MCHAPAKAZZ
Member
- Mar 29, 2016
- 31
- 18
Ikiwa wanajimbo wa Geita wakielekea kusherekea kusimikwa kwa Askofu mteuliwa Askofu Kassala ni vyema kukumbuka kazi kubwa ilofanywa na Askofu Renatusi alipokuwa msimamizi wa jimbo lao,kwa kuhakikisha anatetea matakwa ya Wanageita ya kumpata Askofu anayekidhi vigezo vyao.
Maaskofu wengi wanapochaguliwa kuwa wasimamizi wa majimbo yaliyowazi mara nyingi wamekuwa hawashikamani na wanajimbo husika kutatua matatizo waliyonayo, lakini Askofu Nkwande alihakikisha anajitoa muhanga kuwatetea wanageita ingawa kazi ilikuwa ni nzito. Leo hii Wanageita wapo katika furaha ya kumpata Askofu atakayewatetea na kuwajenga kiimani.
Naomba huu uwe mfano kwa maaskofu wengine wanaopewa nafasi ya kuwa wasimamizi katika majimbo mbalimbali yanapokuwa wazi kwa sababu tofauti tofauti. Tunaomba wawe mstari wa mbele kutatua matatizo wanayoyakuta, huo ndo utakuwa utume sahihi. Leo hii Wanajimbo wa Mbulu wapo katika maombi na jitihada za kumpata Askofu atakayewasaidia,lakini yule aliyepewa nafasi ya kuwasimamia(Askofu Amani wa Moshi) amekuwa mstari wa mbele kukwamisha mahitaji ya wanambulu.
Juzi viongozi wa Mbulu walimfikia mwakilishi wa Baba mtakatifu kuwasilisha maombi na mahitaji yao,Amani akatamka kuwa mipango yake imekwama je hiyo kauli inamaana gani? Hivi sasa Kina Amani, Askofu Ruwaich na Askofu Pengo wanamshawishi Mwakilishi wa Baba mtakatifu amtangaze Marcus Paul Mjokoti Wa Ifakara awe Askofu wa Mbulu jee wana nia gani?
Wanageita hongereni sana ila waombeeni wengine wenye uhitaji wa Askofu mwenye sifa.