu.

Kuhusu Air Hostess kuwamo ndani ya ndege
Hili la Air Hostage(nadhani alimaanisha air hostess), halo halikuwa la kusemwa hadharani maana ni kama waliomfikishia Rais taarifa hizi wakidhani wameibua ufisadi ni kama tu na wao wamejiabisha.

Ndege ya aina ile inapokuwa na safari ndefu nje ya nchi kama Afrika Kusini, ni lazima ibebe hata Flight Attendants wawili, na hii ndio standard, tunapotaka mambo mazuri basi tukubali na gharama zake.

Flight Attendants ni sehemu ya "Cabin Crew", hawa zaidi ya kutugawia chai na kalimati tunaposafiri, wao pia ni wanahusika na mambo ya safety kwa cockpit crew, ndio watoa huduma ya kwanza kama rubani mmoja ataugua ghafla akiwa angani, hawa wana kazi zaidi ya ile tunayodhania, hawa kusafiri na ndege ikiwa haina abiria a safari ndefu ni moja ya hitaji muhimu la kiusalama angani, na pia hata anaongezeka injinia ambaye anapaswa kuwepo ili kutoa msaada wa tatizo la kiufundi ndege ikiwa angani.

Hivyo hawa kujumuishwa katika safari ni hitaji la kiusalama na sio ufisadi, kama tunataka mambo mazuri basi tukubali na gharama zake. Kuna incidence nyingi ambapo cabin crew wamesaidia marubani wakati wa hatari angani na kuokoa maisha ya marubani.

Hivyo, kuna wakati tusidhani kila kilicho nafuu ni faida, nafuu nyingine ni aghali. Na tusitazame kila jambo kwa mentality ya kuwa tunaibiwa ili tuweze kuwa wa kimataifa na tukidhi viwango ni lazima tukubali pia kutumia gharama.

Yote kwa yote, pongezi zimwendee Mh. Rais kwa jinsi anavyolipa nguvu shirika letu na kutufanya sasa na sisi tupatikane katika rada za usafiri wa anga duniani, naona mpaka walio USA wanatuchungulia kwenye flight radar na kutuombea mabaya. Kwenye hili la ATCL, wengi tupo na JPM mpaka tone la mwisho cha muhimu wale waliopandikizwa, wasiangalie kila jambo kwa jicho la ufisadi, tutaendesha mambo chini ya kiwango.

Zaidi, soma hapa:

Naona wewe hujipendi kabisaaa maana ufahamu wa kiwango hicho kwa hapa TZ inaweza kuwa balaa sana.
Kwa kuwa hayo unayoandika wakubwa wetu hawakuyasema kabisaaaaaaa
 
Hawa wahusika wangeachwa na kupeleka ndege SA pamoja na idadi yote ya wasindikizaji tungeona tena wanaojiita wanaharakati wakidai serikali inatumia hela vibaya. wangekuja na msemo wa milioni 200 kupaka rangi tu inamaana hakuna wakupanga rangi nchini? tena ungeitwa huu ni upigaji mwingine.
Ndege imeludiwa rangi sehemu zenye jina na nembo ya twiga tu ambazo hazina madhara yoyote kiufundi kwa sehemu husika.
Tunahitaji kuoshwa akili zetu baazi ya watanzania sio bure kwa hali hii.:eek::eek::eek:
 
1+1=? .... wakuu waka introduce Cos ....
Cos 90=1.... then 1+1= Cos90 + Cos 90 ..... tukajichanganya nje ya mada kabsaaaaaa 🀣

(Weka nembo ya twiga na maneno only .. kitu ipae..... Wakaibuka wataalamu... rangi ndege yote koti 6 .... air hostages... Nyambafu)

Stop misusing your brains na kuzua hadithi na mijadala isiyo tija....
 
Uelewa wako kwenye Engineering matters ni mdogo sana sana, lakini pia inaonekana hujawahi hata kumuliki gari..

Ni ngumu kukuelewesha mtu kama wewe sana, jaribu kuongeza maarifa kwa kusoma soma vitu mbali mbali ili ubongo utanuke, kwa ulichokiandika jamaa yangu unakazi kubwa sana, kama wewe ni msomi umesoma tambua uelewa wako ni mdogo..

Unajaribu kufananisha nyumba na chombo cha moto kwenye Rangi?, jaribu basi hata kufikiria gari iliyorudiwa rudiwa rangi mara kumi na nyumba iliyorudiwa rangi mara kumi fanya uchunguzi wa kina bila shaka utajifunza kitu.
kupiga rangi juu ya rangi kumeongeza uzito wa ndege kiasi gani na umeathiri vipi kwenye urukaji wa ndege hiyo? Kata povu ujibu kwa hoja mkuu. Sayansi siyo siasa.
 
Hoja yangu ni kuwa kwa nini hawa wapiga dili wa bongo kwa kushirikiana na mabeberu wanataka kupeleka ndege ikiwa na "air hostage" badala ya "air hostess"?? Huoni kua hili linafanywa makusudi kukwamisha juhudi za kuelekea uchumi wa vi-wonder unaosimamiwa na serikali tukufu ya chama pendwa cha mapinduzi???Nimelipenda swali lako binti, unaonekana uko upande wa kuunga mkono juhudi!
nenda kwenye vijiwe vya gahawa ukapige story hizo mkuu. Hapa ni hoja za maana siyo bla bla
 
1+1=? .... wakuu waka introduce Cos ....
Cos 90=1.... then 1+1= Cos90 + Cos 90 ..... tukajichanganya nje ya mada kabsaaaaaa 🀣

(Weka nembo ya twiga na maneno only .. kitu ipae..... Wakaibuka wataalamu... rangi ndege yote koti 6 .... air hostages... Nyambafu)

Stop misusing your brains na kuzua hadithi na mijadala isiyo tija....
du!
 
Mkuu unaniuliza mimi kweli? Na mimi natamani kujua hizo sababu za kitaalamu kuhusu kupaka rangi juu ya rangi. Kimsingi mimi naona mtoa mda/wataalamu husika wamefunika kombe tu ili...
Mkuu kupaka rangi juu ya rangi athari yake ni kuongeza uzito wa ndege, kuathiri sensors na vitu vingine vinavyohusiana na mawasiliano kama rada/antena nk
 
1+1=? .... wakuu waka introduce Cos ....
Cos 90=1.... then 1+1= Cos90 + Cos 90 ..... tukajichanganya nje ya mada kabsaaaaaa 🀣

(Weka nembo ya twiga na maneno only .. kitu ipae..... Wakaibuka wataalamu... rangi ndege yote koti 6 .... air hostages... Nyambafu)

Stop misusing your brains na kuzua hadithi na mijadala isiyo tija....

You F F F F F F F.....

Cos 90° = 1..? ❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌
 
Lakini tujiulize, hivi ni kweli katika kipindi hiki cha ukali na ufuatiliaji wa Rais bado kuna watu hawaogopi kiasi cha kutaka kuiba mbele ya macho ya bwana mkubwa? Tena uwizi ndani ya mahali ambapo jicho la Rais lipo saa 24? Maana katika nembo ya mafanikio ya awamu ya tano, basi ni kufufuka kwa ATCL na uwekezaji wa ndege mpya(Kwa hili nipo na JPM mpaka dakika ya mwisho
Hiki ndo kipindi Cha kupiga, jiulize kwanini meya wa ilala amejiengua
 
"Na lengo la ATCL ilikuwa ni kukwangua ndege nzima na kupaka rangi na logo za ATCL na kuondoa zile za TGFA,kitu ambacho ni Standards za usafiri wa anga,ila sababu mwenye nazo kaamua wapake rangi juu ya rangi,basi wale walioamua kuipeleka Afrika Kusini isionekane walikuwa wezi.Ila tuwe tu tayari kwa matokeo ya kupaka rangi juu ya rangi"

Kwenye andiko lako lote ilo eneo limenitafakarisha sana. Natamani sana kama ungeetueleza kidogo madhara yatokanayo na kupaka rangi juu ya rangi.
Acha uongo wewe hao walitaka kula bahati nzuri watazibwa midomo kabla ya tendo. Magufuli oyeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Back
Top Bottom