getrusa
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 2,150
- 1,812
Sidhani kama waweza kuwa mama kweli.!Usitutisheeee
Jukumu kubwa la mama ni kuangalia madhara yajayo kwa watoto wake!
Ukiona mama anajiwazia yeye kwanza waweza kumuweka katika kundi la wanawake waliopata mimba kwa bahati mbaya.!
1: ikitokea vurugu kisha Nchi ikakosa uelekea thabiti wewe na wanao mtakaa wapi kwa amani?
Mifano ipo hai.. fikiri kuhusu wamama wa Syria, Libya, Congo,Iraq, Ukraine. Somalia, South Sudan.. na Nk.
Na hapa nikukumbushe tu. Inapotokea vita ama machafuko yoyote ya kisiasa wanaoathirika zaidi ni akina mama na watoto.!
2: unapochochea machafuko yoyote tegemea kupata pande mbili zinazo kinzana wale wanaoona wako sawa na wale wana ona hawatendewi sawasawa.!
Katika harakati hizo inategemea mwenye Nguvu ni yupi.!
Utakapoenda barabarani kupigania unachodhani ni haki yako.! Huenda ukakutana na askari ambaye atakujeruhi. Ukavunjika ama mguu au kiuno ama mgongo! Kumbuka askari huyu kafundishwa kituliza ghasia kwa nguvu (Field Force Unit.) Ni kitengo maalumu kwa kazi hiyo..
Sidhani kama atakubembeleza ili uache ufanyacho.! Ukipata hayo majeraha atakayetunza wanao ili wawe na afya bora na malezi kutoka kwa mama ni nani?
Huoni kuwa yamkini utakuwa hukuwatendea haki wanao?
Mwisho:
Kabla hujachochewa ama kujichochea mwenyewe kufanya vurugu zozote tafakari..
1:Je hiki ninacho ambiwa nikipinge ni kweli kina huo uovu?
2: baada ya kukipinga wewe binafsi utapata faida gani?
Natumai unaweza ambulia kitu hapa ukitaka.