Askwar Hilonga-Mbunifu aliyeitendea haki PhD yake...

Askwar Hilonga-Mbunifu aliyeitendea haki PhD yake...

Ethos

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2015
Posts
2,294
Reaction score
2,090
Miaka ya Hivi karibuni watanzania wamekuwa wakiamka na kubuni vitu ambavyo vinalinufaisha taifa Kwa kiasi kikubwa .Kama Edwin Bruno alivotengeneza app ya kusoma magazeti Dr Hilonga yeye anagusa maisha ya watu kivingine kabisa!

Kama wengi tujuavyo na wanaharakati wasemavyo kuwa maji ni uhai basi Dr Askwar Hilonga ameamua kulidhihirisha hilo Kwa Vitendo na Sio Maneno Peke yake.

Changamoto ya maji safi na Salama ni yetu sote hivyo wanapotokea wataalam mbalimbali na kuja na njia mbadala ni budi kupongezwa na kupewa Fursa zaidi ili ubunifu huo uifaidishe jamii yote.

Dr Hilonga amebuni Kifaa kiitwacho Nanofilter ambacho kimeshinda tuzo ya ubunifu ya Royal Academy of Engineering mwaka 2015.

Kifaa hicho ambacho kinatumia mchanga ikiongezewa na Nano Materials ili kuondoa vijidudu.

Dr Hilonga akielezea katika video yaYouTube amesema Nanofilter hiyo ina uwezo wa kuondoa vijidudu Kwa Asilimia 97 ila lengo Lake ni kuondoa Kwa Asilimia 99.999 hapo baadae!

Baada ya kutofurahishwa na kitendo cha familia huko kijijini alipozaliwa kutumia maji yasiyo salama alijiuliza Je PhD yake aliyoipata nchini Korea itasaidiaje watu wa kijijini kwake ndipo alipoamua kubuni teknolojia hiyo muhimu katika maswala ya usafi wa maji na afya.

Kwa sasa Dr Hilonga ni mmiliki wa kampuni ya Gongali Model ambayo Jina hilo ni Jina la kijiji alipozaliwa yaani kijiji cha Gongali wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

gongalimodel.com | Empowering Tanzanians; YES, WE CAN

Makao Makuu ya Kampuni hiyo yapo Njiro – Nane Nane mkoani Arusha unaweza watembelea kujifunza zaidi au kujipatia mtambo huo Kwa ajili ya Biashara au Familia yako.

Unaweza mpata na kumfuata katika twitter na facebook pia kwa kutafuta jina Akwar Hilonga au kusoma zaidi katika mtandao wa kampuni inayosambaza mitambo hiyo yaGongali Model.

Source : Askwar Hilonga-Mbunifu anayeokoa mamia ya watanzania Kwa kubuni Kifaa cha Kuyafanya maji yawe safi na Salama!

Kuhusu Tuzo unaweza Pata maelezo kamili hapa... Engineering for clean water across Africa – Tanzanian entrepreneur wins first Africa Prize for Engin - Royal Academy of Engineering
 
Safi sana, Tunaweza fahamu huyu ndugu ana PhD ya field ipi?
 
Safi sana, Tunaweza fahamu huyu ndugu ana PhD ya field ipi?
Chemical Engineering mkuu Kwa taarifa nilizonazo... Ni Senior Lecturer Kwa sasa chuo cha Nelson Mandela Arusha
 
Chemical Engineering mkuu Kwa taarifa nilizonazo... Ni Senior Lecturer Kwa sasa chuo cha Nelson Mandela Arusha

Sawa ni vyema sana kutumia ujuzi wetu tuliopata vyuoni kunufaisha jamii haswa watu tuliosoma course za sayansi, Nampongeza sana kwa kweli
 
Sawa ni vyema sana kutumia ujuzi wetu tuliopata vyuoni kunufaisha jamii haswa watu tuliosoma course za sayansi, Nampongeza sana kwa kweli
Sana mkuu. Tatizo watu kama hawa hata hawajulikani. Nchi imekalia siasa tu...
 
Huo si ugunduzi.

Isitoshe Tanzania hata mbwa anaweza kuwa rais akipigiwa kampeni na CCM.

Tushakuwa na mtu ana uwezo mdogo kuliko mbwa na kashawahi kuwa rais.

So pick something else.
I better stay silent!
 
hizo 97% za vijidudu vilivyotajwa ni vijidudu kama mbu na wadudu walukao wanaofia ndani ya maji ama amei Include na wadudu kama Bacteria nafikiri 3% ya bacteria sio haba bado waweza kupatwa haja kubwa nyepesi!

Itabidi maji yalochujwa na hicho kifaa chake yakafanyiwe Culturing ya micro organisms kwenye Agar ili kujiridhisha kama hapatakuwepo na bacteria wa kutosha kuweza kushambulia guts za wa TZ!
 
Nimefika ofisini kwake.. Nimeona idara ya maji wamethibitisha...
 
Nimefika ofisini kwake.. Nimeona idara ya maji wamethibitisha...
Muulize google anaulizia hayo maji baada ya kuwa filtered yanakuwa salama au safi tu!?

Maji salama ,,, lazima uangalie content ya dissolved oxygen, cl, acid, alkali, dissolved residual, ca, nk... Filtering ni process ya mwisho kabisa kabla ya maji kuwa treated,,msaada zaidi atembelee water treatment plant iliyo karibu naye.
 
Safi na Salama.. Sikiliza Kwenye hiyo video hapo juu...
 
Naona haina tofauti sana na LifeStrew. Sasa hivi technology kupata maji salamu zipo nyingi watu wahimizwe kutumia wasiugue cholera.
 
Safi na Salama.. Sikiliza Kwenye hiyo video hapo juu...
Mkuu siyo salama, filter ni chujio, chujio linachuja maji ila halitibu maji, nimesiliza ila muulize tu.
 
nilicheki clip zake zinazo zungumzia project yake huko kwao kijijini. wakati nipo arusha wakati fulani kupitia kwa Dr. Muneja ambaye ni lecturer pale UOA

NINGESHAURI PIA APANUE HUO MRADI AKACHUJE MAJI YA PALE ARUMERU ambayo si salama kwa mifupa.
 
Ukweli... Ni uvumbuzi mzuri
 
Kuna siku alihojiwa na akasema his education means nothing to him if it can't serve his own people. Ni mtu mmoja very focused and determined. Alishinda ile BBC challenge ya innovation kwa kutumia hii innovation yake ya filter ya maji. Namkubali sana
 
Back
Top Bottom