Askofu Mwamakula: Tusilale usingizi pasipo kujua Moses Lijenje yupo wapi na ana hali gani

Huyo Malaya anayejiita yehodaya ni kimada WA mwendakuzimu , achaneni naye lengo lake hata enzi za makufuli kuandika ujinga kwenye mada critical kama hizi ili kudivert attention muishie kujibizana naye na kushindwa kujikita kwenye mjadala husika
 
acha ujinga wako bhana. kama jambo huna maslahi nalo kaa kimya? hivi leo mtu akihoji
zilipo pesa za pre bagaining anatafuta kiki?
mtu akihoji ni kina nani walimpiga lisu risasi ni kutafuta kiki?
kuhoji aliko Ben sanane ni kutafuta kiki?
yupo wapi anzory gwanda?
ujinga, ushamba na roho mbaya yako peleka lumumba mkuu
Tena kama anajiamini kuwa anayozungumza ni sahihi ajitambulishe hadharani na raia watamtafuta wamsifu na kumpongeza. Ataje na anakoishi tuu ndugu yetu huyu YEHODAYA

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Kwanini kuna watu wanaitwa wajinga?
Ni kwa sababu wanawaza kijinga,wanaongea kijinga na wanaandika kijinga.
Moses ni kijana wa Kitanzania tena askari Jeshi shupavu na komandoo. Kwa nyakati tofauti ametetea maslahi ya nchi hii kwa kuhatarisha maisha yake binafsi bila hofu, jee unadhani wanajeshi wenzake na watu wema wanawadha nini kama huyo anapotea tena mikononi mwa vyombo vyetu vya usalama?
Angepotezwa Mwigulu au Makonda mngeishia kusema hajulikani alipo tuu?
Tunamtaka Moses sisi wananchi, na wale wenzake wanamtaka mwenzao!
Mkuu unaweza kunitoa gizani suala la huyu bwana,ilikuaje?..maana nimeiona ni komandoi
 
Mwamakula anataffuta kick
Baada ya kuona watu wamempuuza na umaarufu wake kwisha
ACHA UJINGA !

Tuambie Moses lijenje yuko wapi!

Watoto wake wanamsumbua mama yao "Baba yuko wapi"!?

JWTZ WAUNGANE WAMTAFUTE MWENZAO KWANI NA WAO NI WASTAAFU WATARAJIWA!!
 
TUSILALE USINGIZI PASIPO KUJUA MOSES LIJENJE YUKO WAPI NA ANA HALI GANI!

View attachment 2391595

Kamanda Kingai na Afande Mahita katika nyakati tofauti kila mmoja akiwa chini ya kiapo, walitoa ushahidi Mahakamani kuwa walikuwa wakimtafuta mtuhumiwa Moses Lijenje kule Moshi. Lakini mmoja wa watuhumiwa hao (aliyesadikiwa kuwa pamoja na Moses Lijenje katika program ya VIP Protection ya Mbowe); akiongozwa na Mawakili wa Utetezi, ameieleza Mahakama mara kadhaa juu ya Moses Lijenje.

Shahidi (mtuhumiwa) huyo ameieleza Mahakama kuwa alipokuwa akiteswa, alitishwa na mmoja wa wasulubu (Polisi) wake huku akigusishwa bastola kichwani kuwa na yeye angelitupwa kama alivyotupwa Moses Lijenje bila kutaja alitupwaje na alitupwa wapi na kwa sababu gani. Kwa maneno mengine, wasulubu (Polisi) hao ndio 'walimtupa Moses Lijenje'!

Mambo mengine ni ya Jaji na Mahakama, sisi watetezi wa haki tuna jambo letu. Kama watetezi wa haki ni lazima tutake kujua Moses Lijenje yuko wapi na hali yake ikoje huko aliko. Kama kweli ametupwa, ametupwa na nani na kwa sababu gani na ametupwa wapi na hali yake ikoje huko aliko? Kutupwa huko kuna maana gani? Kesi hiyo inaweza kuchukua muda mrefu kuisha, lakini hiyo haituzuii sisi watetezi wa haki kutafuta kujua wapi aliko mtu anayeitwa Moses Lijenje na hali yake ikoje.

Kwa sababu hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito wa kila Mtanzania kufanya 'manhunt' yaani kuanza kumtafuta mtu aitwaye Moses Lijenje kuanzia muda huu. Jeshi la Polisi linao wajibu wa kuuambia umma ni wapi alipo ndugu Moses Lijenje! Paza sauti yako kwa kusema, kuandika na kusambaza ujumbe hadi uwafikie walio karibu na Lijenje, wanaomhifadhi, alikokimbilia au waliomtupa!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Mwanakondoo Amwshinda. Mungu amtetee sana Moses Lijenje.
 
Halafu akishakuwa maarufu iweje?
Acha hizo aiseee hapo yanazungumziwa maisha ya mwanadamu tena mwanaume mwenye familia.
Kuwa na huruma siasa za kingese zisikutoe kwenye kufikiria zawadi ya maisha tuliyopewa na muumba wetu.
Magufuli aliharibu Sana mentality za hao matahila kina YEHODAYA , yaani wao mtu akiuliwa au kupotezwa kwao Ni sawa
 
Kwa kweli tulifikia pabaya. Hebu fikiria mtu anapata wapi ujasiri wa kuomba tenda kutoka kwa Rais wa Tanzania ya kumuua Mtanzania na kui-post humu JF. Tulioisoma hiyo post tulipigwa butwaa!

Baadaye post hiyo inaonekana ilifutwa baada ya kuchangiwa na wazalendo wengi tu wakiulizia huu ujasiri unatoka wapi? Kwa shetani mwenyewe? Mashahidi wa hili ni wale wana JF wote walioisoma.

Hadi leo hii mtu huyo anayejiita YEHODAYA, bado anao uthubutu wa kuandika humu akimkebehi Askofu Mwamakula kwa kuhoji alipo Moses Lijenje! Yaani hadi leo haya makatili bado yapo yanadunda tu!

Kwa hakika inafikirisha sana!
Ndio maana Tundu Lissu anaomba ahakikishiwe usalama wake kabla ya kurudi jehanamu
 
Kamanda Kingai na Afande Mahita katika nyakati tofauti kila mmoja akiwa chini ya kiapo, walitoa ushahidi Mahakamani kuwa walikuwa wakimtafuta mtuhumiwa Moses Lijenje kule Moshi. Lakini mmoja wa watuhumiwa hao (aliyesadikiwa kuwa pamoja na Moses Lijenje katika program ya VIP Protection ya Mbowe); akiongozwa na Mawakili wa Utetezi, ameieleza Mahakama mara kadhaa juu ya Moses Lijenje.
Siku zote damu ya Binadam huwa inanuka
Ole wao wauaji hawa adhabu ya laana ipo juu yao, watoto na wajukuu wao!
Fuatilieni matukio ya familia za watu hawa kwa siku sijazo mtaona kitu ambacho sio kawaida!
Damu zitakuwa zinatafuna familia hizi kila uchwao!
 
TUSILALE USINGIZI PASIPO KUJUA MOSES LIJENJE YUKO WAPI NA ANA HALI GANI!

View attachment 2391595

Kamanda Kingai na Afande Mahita katika nyakati tofauti kila mmoja akiwa chini ya kiapo, walitoa ushahidi Mahakamani kuwa walikuwa wakimtafuta mtuhumiwa Moses Lijenje kule Moshi. Lakini mmoja wa watuhumiwa hao (aliyesadikiwa kuwa pamoja na Moses Lijenje katika program ya VIP Protection ya Mbowe); akiongozwa na Mawakili wa Utetezi, ameieleza Mahakama mara kadhaa juu ya Moses Lijenje.

Shahidi (mtuhumiwa) huyo ameieleza Mahakama kuwa alipokuwa akiteswa, alitishwa na mmoja wa wasulubu (Polisi) wake huku akigusishwa bastola kichwani kuwa na yeye angelitupwa kama alivyotupwa Moses Lijenje bila kutaja alitupwaje na alitupwa wapi na kwa sababu gani. Kwa maneno mengine, wasulubu (Polisi) hao ndio 'walimtupa Moses Lijenje'!

Mambo mengine ni ya Jaji na Mahakama, sisi watetezi wa haki tuna jambo letu. Kama watetezi wa haki ni lazima tutake kujua Moses Lijenje yuko wapi na hali yake ikoje huko aliko. Kama kweli ametupwa, ametupwa na nani na kwa sababu gani na ametupwa wapi na hali yake ikoje huko aliko? Kutupwa huko kuna maana gani? Kesi hiyo inaweza kuchukua muda mrefu kuisha, lakini hiyo haituzuii sisi watetezi wa haki kutafuta kujua wapi aliko mtu anayeitwa Moses Lijenje na hali yake ikoje.

Kwa sababu hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito wa kila Mtanzania kufanya 'manhunt' yaani kuanza kumtafuta mtu aitwaye Moses Lijenje kuanzia muda huu. Jeshi la Polisi linao wajibu wa kuuambia umma ni wapi alipo ndugu Moses Lijenje! Paza sauti yako kwa kusema, kuandika na kusambaza ujumbe hadi uwafikie walio karibu na Lijenje, wanaomhifadhi, alikokimbilia au waliomtupa!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Hizi sasa bangi, yaani niache kutafuta riziki kuendeleza maisha yangu eti nimtafute Moses Lijenje
 
Shahidi (mtuhumiwa) huyo ameieleza Mahakama kuwa alipokuwa akiteswa, alitishwa na mmoja wa wasulubu (Polisi) wake huku akigusishwa bastola kichwani kuwa na yeye angelitupwa kama alivyotupwa Moses Lijenje bila kutaja alitupwaje na alitupwa wapi na kwa sababu gani. Kwa maneno mengine, wasulubu (Polisi) hao ndio 'walimtupa Moses Lijenje'!
nditolo....
 
Back
Top Bottom