Atakaeuliza kwanini CHADEMA hawahudhurii vikao vya Bunge, aulize pia kwanini Rais yuko Chato kwa siku 35+??

Mtoa mada kwn Chato sio Tz?, isitoshe mh ni lazima alindwe kwa nguvu na gharama yoyote. Hebu jipe tafakari ya kulazimika kufanya uchaguzi wa rais.
 
Uongozi wa CHADEMA umesema kuwa wanajiweka karantini katika juhudi za kupambana na Corona, hii si mbaya kutokana na hali ilivyo.

Iwe ni kwenye KAMPENI hapo baadae au sasa hivi, atakayeuliza kwa nini CHADEMA hawahudhurii Bungeni, aulize pia kwanini Raisi Magufuli ameenda kujificha Chato? Nasema ni kujificha kwasababu ikulu Rasmi ni Magogoni, Chamwino tunasubiria atangaze rasmi kuhamia.

Tunatambua kuwa kila wilaya na mkoa una ikulu ndogo ambazo hata Maraisi wengine walikuwa wakifikia wakiwa kwenye ziara ama kampeni, lakini hii ya kukaa siku 35+ (Tangu tarehe 28 March, 2020) hajawahi kutokea. Hata Nyerere alikuwa akienda Butiama ila hii.. Ni kukimbia mpambano wa Corona.

Hivi na Mabunge ya EAST AFRICA yanaendelea?? Tumezoea Bunge la bajeti katika nchi za Afrika Mashariki zikiwa kwenye vikao vya Bunge katika kipindi kinachofanana. Hata Bajeti kuu husomwa kwa siku moja.

TUENDELEE KUJILINDA NA CORONA
Aah huyu ni CCM bwana kila siku wako sawa na yule ni Chadema kila siku hawako sawa.
 
Back
Top Bottom