EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,709
- 35,702
Tunamshukuru Mungu kwamba umerudi katika maisha haya. Naungana na wengine kukupa pole. Hukurudi kwa ajili ya wema na huruma ya watekaji na watesi wako bali umerudi kwa huruma na kusudi la Mungu. Unapaswa kumshukuru sana Mungu na kamwe usimuache. Pia wakumbuke kwa moyo wa shukrani wale wote waliokuombea na kupaza sauti zao ili uachiliwe huru. Ni furaha na faraja iliyoje kwamba siku moja sote tutakufa na kusimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mfalme wa wafalme! .
Ulipokuwa mikononi mwa watekaji na watesi wako hukuwa na thamani. Kwa kuwa hukuwa na thamani basi kwa vyovyote waliburudisha mioyo yao kwa kukufanyia walivyotaka. Wao walikuwa na malengo yao na bila shaka njia zozote za kutimiza malengo hayo zilikuwa halali. Ujue kwamba mateso yako, maumivu yako, kilio chako na machozi yako ndio ilikuwa furaha yao. Nakupa pole sana.
Watu hao waliokuteka na kukutesa hawajulikani lakini wapo hapa duniani na pengine tunapishana nao mitaani. Njia walizotumia kukuteka na kukurejesha inaonyesha kuwa wanafanya kazi nje ya mfumo na taratibu za kisheria ndio sababu hawakukurejeshea hospitali. Wapo wengine wanaotajwa kwamba nao walitekwa na hadi leo hawajapatikana. Ungana na wale wanaoendelea kuwaombea watu hao kwamba katika mateso, maumivu na machozi yao Mungu asimame upande wao.
Bila shaka unayo mengi ya kusimulia lakini kila simulizi yako uimalizie kwa kumshukuru Mungu. Ninamuomba Mungu akupe kupona na kusimama tena. Pia tafuta sana makusudi ya Bwana kukurejesha toka tundu la simba. Bwana Yesu anatuambia tuwaombee wanaotuudhi. Wewe waombee wala usiwalaani kwani ukifanya hivyo utakuwa umewapalia makaa ya moto vichwani mwao. Hata sasa usidhani kwamba waliokufanyia haya wana amani na furaha mioyoni mwao. La hasha! Damu na uhai wa mwanadamu sio mali ya mtu awaye yote bali ya Mungu. Kucheza na hivyo kinyume na sheria za nchi ni kuingilia himaya ya Mungu. Kwa hiyo wewe huhitaji kuwalaani kwani watekaji na watesi wako walikwisha kujilaani wenyewe. Jambo moja ambalo napenda kukuhakikishia ni kwamba: mateso yako, maumivu yako, uchungu wako, na machozi yako vitabaki kuwa kumbukumbu madhabahuni mbele ya kiti cha enzi cha Mungu aliye hakimu wa haki. Hivyo vitabaki kuwa kumbukumbu mpaka wale wote waliofanya hayo watakapokuja kusimama mbele za Mungu BWANA. Amani iwe nawe Mdude Chadema.

.