jerrytz
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 5,975
- 4,266
Shirika la ndege la Tanzania lina mpango wa kununua mfumo wa kiteknolojia wa ukataji wa tiketi (ticketing reservation system) kutoka nchini Uturuki.
Mfumo huo utagharimu kiasi cha shilingi za Kitanzania milioni 147/-sawa na dola 67,000/-.
Uwekwaji na matumizi ya mfumo huo utasaidia shirika hilo kuepuka usimamizi mbaya katika uuzwaji wa ticket na pia kuboresha huduma kwa wateja alisema mkurugenzi mtendaji ndugu Ladislaus Matindi.
" Tumeingia makubaliano na Hitit Solutions Co. Wiki Mbili zilizopita ila kupata mfumo huo na mafunzo kwa Wafanyakazi wa ATCL yameshaanza ili kuwafundisha jinsi ya kutumia mfumo huo.
Matumizi ya mfumo huo yanatarajiwa kuanza mwezi ujao.
ATCL ilipoteza kiasi cha shilingi milioni 715 kutokana na mfumo mbovu wa ukatishaji wa ticket hali iliyopelekea waziri Prof. Makame Mbarawa kumsimamisha kazi meneja fedha wa ATCL ndugu Stephen Kasubi.
Tanzania yetu!