Askofu Nzigilwa: Rugemalira alitoa fedha za matoleo

..maaskofu kama hawa wanachangia sana waumini wao kuwakimbia...mimi siwezi kuhudhuria misa inayoongozwa na huyu nzigilwa ama yule kilaini..never....wawadanganye waumini wanaofaidi hela zao...Inasikitisha sana...alafu unakuta radio Maria ya Roman wanalialia kila siku kuomba hela kwenye mitandao...wakichangisha watu hadi sh.100....leo maaskofu wao hawa wanapitishiwa mabilioni ya sh kwenye account zao...sasa hiki nini???sijasikia hawa maaskofu wakichangia hata senti huko radio maria....leo wanataka sisi waumini tuwasikilize na kuwaamini wasemayo????never.....wizi nchi hii huko kila mahali...inasikitisha hadi makanisani....sasa watu wakimbilie wapi???...so sad....
 
Unapoongelea sadaka kanisani uko nje ya alichokitoa Rugemalila, kama ndivyo akina Ngeleja, Tibaijuia na wengine ilikuwa form ya sadaka kanisani au shughuli za maendeleo katika majimbo wanayowakilisha? Namna alivyowekewa pesa askofu kwenye account yake vivyo hao wengine waliwekewa kwa hoja kama aliyosema Tibaijuka shughuli za maendeleo ya ujenzi wa shule jimboni kwake. Watu macho futu kwa Askofu kukazania sadaka na ninyi ndio mnaopeleka watoto wenu kwenye shule zinazojengwa na pesa za wahisani, mnaoenda kwenye hosptali zilizojengwa na pesa za wahisani waliotoa kama livyofanya Rugemalila.

Wote naona ni kulalamika tu wizi, money laundaring lakini hakuna anayechambua na kuonyesha wizi sipo tayari kuw amtumwa wa mambo ya kufikirika bila hoja ya kujenga kuonya wizi ulivyofanyika.

CC; Nguruvi3, TAU 1,
Munabusule, Mwanamayu, SMU

Ukiongelea 'matoleo' ni Kanisani wakati wa Misa. Kuna namna zifuatazo za kumtolea Mungu: zaka, vipaji, matoleo/ sadaka, malimbuko, mavuno/ shukurani. Ni vyema ukatoa maana ya matoleo unayoifahamu wewe na ndio anayoifahamu Askofu Nzigilwa.

Kama hizo fedha hazikuwa za wizi wizi kwa nini akina Werema wame-resign? Kukosa maadili?

Halafu pattern inaonesha bila hii issue kuweka hadharani pesa zile zisingeingia huko wanakodai zingeenda - Askofu akaunti binafsi badala ya Jimbo, Prof. Tibaijuka akaunti binafsi badala ya shule (masharti ya mtoaji).

Nakubaliana na wewe kuwa jambo la msingi ni ku-simplify jinsi wizi ulivyofanyika, halafu na wale wa benki nyingine tuwafahamu pia, na kiasi walichopokea, na sababu za kupata huo mgao. Panya Road hawajaingia barabarani hivi hivi tu bali wanaendeleza walichofanya Escrow kwa namna na scale tofauti.

Usimtetee Askofu Nzigilwa kwa sababu ni Askofu kwani ni binadamu na lolote laweza kufanywa na hawa watumishi wa Mungu, hivi nani alitarajia kama Yuda Iskariote angevuta mlungula kumtoa Christ (ili ni la Kiimani zaidi, kama sio wa Imani hii chukua mfano tu!).
 
Mkuu kwahiyo akikudhibitishia kwamba pesa hizo amezitumia katika shughuli za maendeleo ya kanisa utaridhika?.Huyo Pengo ulimuuliza akakuambia kwamba hanataarifa na hizo pesa?. Achakufuata upepo tafakari upya, kanisani we unamfuata askofu au ibada?.
Read the Bishop's statements in the media between the lines. You seem to be bankrupt upstairs. Your comments are simply offroad. Akili za kuambiwa changanya na za kwako. La sivyo, kaa kimya badala ya kurusha -----!
 
Unajua utaratibu, uwajibikaji, na utoaji matamko kwenye media kwa watujishi wa kanisa katoliki au unaongea tu unachofiria wewe unavyoona bila kujua taratibu zao?
 
Ukiongelea 'matoleo' ni Kanisani wakati wa Misa. Kuna namna zifuatazo za kumtolea Mungu: zaka, vipaji, matoleo/ sadaka, malimbuko, mavuno/ shukurani. Ni vyema ukatoa maana ya matoleo unayoifahamu wewe na ndio anayoifahamu Askofu Nzigilwa.

Kama hizo fedha hazikuwa za wizi wizi kwa nini akina Werema wame-resign? Kukosa maadili?

Halafu pattern inaonesha bila hii issue kuweka hadharani pesa zile zisingeingia huko wanakodai zingeenda - Askofu akaunti binafsi badala ya Jimbo, Prof. Tibaijuka akaunti binafsi badala ya shule (masharti ya mtoaji).

Nakubaliana na wewe kuwa jambo la msingi ni ku-simplify jinsi wizi ulivyofanyika, halafu na wale wa benki nyingine tuwafahamu pia, na kiasi walichopokea, na sababu za kupata huo mgao. Panya Road hawajaingia barabarani hivi hivi tu bali wanaendeleza walichofanya Escrow kwa namna na scale tofauti.

Usimtetee Askofu Nzigilwa kwa sababu ni Askofu kwani ni binadamu na lolote laweza kufanywa na hawa watumishi wa Mungu, hivi nani alitarajia kama Yuda Iskariote angevuta mlungula kumtoa Christ (ili ni la Kiimani zaidi, kama sio wa Imani hii chukua mfano tu!).

Matolea yapo mengi na ya aina mbalimbali, tunachoongelea sasa ni pesa ya Lugemalila na uhalali wa pesa hiyo kuwagawia wahusika kwa shughuli za maendeleo. Naendelea kusema mnakazana na kulalamika kwamba pesa ni chafu bilak ueleza na kufafanua kinaganaga cha uchafu huo ni dhahiri mmeshindwa hoja dhini ya hoja zangu kwamba pesa si ya wizi kwa vile ni gawio halali la ubia wa Rugemalila tokana na mtakaba wa kuiuzia tanesco umeme. Mahakama chombo ha haki liliridhia na banki ya mkombozi ilikokotoa kwa kukata kodi pesa hizo hivyo ni halali. Hamna hoja ila ni kulalamika tu bila hoja.
 
..maaskofu kama hawa wanachangia sana waumini wao kuwakimbia...mimi siwezi kuhudhuria misa inayoongozwa na huyu nzigilwa ama yule kilaini..never....wawadanganye waumini wanaofaidi hela zao...Inasikitisha sana...alafu unakuta radio Maria ya Roman wanalialia kila siku kuomba hela kwenye mitandao...wakichangisha watu hadi sh.100....leo maaskofu wao hawa wanapitishiwa mabilioni ya sh kwenye account zao...sasa hiki nini???sijasikia hawa maaskofu wakichangia hata senti huko radio maria....leo wanataka sisi waumini tuwasikilize na kuwaamini wasemayo????never.....wizi nchi hii huko kila mahali...inasikitisha hadi makanisani....sasa watu wakimbilie wapi???...so sad....

Unacholalamika nini? Chambua hoja kuonyesha uchafu wa pesa hizo ndiovyo great thinker tunavyofanya, malalamiko tumeyachoka ni dalili ya kuishiwa hoja.
 
kwayo ikigundulika zilikuwa pesa za wizi itakuwaje kwa kanisa?

Itagundulika lini wakati vyombo vyote husika vimefanyia kazi suala hili hadi mahakamani na kuishia kuhukumu pesa walipwe wabia wa kuiuzia tanesco umeme na ndicho kilichofanyika, nini zaidi?
 
wakatoliki popote walipo Tanzania lazima waelewe kuwa kuna Mwizi kaiba pesa ya umma, baada ya kuiba akaamua kutapanya pesa hiyo kwa kugawa hovyo.mmoja wa wanaufaika ni maaskofu wawili wa kanisa katoliki.Watanzania wanadai haki yao.Maaskofu hawa wamesikia watanzania wakilalamika kuwa pesa zao zimeibiwa na zikatapanywa.Nashangaa hadi sasa maaskofu wale Bado Somo halijaeleweka kuwa zile Pesa ni za umma!!!!! Jamani wanataka kusikia maneno gani ili waelewe,Bunge wameshindwa kulielewa, Vyama vya siasa wameshindwa kuvielewa, asasi za kiraia zimesema hawakuelewa.
Hawa maaskofu watamsikiliza nani wa kuwaelewesha waelewe kwamba lile ni jasho la watanzania limeporwa??????!!!!
Kwa kweli inakatisha tamaa kuwa na viongozi hawa

Ni kweli kanisa hili limekubaliana na maelezo ya hawa maaskofu, kwamba pesa hii chafu iwe sehemu ya bajeti ya Kujenga kanisa la Mungu,kujenga hospital za kanisa, kujenga shule za kanisa.Ngoja tusikilize mwisho wa hii mambo ndani ya kanisa kama itakubalika kama ni UTUKUFU

Ufafanuzi upi uliotolewa na bunge kwamba pesa ni za umma?
Ludovic wiki moja iliyopita alisema ndani kulikuwa na pesa za umma ambazo ni kodi, bank ya mkombozi ilikata kodi kwa pesa hizo, hata Mwigulu alieleza kwamba kodi lazima ilipwe tokana na pesa hizo, hivyo waliopata pesa hizo kupitaia benk ya mkombozi pesa zao halali kwa vile zilikatwa kodi.

Fafanua yakhe wizi ulivyotokea katika pesa hizo balada ya kuendelea kulalamika tu pesa ni za wizi, ni mhemuko usio na maana na mwisho kuishia kupata BP bila sababu.

Ninachofahamu jambo muhimu watanzania ni watu wenye wivu sana.
 
Read the Bishop's statements in the media between the lines. You seem to be bankrupt upstairs. Your comments are simply offroad. Akili za kuambiwa changanya na za kwako. La sivyo, kaa kimya badala ya kurusha -----!

Statement imeelezea jinsi alivyopata hizo pesa na jinsi zinavyo tumika, sasa kitugani ambacho hakieleweki, we na wenzako mmeng'ang'ana kusema tu pesa ni za wizi na askofu ni mwizi, ukiambiwa udhibitishe,unasema bankrupt upstair, unataka tuanze matusi kama wewe badala ya kutoa hoja za maana? Mimi sitatukana coz i don't wanna be idiot.
 
Candid Scope amekuwa burudani tosha kwangu kwenye thread hii. Hawa maaskofu hawasafishiki tena inawezekana huyu Kilaini alikula rushwa ya wanamtandao mpaka akatudanganya wafuasi wake eti Kikwete ni chaguo la mungu. Sasa Mungu mwenyewe original hadhiakiwi ona nchi ilivyopigwa laana.
 
Last edited by a moderator:
Unacholalamika nini? Chambua hoja kuonyesha uchafu wa pesa hizo ndiovyo great thinker tunavyofanya, malalamiko tumeyachoka ni dalili ya kuishiwa hoja.
..sikutaka kukujibu lakini imenibidi...

..wewe kwangu sio great thinker...kama unajiona hivyo basi kwangu sivyo.....Nakuona unavyohangaika kumtetea askofu wako...unajidhihirisha ulivyo na maslahi binafsi kwenye jambo hili....We kama hadi leo kwenye kashfa hii ya escrow hujaona kosa la hawa maaskofu kuingiziwa mabilioni ya fedha (zilizotokana na escrow account)kwenye acc.zao..basi wala haina haja kukujibu..

...Unauliza kuonyeshwa uchafu wa hela!!inaonyesha we wala hujui dhana ya kutakatisha fedha...na iweje fedha za misaada/sadaka iwekwe kwenye account zao na si taasisi zao??utasema walipewa sharti hilo...we unajua kwanini walipewa sharti hilo??....Malalamiko umeyazoea??yani watu tukiona ushenzi tusilalamike??are you out of your mind???tukae tu kimya wakati tunaona kinachofanyika sicho??..we jamaa unaishi TZ kweli???

...Btw..nimeona huko kwenye post zako nyingine unasema eti tunalalmika wakati tunapeleka watoto wetu kwenye taasisi za dini/Roman!!...ndio tunawapeleka ...kwani tunawapeleka huko bure?????Kuna taasisi ya dini inasomesha watoto bure nchi hii???..hata waumini maskini hawaendi kanisani bila sadaka.usitake kutuchefua hapa we.....Unajiita thinker!!!my foot!! watu makini hawatambi bana....acha ujinga...
 
Ufafanuzi upi uliotolewa na bunge kwamba pesa ni za umma?
Ludovic wiki moja iliyopita alisema ndani kulikuwa na pesa za umma ambazo ni kodi, bank ya mkombozi ilikata kodi kwa pesa hizo, hata Mwigulu alieleza kwamba kodi lazima ilipwe tokana na pesa hizo, hivyo waliopata pesa hizo kupitaia benk ya mkombozi pesa zao halali kwa vile zilikatwa kodi.

Fafanua yakhe wizi ulivyotokea katika pesa hizo balada ya kuendelea kulalamika tu pesa ni za wizi, ni mhemuko usio na maana na mwisho kuishia kupata BP bila sababu.

Ninachofahamu jambo muhimu watanzania ni watu wenye wivu sana.
Unajaribu sana kujenga utetezi ukiacha masuala muhimu sana.

1. Kama pesa ni za halali, Tibaijuka,Werema, Maswi Wameonewa au la. Na kwanini
2. Je, Rugemalrila aliuza umeme kulingana na mkataba wake? Kama hakufanya hivyo, je hapo hakuna wizi?
3. Askofu aliingiziwa pesa kwenye account binafsi. Je kanisa lina taarifa hizo?
4. Unapowaweka akina Ngeleja, Werema, Chenge na Nzigilwa kwa pamoja, unapata picha gani
5. Kwani kusomesha watoto katika makanisa kunondoa dhambi ya wizi wa ada iliyopitakana kwa njia haramu?
6. Nafasi ya Nzigilwa, inaruhusu achukue pesa zenye utata kama hizi? Na je alijua ni halali? Na sasa anaweza kusimama na kutuambia pesa zile ni halali?
 
Tatizo wengi wetu hawajui taratibu za uhasibu. Jimboni kuna mhasibu mkuu wa jimbo ambaye anasimamia hazina ya jimbo. Ndani ya hazina kuna account mbalimbali za watumishi binafsi, za idara na miradi mbalimbali. Wenye mamlaka ya matumizi ya pesa katika account hizo ni wenye account na mhazina hana mamlaka ya kuzuia isipokuwa account ya hazina kuu.

Hivyo pesa inapoingia kwenye account ya mtumishi binafsi mwenye mamlaka na control ya pesa ni mwenye account.

Kama ilvyo serikalini hazina kuu haihusiki katika kuongoza kwa kuruhusu na kuzuia matumizi ya pesa ya kila wizara, idara ya serikali nk, bali husimamia na kutunza hazina ya pesa hizo. Ndivyo inavyofanyika kanisani.

Nawaombeni mjue kuwa kuna mambo tunajadili kwa mtazamo binafsi bila kuangalia taratibu na sheria za wahusika zipoje.

Kuna wanaojielewa kwamba hapa ni wakatoliki haina maana kuwa mkatoliki kujua taratibu zote ni sawa na raia kusema anajua yote yanayoendelea huko kwenye ofisi za serikali na taratibu zake.

Tatizo letu kubwa ni kutoangalia masuala ya msingi katika ujenzi wa hoja. Shida ni moja, fedha ya Rugemalila ni halali au la? Kama ni haramu, itakuwa haramu hata kwa waliopewa. Kama ni halali itaendelea kuwa halali hata kwa waliopewa.

Hakuna mwenye haki ya kuniamria niutumieje mshahara wangu baada ya kuufanyia kazi kwa mwezi mzima. Kama Watanzania tuna ushahidi kama James Rugemalila alituibia tuishinikize serikali imfungulie mashitaka ya wizi.
Tuache chuki, maana naona baadhi ya watu wameanza kuingiza suala la uhaya wa Rugemalila na Askofu Kilaini na jaji Luangisa. Wanasahau kuwa Chenge, Kimiti, Ngeleja n.k sio wahaya. Wengine wanaingiza ukatoliki wa Askofu Kilaini na Nzigilwa, kana kwamba kanisa ndio lilitoa idhini Rugemalila alipwe! Kwanini watu wote wako kimya kwa kiasi kingine cha fedha kilichopitia kwenye bank nyingine? Au kuna ushahidi kuwa waliolipwa na benki nyingine hakuna wahaya na wakatoliki? Hii inashangaza sana.

Ninayasema haya kwa uchungu kwa maana mimi ni mhaya kwa kabila na mkatoliki kidhehebu. Silioni kosa la wahaya kama kabila kama ambavyosilioni kosa la katoliki kama dhehebu. Tujalidili hoja bila kuhusisha makabila ya watuhumiwa na wala uumini wao.
 
Nakubali kuwa pengine uelewa wangu ni mdogo (kuliko wako?).

Naweza kukubaliana na wewe kama pesa hizi alipewa Nzigilwa kama mtu binafsi na hivyo anao uhuru wa kutumia pesa hizo vyovyote atakavyo (kujenga, kusaidia masikini etc) bila kuwajibika kwa yeyote. Ni "zawadi" tu.

Lakini kama aliyetoa pesa hiyo aliitoa kwa taasisi(kanisa) ni wazi kuna maswali mengi ya kujiuliza hasa kuhusiana na governance (accountability). Je, isingekuwa suala la escrow kuwekwa wazi, kanisa lingejua kuwa kuna muumini amelichangia mamilioni hayo kupitia kwa Nzigilwa? Upo utaratibu wa maaskofu/mapadre/masista kuweka wazi zawadi na michango wanayopokea kutoka kwa wahisani? Askofu Nzigilwa (na Kilaini) waliweka wazi michango hiyo ya Ruge? Kwa nini Nzigilwa na Kilaini?

Tunalo tatizo la kimaadili kama taifa. Tunaweza kutetea tunavyoweza, lakini hilo halitusaidii kutibu tatizo. Angalia hata muda tu waliotumia maaskofu hawa kutolea maelezo pesa hizo tangu mambo haya yawekwe hadharani. Ukiangalia kwa makini mgawo wa Ruge, utaona kuna "formula" fulani kaitumia - kuna uhusiano wa viwango alivyogawa kwa watu mbalimbali.

Rugemalila, aligawa kutokana na kiwango cha fedha alichonacho, kwa mtu kugawa kwa rafiki, jirani au hata mtu baki asilimia kumi ya kipato chake mbona ni jambo la kawaida? Mwenye mshahara wa shilingi 1.5 milioni kumpa mtu shilingi laki moja na nusu mbona hili halishangazi? Ruge alipata zaidi ya bilioni 75 baada ya kulipa kodi. asilimia 10 ya bilioni 75 ni bilioni 7.5, lakini katika benki ya mkombozi mgao ulioenda kwa watu baki ambao sio watoto wake na kampuni yake ya Mabibo ni chini ya bilioni 3. Kama ni kusaidia jamii mbona inasemekana anataka kujenga hospitali ya kisasa ya kansa katika mkoa wa Kagera?
Kama tunaushahidi wa wizi wa mali ya umma uliofanywa na Rugemalila tumshitaki na watoa wahukumu zamu hii wasiwe wahaya kama ambavyo aliyetoa hukumu ya kumlipa hakuwa jaji wa kihaya. Nadhani suala hili sasa litakuwa limeeleweka vizuri
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Unajaribu sana kujenga utetezi ukiacha masuala muhimu sana.

1. Kama pesa ni za halali, Tibaijuka,Werema, Maswi Wameonewa au la. Na kwanini
2. Je, Rugemalrila aliuza umeme kulingana na mkataba wake? Kama hakufanya hivyo, je hapo hakuna wizi?
3. Askofu aliingiziwa pesa kwenye account binafsi. Je kanisa lina taarifa hizo?
4. Unapowaweka akina Ngeleja, Werema, Chenge na Nzigilwa kwa pamoja, unapata picha gani
5. Kwani kusomesha watoto katika makanisa kunondoa dhambi ya wizi wa ada iliyopitakana kwa njia haramu?
6. Nafasi ya Nzigilwa, inaruhusu achukue pesa zenye utata kama hizi? Na je alijua ni halali? Na sasa anaweza kusimama na kutuambia pesa zile ni halali?

Rudia kusoma post za nyuma maswali yako yate niliyajibu, unarudiarudia kitu ambacho nimeshakijia no sense.
 
..sikutaka kukujibu lakini imenibidi...

..wewe kwangu sio great thinker...kama unajiona hivyo basi kwangu sivyo.....Nakuona unavyohangaika kumtetea askofu wako...unajidhihirisha ulivyo na maslahi binafsi kwenye jambo hili....We kama hadi leo kwenye kashfa hii ya escrow hujaona kosa la hawa maaskofu kuingiziwa mabilioni ya fedha (zilizotokana na escrow account)kwenye acc.zao..basi wala haina haja kukujibu..

...Unauliza kuonyeshwa uchafu wa hela!!inaonyesha we wala hujui dhana ya kutakatisha fedha...na iweje fedha za misaada/sadaka iwekwe kwenye account zao na si taasisi zao??utasema walipewa sharti hilo...we unajua kwanini walipewa sharti hilo??....Malalamiko umeyazoea??yani watu tukiona ushenzi tusilalamike??are you out of your mind???tukae tu kimya wakati tunaona kinachofanyika sicho??..we jamaa unaishi TZ kweli???

...Btw..nimeona huko kwenye post zako nyingine unasema eti tunalalmika wakati tunapeleka watoto wetu kwenye taasisi za dini/Roman!!...ndio tunawapeleka ...kwani tunawapeleka huko bure?????Kuna taasisi ya dini inasomesha watoto bure nchi hii???..hata waumini maskini hawaendi kanisani bila sadaka.usitake kutuchefua hapa we.....Unajiita thinker!!!my foot!! watu makini hawatambi bana....acha ujinga...

Ulichoandika hakieleweki, haujachambua kubainisha kwamba pesa ni za wizi. Lete hoja zako kuchambua wizi ulivyotokea vinginevyo ni wivu tu na mhemuko wa kufuata mkombo. Sihitaji kukujibu maswali maana mabandiko yangu yameainisha hoja na mmeshindwa kuzipiku ila mnalalama tu bila hoja.
 
..wewe kama unashindwa kuelewa mistari michache ya nilichoandika hapa utawezaje kuelewa kama pesa ni za wizi??..and you call yourself a great thinker!!...You prove to be very ignorant...siku nyingine usije kuni quote kipumbavu..maana sitakujibu....endelea kuwatetea wezi....
 
Rudia kusoma post za nyuma maswali yako yate niliyajibu, unarudiarudia kitu ambacho nimeshakijia no sense.
Candid scope , umesema hoja zangu ni non sense. Nimejaribukurudi tena kusoma kama ulivyonishauri. Nazipitia hoja zako katika ububusa busawangu, nivumilie kwa hilo

Kwanza nakutaarifu,chochote kinachotolewa kwa hiari au kwa misingi ya imani ni sadaka.
Matoleo na michangoni sadaka. Nasikitika unapopotosha umma kuhusu hilo.
Lau unadhani si sahihi,nitaarifu nikutembeze kuanzia Jamatini, Kanisani na Misikitini kwa ufafanuzi.

Candid scope:
Rugemalira pato lake ni kubwa, na ameelekezapesa zake kwa shughuli za Umma, kupitia watu anaowaamini kama maaskofuwanaofanya maendeleo ya umma bila kinyongo au bodi za kugawiana pesa

My take: Kwanzautambue tofauti ya umma na Jamii. Umma unahusisha sehemu kubwa yajamii likiwana mchanganyiko wa watu(diversity)

Jamii ni kundilenye tabia, mwelekeo, malengo na ufanano wa hali fulani.
Kunaweza kuwana Umma wa Watanzania, au umma wa chama cha siasa.
Pia kuna jamii ya wahindi,jamii ya waislam na jamii ya wakristo, wapagani, wasioamini, wabondei, wamasain.k.

Rugemalirahakuelekeza pesa zake katika shughuli za umma. Ni upotoshaji mkubwa.
Ujenzi wa nyumba na makanisa ya Makongo kwa mujibu wa Nzigilwa si shughuli zaumma, ni shughuli za jamii.

Hivyo, umetumia neno umma mara nyingi kwa upotofu ukilenga kuonyesha uzuri wa Nzigilwa na Ruge.
Huu upotoshaji. Sema hivi, Rugemalira ameelekeza pesa zake kwenye shughuli zajamii.
Hajahudumia umma, acha upotoshaji huu. Unapotumia maneno angalia maanayake kwanza

Pili, kamaRugemalira anaelekeza pesa zake kwa ‘umma' ili zifanye shughuli za ''umma''tunajiuliza, zile milioni 40 za Ngeleja, Milioni 40 za Jaji Utamwa, bilioni 1.6za Chenge na zile za Stanbic unazosema zimefichwa, pesa hizo zimeleekezwa kwashughuli gani ya umma unayoijua inafanywa na watu hao?

Candid scope: Walioboronga ni serikali ilizombea kwakukubalikuuziwa umeme wa ghali.Rugemalaira si mwizi

My take:Mkataba ulitamka kiwango cha mashine za uzalishaji zinazotakiwa.
Hakuna umemewa ghali. Kilichopo ni kutoheshimu mkataba

Ni kuuza bidhaakwa kucheza na mizani. Ruge alijua hilo
Ndio maana bodiya Tanesco ilisaini mikataba na pengine kufanya uzembe

Ukweli si uzembe, niuhalifu uliochagizwa na rushwa aliyotoa Ruge.

Ndio msingi wawatu waliokuwa na maamuzi kama Ngeleja na Jaji Utamwa kupewa pesa unazoita za maendeleo

Kwa vile Rugeni ‘muumini mzuri sana' kitendo cha kucheza na mizani ni kukiuka maadili ya kiroho(moral decay) na imani zingine zinatamka ni wizi. Hili si kwamujibu wangu, ni kwa mujibu wa vitabu vitakatifu ikiwemo anavyoamini Rugemalirana anavyohubiria Nzigilwa.

Kwa taarifa yako, askofu Nzigilwa hajasema mahali popotepale kuwa pesa alizopewa ni kwa ajili ya maendeleo. Hizo ni hoja zako mwenyewe.
Askofu alitoa ufafanuzi wa jinsi pesa zilivyoingia katikaaccount yake kutoka kwa mtu anayemjua ni mfanyabiashara maarufu na mzuri tu.
Hakuna suala la shughuli za umma, umma ni mpana kulikoNzigilwa na Ruge. Na hakuna shughuli za maendeleo ya umma. Hawakujenga chochotekwa umma wala kuhudumia lolote kwa umma. Labda kama wamefanya hivyo kwa jamiiyao na si umma.
Acha kutumia maneno umma na maendeleo kujenga uhalalikatika uharamu.
 
Back
Top Bottom