Askofu Zakaria Kakobe: Tanzania siyo nchi ya chama kimoja! Amtaka Rais Magufuli atubu

Muda upi tena kama sasa ni zaidi ya miaka 50 na ndiyo kwanza kama wamezaliwa mwaka 2017....kwa watanzania hawa hawa na ipinzani huu huu, tutasubiri sana huo muda.
Utafika tu kama ulivyowafikia akina Mugabe Mobutu kamuzu Banda gadaff na uchwara wengine wote waliokutangulieni
 
Mleta mada yaelekea hajui namna ya kupinga hoja. Amepoteza muda kuelezea mapungufu ya Kakobe kuliko kujibu hoja. Hoja ya msingi ya Kakobe ni juu ya Rais kutopenda kukosolewa, hajaijibu mahali popote hoja hiyo. Huu ndiyo unaitwa utetezi wa kipuuzi. Na huyu kama kazi yake ni kumtetea Rais, hafai hata kidogo maana uwezo wake wa kujenga hoja ni mdogo mno.
 
Straight crap. Kwanini kila anayemchallenge magufuli mumtafutie weakness zake. Ukiamua kuwatumikia watu lazima tuhoji kila kitu na ndo sababu uko hapo.
 
Kwa kitendo cha kuweka jina tu inaonekana andiko halina nia njema bali ni la kujipendekeza zaidi kutafuta huruma au grisi
 
Kiongozi wa dini kuongea huu utumbo ni ishara ya kuchanganyikiwa...yeye anapaswa kufundisha watu wasitukane...baadalayake, ana justify rais kutukanwa simply because hata Mungu anatukanwa?? Plain stupid...
 
bora kakobe hajawahi kutuma watu fulani wakampige risasi Tundu Lissu wamuue
 
*ASKOFU KAKOBE AJIPE MUDA KUTAFAKARI ...*

*Na Shilatu E. J*

Nimesoma mitandaoni maneno anayosadikiwa kuyasema kiongozi mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) lililopo Mwenge, Askofu Zakaria Kakobe akimsakama Rais Magufuli kwa maneno mazito na kumtaka atubu. Lahaula!

Nimebaki nikijiuliza kati ya Rais Magufuli na Askofu Kakobe nani anatakiwa atubu?!. *Askofu Kakobe anatakiwa aanze kutubu yeye* kwa sababu:-

1. Mwaka 1995 aliwaaminisha Watu kuwa Augustine Mrema atashinda urais na kuingia Ikulu. Kakobe alidai amepewa maono hayo lakini mwisho wa siku Mrema aliangushwa vibaya na Benjamin Mkapa akashinda urais. Kakobe ulishatubu juu ya hili?

2. Kakobe huyu huyu akaibuka tena 2015 akasema Mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa atashinda urais lakini akaishia kupata aibu nyingine ya Mgombea wake huyo kushindwa urais. Kakobe hakuwahi kutubu dhambi hii ya kuwadanganya Watanzania.

3. Kakobe aliwahi kuwaambia waumini wake umeme uliopita juu ya kanisa lake hautakaa ufanye kazi. Mpaka kesho umeme huo unafanya kazi. Kakobe alitakiwa aendelee kutubu tu kwa dhambi hii ya kuwadanganya mpaka waumini wake.

4. Kakobe huyu anayemvaa na kumrarua Rais Magufuli kwa maneno makali anatakiwa kuanza kutubu yeye maana ameshindwa kuheshimu mamlaka ya hapa Duniani wakati kwenye kitabu kitakatifu cha Biblia Mwenyezi Mungu amewaagiza Wanadamu kuheshimu mamlaka za hapa Duniani na za Mbinguni lakini huyu anayejiita Askofu Kakobe ameshindwa kulitambua na kuheshimu hili. Kakobe nenda katubu kabisa kwa kushindwa hata kuheshimu mamlaka, kuitii Biblia na kuheshimu agizo la Mwenyezi Mungu.

5. Kakobe huyu huyu anatakiwa atubu kabisa kwa kuanza kuhubiri siasa kanisani tena Madhabahuni (sehemu takatifu) badala ya kuhubiri neno la Mungu, kuhubiri Biblia inasemaje na kumuhubiri Mwenyezi Mungu. Kitendo cha kutelekeza neno la Mungu na kuvaa uanasiasa si tu kuwagawa Waumini wake bali pia ni kutikisa misingi ya amani ambayo imejengwa kwa gharama kubwa za jasho, mateso na kujitoa kwingi kwa Waasisi wetu. Kakobe nenda katubu kwa uchochezi huu.

Askofu Kakobe alitakiwa ajipe muda wa kutosha wa kufikiri juu ya matendo yake na kauli zake kabla ya kuzitoa madhabauni. Alipaswa kujifunza faida na hasara zake.

Askofu Kakobe alitakiwa aendelee kujifunza juu ya mwelekeo wa Tanzania Mpya na mwelekeo wake Mpya kwa sasa. Tanzania mpya ya sasa inayoongozwa na Rais Magufuli haina muda wa siasa za chini ya Mwembe tena.

Kwa Wahubiri wanasiasa kama Kakobe watamuona Magufuli ni tatizo ila kwa Watanzania Wazalendo tunamuona Rais Magufuli ni Mkombozi kwa Taifa letu. Tunamuona Rais Magufuli ndiye Mussa wa Watanzania wetu kwa sasa anayetutoa Misri kwenye mateso, anatuvusha bahari ya Shamu na kutupeleka Kaanani, nchi ya Maziwa na Asali. Daima sisi Watanzania wanyonge tutaendelea kumuunga mkono Rais Magufuli siku zote, nyakati zote.

*Na Shilatu E.J*
Cheap.
Sijaona ukijibu hoja zake unamuattack yeye personally tu.
 
Unajua Askofu kakobe anajijua uaskofu aliupataje kitapeli Askofu wa kiukweli angekuwa na uhusiano nzuri na Askofu wa Magufuli ambaye ni kardinali lengo akiwa na jambo angeenda kuongea na Askofu wa Magufuli Pengo na kumnongoneza kitu akamnongoneze muumini wake Magufuli .ninachokiona kuna maaskofu immature Ndani ya katoliki ,Lutheran,akina gwajima ,kakobe nk ambao hawajui majukumu ya uaskofu ni yepi na ukiwa na jbo na muumini wa kanisa lingine lisilo lako unatakiwa ufanyaje.shame on them all
Kwa mujibu wa Biblia, Askofu ni Mwangalizi wa Kanisa.

Kanisa analoliongoza Kakobe lina matawi zaidi ya 100 nchi nzima, naye ndiye Mwanzilishi (Founder) na Mwangalizi wa hilo kanisa, hivyo kuitwa Askofu ndipo stahiki yake.

Utumishi wa Mungu Aliye Juu haupo katika syllabus na mitaa ya kiteolojia, Utumishi huu ni wa Roho Mtakatifu mwenyewe. Aliyepewa maono ya kazi hupewa na karama za uongozi.
 
Mleta mada wewe ni msukuma SHILATU=YEBOYEBO, nawe umetoka kolomije juzi umefika hapa dar kupiga vibarua sasa unataka uteuzi! Kipengele cha nne kwamba kakobe aheshimu mamlaka za duniani mfano, mamlaka za akina Mussolini, Hitler, Pinochet, archduke, za akina kolomije ni za kuheshimu? Mbona unasoma baibo kama gazeti la sani? Hivi tawala za kipuuzi kama tajwa hapo ukiziheshimu si hata Mungu atakuona mwehu? Nafasi za uteuzi zilisha isha ulikuwa wapi? Au ndo umepata nauli juzi? Bila shaka umefika dar kwa kutumia magari yiliobeba ng'ombe wa Xmas kutoka ikungulyabashashi kuja dar sasa umevamia jamii forum! Kinehe lolo ngosha au fulushi la michembe limeisha
 
Wewe akili zako itakua zmechanganyika na mavi katika dunia hii kila binadamu anakosea lakn aina maana kama akikosea atakiwi kukosoa!
 
Duh hebu jitafakari upya kwa ulichoandika wew kwanza... Maana mtu anazungumzia raisi wa Tanzania we unawazungumzia watu wasio na vyeo kitaifa... Au umekula ugali leo
 
Kiongozi wa dini kuongea huu utumbo ni ishara ya kuchanganyikiwa...yeye anapaswa kufundisha watu wasitukane...baadalayake, ana justify rais kutukanwa simply because hata Mungu anatukanwa?? Plain stupid...
Hajafundisha watu watukane bali anawafundisha watawala wawe wavumilivu na matusi kwani matusi hayampunguzii mtawala hata sehemu ndogo ya madaraka yake.
 
Kiongozi Wa dini akimsifia sizonje hiyo sio siasa lkn akimponda tuu hiyo tayari ni siasa nyie watu wa namna gani nyie,
 
Hajafundisha watu watukane bali anawafundisha watawala wawe wavumilivu na matusi kwani matusi hayampunguzii mtawala hata sehemu ndogo ya madaraka yake.
Hiyo ni tafsiri yako...naiheshimu...ila mimi tafsiri yangu ni ana justify matusi..
 
Back
Top Bottom