Askofu Mwamakula: Watanzania tumsikilize Mzee Wassira kuhusu Mwalimu Nyerere

comrade wetu

JF-Expert Member
Nov 5, 2018
964
605
FB_IMG_1571064922706.jpg


Mkuu wa kanisa la Monrovian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Monrovian ya Uamsho Duniani, Baba Askofu Emmaus Bandikile Mwamakula amesema amemsikiliiza sana Mzee Wassira alipoongea leo Butiama katika katika kumbukizi ya miaka ishirini bila Mwalimu Nyerere.

Mzee Wassira ni mmoja ya watu wachache waliomjua sana Mwalimu Nyerere na amemuelezea kiundani kuonesha uhalisia kuhusu kiongozi huyo; kikubwa amemuelezea katika mtizamo wa anavyoheshimu mawazo ya kila mtu na alivyoheshimu uhuru wa kutoa mawazo na uhuru wa kujieleza, na pia,katika mtizamo wa usikivu kwa maneno haya " Nyerere msikivu na anayeshaurika"

Baba Askofu amempongeza Mzee Wassira kwa mada hiyo na kuongeza, "Umenivutia sana hasa ukizingatia kuwa tunaishi katika kipindi hiki ambacho kimeibuka kizazi cha viongozi wajuaji, wasioheshimu mawazo ya wenzao, wanaowatisha wengine kwa kujimwambafai.''
 
"Umenivutia sana hasa ukizingatia kuwa tunaishi katika kipindi hiki ambacho kimeibuka kizazi cha viongozi wajuaji,wasioheshimu mawazo ya wenzao ,wanaowatisha wengine kwa kujimwambafai
Askofu Mwamakula mwenyewe angekuwa msikivu asingetimuliwa kanisa la Moravian Tanzania na kwenda kuanzisha lake lisilokuwa na waumini la kusali mwenyewe na mkewe
 
Askofu Mwamakula mwenyewe angekuwa msikivu asingetimuliwa kanisa la Moravian Tanzania na kwenda kuanzisha lake lisilokuwa na waumini la kusali mwenyewe na mkewe
Bange hizo,sasa hapo kilichokukera nini kuambiwa ukweli.
 
Back
Top Bottom