Askofu: Uchaguzi kushangaza mwaka huu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu: Uchaguzi kushangaza mwaka huu!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtaka Haki, Oct 1, 2010.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna Askofu mmoja huko Moshi alisema kuwa uchaguzi mkuu mwaka huu utashangaza na kama haitakuwa hivyo basi yuko tayari kupigwa mawe.
  Nakubaliana naye na hapa kuna mengi ya kuangalia.
  Ndio mwaka pekee ambao CCM kuliko vyama vingine vyote vimkumbwa na kamata kamata ya takukuru.
  Wengine wamesema kuwa Karibu mkuu Makamba ndiye chagua la Mungu kipindi hiki kwa ajili ya kuimalizia CCM.
  Yaani amekuwa kila maamuzi anayoyatoa yanaingamiza CCM. Nitatoa mifano.
  1. Kuwaruhusu wanachama wenye kadi hata kama ni mpya apige kura za maoni. Wenye kadi walizotengeneza walifaidika.
  2. Kuwanyima wagombea kutokushiriki mdahalo. Wapinzania wamepata angalao fursa ambayo wabunge wa CCM hawana.
  Kikwete naye anatabiri kumalizia kipindi chake.
  1. Dr. Slaa alisema wakati mwisho wa uongozi wa mtu ukifika Mungu huachia useme mwenyewe kumalizika kwako. ( Alisema hataki kura za wafanyakazi) Hapa wafanyakazi ni pamoja na nyie polisi, Usalama wa taifa, Wasimamizi wa uchaguzi, Mahakimu, Wakuu wa wilaya, Msajili, waalimu,nk.
  Wengine wanaweza kutafsiri kuwa anataka za wale wasiofanya kazi yaani wanaotumia jasho la wengine bila kazi?
  2. Anawashambulia wagonjwa wa ukimwi na kusema ni kiherehere chao.
  Watu wengine wasio na busara wanaweza kusema kuwa anafanya hivyo kisaikolojia kuficha kitu fulani. Kwani washauri wangeshamnyima kuendelea kusema hivyo. Niliwahi kusikia kisa cha watu wawili waliokuwa wakivusha magendo. Mmoja alipokamatwa mwingine akamwendee yule aliyekamatwa na kumshambulia juu ya ubaya wa magendo na anathubutuje kufanya magendo.
  Ilikuwa ni vigumu kwa polisi kudhani kuwa huyo aliyekuwa anafoka anaweza kuwa na magendo.
  Hivyo ameacha kuona hilo wanaloweza kufikiri watu.
  3. Kuanguka siku ya kwanza ya uzinduzi yaweza kuwa ishara toka kwa Mungu ya kuanguka nafasi yake ya uraisi.
  4. Kushindwa kuheshimu watanzania angalao hata kwa unafiki na kujiweka mbali na wenye tuhuma zinazochukiwa na watanzania na hata kuwapigia debe ni ishara ya kuanguka.
  Kushindwa kukemea wanaonunua uongozi na hata baadhi ya waliopita bila kupingwa kuiharibu demokrasia kwa kutumia umaskini wa watanzania ni ishara ya kuonyesha wananchi na Mungu anavyoweza kushangaza wenye jeuri mwaka huu.
  5. Kuwasimamisha washirikina waliofika drs la saba huku umaarufu wao ukiwa ni ramli, kugombea ubunge na kusifiwa na rais hiyo ni ishara nyingine kuwa busara imepotea au wanausalama wamekubali kumnyima kura zao.
  Ni vizuri akaendelea kupewa heshima na kuagwa vizuri kila anakopita mpendwa raisi wetu.
   
 2. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Ni kweli yule askofu alitoa msisitizo kwamba mgombea yeyota atakaetegemea ushindi kupitia kwa sangoma hatashinda na kama akishinda basi apigwe mawe. Jk ameagiziwa majini ya kumlinda dhidi ya wapinzani wake na mnajimu Yahaya na hatujamuona popote akikanusha kwamba hana mafungamano na huyu sangoma. Sasa tujiulize askofu atapigwa mawe ama Jk hatoshinda?
   
 3. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Nina wasiwasi kuwa huyo askofu huenda atapigwa mawe. Sisemi hivyo kwa sababu JK atashinda, ninasema hivyo kwa sababu JK lazima ashinde kwa nji ayoyte ile, au niseme lazima atangazwe mshindi!!!.

  Jk ni mtu hatari sana, na sijui kwa nini Mkapa hakuliona hilo, but duru zinasema kuwa Mkapa alitishwa sana. JK alitaka kuingia madarakani kwa njia yoyote ile, alianza kufyeka vikwazo toka mwanzo, marehemu Dr Omari, ambaye ukweli he was the best candidate kuwa mrithi wa Mkapa kuliko JK. Omari akakatika kama mua wa kondeni. Watu kama kina SAS, Sumaye, Malecela, Mwandosya walivunjwa vunjwa isivyo kawaida, na SAS aliyeonekana dhahiri kuwa tishio akazushiwa kashfa mbaya. JK aliutaka uraisi kama sijui nini-- lazima tujiulize kwa nini aliutaka na hata sasa baada ya kufail for the last 5 years, bado anautaka kwa udi na uvumba? Haogopi kutumia hata ushirikina kuhakikisha kuwa anautaka. Huyu ni mtu hatari sana kwa mstakabali wa taifa letu!!

  So atatumia nguvu zile zile alizotumia kuwanyamazisha wapinzani wake 2005, kuchakachua kura. This time atatumia jeshi la wananchi wa tanzania, kwa kuwa polisi na usalama wa taifa inaelekea wameshasoma mazingira na wanajua kuna hofu. In all these years, sikuwahi kusikia kutoka nchi yoyote jeshi likiingilia mambo ya uchaguzi na kuwataka wagombea wakubali matokeo. Kazi ya jeshi ni kulinda nchi nje ya mipaka yetu, mambo ya ndani na fujo baada ya uchaguzi ni kazi ya jeshi la polisi.

  So huyo askofu atapigwa mawe kwa kuwa mgombea atakayeshindwa ambaye ni JK ndiye atakayetangazwa kuwa ameshinda! Pole sana askofu wetu, lakini moyoni umeshinda kabisa
   
 4. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  .
  Mkuu sitaki kuamini kwamba yule askofu alikuwa anacheza na akili zetu, na kama basi haikuwa hivyo basi maana yake ni kwamba Mungu alizungumza na askofu. Na kama Mungu alizungumza na askofu, ni dhahiri kwamba neno lile alilompa ni hakika nalo limethibitishwa. Jk aliwasukumia mbali wapinzani wake wote wakati ule ila hana ubavu wa kumsukumia mbali Muumba. Kuna njia moja tu yake kuokaka,ama ajitoe kabisa katika kuwategemae wachawi au afanye shingo yake kuwa ngumu ili apime kama Mungu hutawala pia duniani.
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  na iwe hivyo
   
 6. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anategemea Watanzania wapiga kura kwa mujibu wa maelekezo ya MWONGOZO wa Kanisa. Lakini hivyo haitatokea. :tonguez:
   
Loading...