Askofu Mwamakula: Tunduma hali sio shwari

Askofu Mwamakula: Tunduma hali sio shwari

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,331
TUNDUMA HALI SIO SHWARI!

Hali ya Tunduma mkoani Songwe siyo nzuri. Hadi sasa wamekufa watu wawili mmoja wa CCM na mwingine wa CHADEMA. Vurugu zilizosababisha vifo hivyo zina uhusiano kwa sehemu na 'mienendo' au 'matendo' ya baadhi ya Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kuhusiana na suala zima la kutenda haki katika mchakato wa Uteuzi wa Wagombea mkoani Songwe. Kwa upande mwingine ni mvutano kati ya CCM na CHADEMA wanaogombania umiliki wa Tunduma kisiasa!

Sisi kama viongozi wa dini tumeonya na tumeendelea kuonya sana juu ya mwenendo wa baadhi ya Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika Majimbo na Kata nchini kote. Kwamba malalamiko na hisia kutoka kwa baadhi ya vyama vya siasa kuonewa visiposhughulikiwa huondoa utulivu katika jamii. Tunduma sasa hali inaelekea mahali pabaya.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tunduma, Mheshimiwa Frank Mwakajoka amenieleza kwa mtazamo wake hali ilivyo kule. Anasema Wagombea Udiwani watatu wa CHADEMA wameunganishwa katika Kesi ya Mauaji. Anaendelea kueleza kuwa: "Kuna Madiwani wengine wanaotakiwa kukamatwa wakiwemo Ally Mwafongo (Kata ya Makambini), Mosses Mshani (Kata ya Muungano), Frowini Mwalongo (Kata ya Maporomoko), Osiah Kibwana (Kata ya Kaloleni), Boniphas Mwakabanje (Kata ya Majengo) na M/kiti wa Mkoa wa Songwe Isakwisa Lupembe, Mtunza Hazina wa Jimbo, ndugu Hamza Huseni na baadhi ya viongozi wa Kata na Matawi mbali mbali".

Hali siyo shwari kule Tunduma! Hao wote waliokamatwa na wanaotafutwa kukamatwa ni viongozi wa Kisiasa ambao nyuma yao kuna kundi kubwa la watu. Ni Wagombea wa Udiwani. Hekima kubwa inahitajika katika kutatua tatizo la Tunduma. Kuna uwezekano mkubwa kuwa nyuma ya vurugu hizi kuna hujuma za kisiasa, matendo na mienendo ya baadhi ya Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi.

Pengine swali la kujiuliza ni je, baadhi ya Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika Mkoa wa Songwe watawajibika vipi kwa mienendo na matendo yao ambayo kwa sehemu yalipelekea vurugu zilizopelekea vifo na kutaka kusababisha Wagombea kukosa nafasi ya kuwakilisha sehemu kubwa ya watu? Hekima kubwa itumike ili kutokuwanyima haki ya kugombea Wagombea wanaowindwa kama ndege ili kukamatwa kuhusiana na vurugu za Tunduma.

Tunazidi kuonya na kutahadharisha kuhusu umuhimu wa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutenda Haki ili kutunza amani ya nchi. Tunaweza kuepusha vurugu na vifo nchini kwa kutenda haki katika Uchaguzi Mkuu.

Kuonya na kutahadhalisha ni wajibu waliopewa baadhi yetu na ole wetu tusipofanya (Ezekieli 33:1-20).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
 
Huu uchaguzi utapita lakini kutakua na kesi za uchaguzi zitakazokwenda miaka 2-3 mbele

Sidhani kuwa kesi hizo zitachukua muda mrefu hivyo sababu zimepangwa na zinatakiwa zifuate mtiririko wake ambao ni mfupi tu, Jaribu kuangalia kwanza wamejipangaje ndio utajua mwisho wa kesi hizo utakuwaje
 
Mnafanya maigizo wenyewe halafu knakuwa wakwanza kukimbilia mitandaoni kutafuta promo, hatuwaachi jamaaa.
Tukaneni tuuuu.
Ilamaigizo yenu kwisha habari yenuuu.

Tuliza hasira mamaa.
Unadhani watu 2 kuuwawa ni maigizo? Dalili ya mvua ni mawingu! Penye moshi pana moto!!! Heri kuzuia kuliko kuponya!! Kama una masikio, sikia!!!
 
Unadhani watu 2 kuuwawa ni maigizo? Dalili ya mvua ni mawingu! Penye moshi pana moto!!! Heri kuzuia kuliko kuponya!! Kama una masikio, sikia!!!
Haya yote yanatengenezwa na nyie ilimpate kiki yakwamba Tanzania kunamachafuko ya kisiasa ilimuipake doa Tanzania.
Maaana kila siku furaha yenu, ni Tanzania ipate machafuko, ndo mkaimbe ngonjera zenu kwa mabeberuuu.
Hatuko tayali amani yetu ichafuliwe na wahuni wachacheee, kwa kisingizio cha kutafuta kiki ya kisiasaa.
 
Hilo Kanisa limetokea wapi?
Sisi wamoravian tuna Kanisa la Moravian Tanzania. Huyo lazima atakuwa naye alihasi
 
Uhuni wa. wazi kabisa huu, halafu CCM ndio wanajidai kuhubiri amani kila siku, amani gani wakati mnajua fika mnawafanyia watu mambo mabaya kila siku?

Tunduma damu itamwagika, na wa kwanza kupelekwa mahakamani ni hao wakurugenzi wanaotumika kisiasa.
 
Back
Top Bottom