Askofu Mwamakula: Rais Magufuli tunakuomba utoe kauli ya kumkaribisha nchini Tundu Lissu na rai ya kuwafutia kesi za uchochezi viongozi wa upinzani

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
MHESHIMIWA RAIS, TUNAKUOMBA UTOE KAULI YA KUMKARIBISHA NCHINI MHESHIMIWA TUNDU LISSU NA RAI YA KUWAFUTIA KESI ZA UCHOCHEZI VIONGOZI WA VYAMA VYA UPINZANI.

Mpendwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli (PhD), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Ninakusalimu katika Jina la Yesu Kristu!

Ninaandika waraka huu kwako nikijua fika kuwa wewe ni Mkristu unayefahamu maana ya neema na hivyo utakuwa unajua kuwa wewe peke yako miongoni mwa watu zaidi ya milioni 55 katika Nchi hii ndiye uliyepata neema na kibari cha kutawala na kuiongoza Nchi hii katika zama hizi.

Mheshimiwa Rais, ninapenda kukiri kuwa katika siku za hivi karibuni yapo mambo kadhaa yaliyonitia moyo lakini ningependa kuyasema haya machache kwanza. Mosi, hatua ulizochukua kuhusiana na Mheshimiwa Hussein Bashe, Mheshimiwa January Makamba, Mheshimiwa Nape Nnauye, nk zinatia moyo sana kwani ni dalili kwamba tunaingia katika awamu ya kuendesha siasa za uvimilivu na staha katika Nchi hii. Pili, kauli yako na nia yako ya kutaka kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi ni ishara ya maridhiano na mapatano mazito yenye kutaka kushirikisha kila mtu katika kujenga uchumi wa Nchi. Nakumbuka mambo haya niliwahi kuyasema pia huko nyuma. Leo nimeona hatua za utekelezaji katika kauli yako. Ni dhahiri kuwa wapo watakaohoji au hata kubeza kauli yako kuhusiana na hilo na huo ndio uhuru wenyewe wa kufikiri, lakini kwetu sisi tunaotambua nguvu ya kauli hasa itokayo katika kinywa cha mkuu kamwe hatuwezi kubeza bali tunaingia katika hatua ya kuombea ili nia njema katika kauli hiyo ikazae matunda mema.

Mheshimiwa Rais, pamoja na mambo hayo muhimu, ninapenda kuhudhurisha kwako sehemu ya yale yaliyomo katika moyo wangu kama Askofu na mioyo ya Maaskofu wengine wanaokuombea katika Nchi hii na hata mioyo au matamanio ya watu walio wengi ambao kwa hakika wanaweza wasipate nafasi au hata ujasiri wa kukushirikisha jambo lo lote lililo jema. Uwoga au hofu yao kuyasema haya haitokani na wao kukuogopa wewe la hasha! Wewe umejipambanua kuwa uko tayari kumsikiliza mtu ye yote. Bali hofu yao kwa sehemu inaweza kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na kuwaogopa baadhi ya watu wanaoizunguka taasisi ya Rais ambao wanaweza kupotosha ukweli kwa Mheshimiwa Rais au kwa sababu za kutaka upendeleo wakataka kumshawishi Rais ili afikiri kuwa kuna watu wanampinga Rais! Watu hawa hata kama ni wachache ndio wanaofanya watu wengi wenye nia njema wafunge vinywa na akili zao kwa kuogopa kueleweka vibaya.

Mheshimiwa Rais, thamani yangu kama Askofu itakuwa na maana pale tu nitakapoweza kufumbua kinywa na kwa tahadhari kubwa nikalisema jambo lolote lililo jema na linalojenga pasipo kuogopa (Wafilipi 4:8).

Mheshimiwa Rais, ninakumbuka mara tu baada ya Mheshimiwa Tundu Lissu kushambuliwa kule Dodoma miaka miwili iliyopita wewe ulitoa kauli ya kumtakia heri na ahueni. Taifa lilisikia kauli yako katika saa ile ya giza katika historia ya Nchi. Ni dhahiri kuwa Taifa linatarajia kusikia tena kauli yako ya kumkaribisha Mheshimiwa Lissu akiwa amepona. Kauli yako haitakuwa udhaifu lakini itakuwa na maana kubwa sana katika kuimarisha utulivu katika ulimwengu wa diplomasia. Haya ya kufutiana Ubunge ni mikakati ya kisiasa ambayo haiwezi kumzuia Rais wa Nchi katika kutimiza majukumu yake katika kuliunganisha taifa.

Mheshimiwa Rais, ninapenda kurudia tena rai yangu ya kuomba na kushauri viongozi wa vyama vya upinzani kufutiwa kesi za uchochezi. Kama hili limeweza kuwezekana kwa watuhumiwa wa uhujumu uchumi ninaamini linawezekana pia kwa viongozi wa vyama vya siasa na Waandishi wa Habari wanaotuhumiwa kwa uchochezi. Mambo hayo mawili hapo juu yakifanyika ndio kile ambacho Waingereza wanakiita "reaching out to the opposition" kitendo ambacho wanaweza kufanya viongozi majasiri tu duniani.

Mheshimiwa Rais, mimi ni mzaliwa wa Nchi hii na ndio maana najisikia fahari kumshauri Rais wangu yale ambayo nayaona kuwa yanabeba maslahi mapana ya taifa na Ufalme wa Mungu ninayemtumikia.

Mheshimiwa Rais, miradi uliyoianzisha ni mikubwa na inahitaji sana utulivu wa kisiasa na amani ndani ya Nchi katika kuitekeleza. Ni dhahiri kuwa jamii iliyogawanyika haiwezi kutekeleza kwa ufanisi mkubwa miradi kama hiyo. Kwa vyo vyote vile, ikiwa sehemu ya jamii ye yote imo katika maumivu au chuki au uhitaji basi ushiriki wake katika maendeleo ya pamoja hautakuwa wa kuridhisha.

Ni matumaini yangu kuwa Mheshimiwa Rais utaongozwa na Roho wa Mungu katika kupambanua nia njema iliyomo katika waraka huu kama sio sasa basi katika siku za usoni. Ninaamini na ni maombi yangu kuwa Mheshimiwa Rais hatakwazwa na ushauri huu wa Kichungaji ambao unatolewa kama sehemu ya Askofu katika kutii na kutimiza wajibu wake. Ninakutakia heri na baraka unapoendelea kutimiza majukumu yako ya u-Rais. Ninakuomba ukipata nafasi uweze kutafakari Zaburi 1 na Zaburi 101 hasa kila unapotaka kuteua au kutengua wasaidizi na washauri wako.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duaniani (World Fellowship of Moravian Revival Churches)
 
Who the hell is tundu lissu? He is just just a kibaraka wa mabeberu!
Yawezekana ulizaliwa ukiwa pungufu au umepungukiwa baadaye. Lakini kwa walio kamili wanajua kuwa kila utakapokwenda, iwe mjini au kijijini, tamka jina la Tundu Lisu, hutakosa mtu anayemfahamu.

Jina la Tundu Lisu katika nchi hii linafahamika na Watanzania wengi kuliko jina la Waziri yoyote wa serikali ya Mwungano wa Tanzania.
 
Hahahaaa Jamaa anayoa misamha ya kinafiki ya kulazimishana ukiwa mahabusu lazima ukubali kuwa inehujum uchumi hata kama huna hatia ili uachiwe huru, dhambi hii anayofanya Magufuli madhara yake yatamtafuna.

Kama ana huruma hadi ya kusamehe wahujumu uchumi anashindwaje kuacha ujatili wa kutesa kuteka na kusulubu wanaompinga kikatiba kwa njia halali za kisiasa??

Unafiki mkubwa.
 
Duh...!, kwa ushauri kama huu, hala hala
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duaniani (World Fellowship of Moravian Revival Churches), asije kuchunguzwa uraia wake.
P
 
MHESHIMIWA RAIS, TUNAKUOMBA UTOE KAULI YA KUMKARIBISHA NCHINI MHESHIMIWA TUNDU LISSU NA RAI YA KUWAFUTIA KESI ZA UCHOCHEZI VIONGOZI WA VYAMA VYA UPINZANI.

Mpendwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli (PhD), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Ninakusalimu katika Jina la Yesu Kristu!

Ninaandika waraka huu kwako nikijua fika kuwa wewe ni Mkristu unayefahamu maana ya neema na hivyo utakuwa unajua kuwa wewe peke yako miongoni mwa watu zaidi ya milioni 55 katika Nchi hii ndiye uliyepata neema na kibari cha kutawala na kuiongoza Nchi hii katika zama hizi.

Mheshimiwa Rais, ninapenda kukiri kuwa katika siku za hivi karibuni yapo mambo kadhaa yaliyonitia moyo lakini ningependa kuyasema haya machache kwanza. Mosi, hatua ulizochukua kuhusiana na Mheshimiwa Hussein Bashe, Mheshimiwa January Makamba, Mheshimiwa Nape Nnauye, nk zinatia moyo sana kwani ni dalili kwamba tunaingia katika awamu ya kuendesha siasa za uvimilivu na staha katika Nchi hii. Pili, kauli yako na nia yako ya kutaka kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi ni ishara ya maridhiano na mapatano mazito yenye kutaka kushirikisha kila mtu katika kujenga uchumi wa Nchi. Nakumbuka mambo haya niliwahi kuyasema pia huko nyuma. Leo nimeona hatua za utekelezaji katika kauli yako. Ni dhahiri kuwa wapo watakaohoji au hata kubeza kauli yako kuhusiana na hilo na huo ndio uhuru wenyewe wa kufikiri, lakini kwetu sisi tunaotambua nguvu ya kauli hasa itokayo katika kinywa cha mkuu kamwe hatuwezi kubeza bali tunaingia katika hatua ya kuombea ili nia njema katika kauli hiyo ikazae matunda mema.

Mheshimiwa Rais, pamoja na mambo hayo muhimu, ninapenda kuhudhurisha kwako sehemu ya yale yaliyomo katika moyo wangu kama Askofu na mioyo ya Maaskofu wengine wanaokuombea katika Nchi hii na hata mioyo au matamanio ya watu walio wengi ambao kwa hakika wanaweza wasipate nafasi au hata ujasiri wa kukushirikisha jambo lo lote lililo jema. Uwoga au hofu yao kuyasema haya haitokani na wao kukuogopa wewe la hasha! Wewe umejipambanua kuwa uko tayari kumsikiliza mtu ye yote. Bali hofu yao kwa sehemu inaweza kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na kuwaogopa baadhi ya watu wanaoizunguka taasisi ya Rais ambao wanaweza kupotosha ukweli kwa Mheshimiwa Rais au kwa sababu za kutaka upendeleo wakataka kumshawishi Rais ili afikiri kuwa kuna watu wanampinga Rais! Watu hawa hata kama ni wachache ndio wanaofanya watu wengi wenye nia njema wafunge vinywa na akili zao kwa kuogopa kueleweka vibaya.

Mheshimiwa Rais, thamani yangu kama Askofu itakuwa na maana pale tu nitakapoweza kufumbua kinywa na kwa tahadhari kubwa nikalisema jambo lolote lililo jema na linalojenga pasipo kuogopa (Wafilipi 4:8).

Mheshimiwa Rais, ninakumbuka mara tu baada ya Mheshimiwa Tundu Lissu kushambuliwa kule Dodoma miaka miwili iliyopita wewe ulitoa kauli ya kumtakia heri na ahueni. Taifa lilisikia kauli yako katika saa ile ya giza katika historia ya Nchi. Ni dhahiri kuwa Taifa linatarajia kusikia tena kauli yako ya kumkaribisha Mheshimiwa Lissu akiwa amepona. Kauli yako haitakuwa udhaifu lakini itakuwa na maana kubwa sana katika kuimarisha utulivu katika ulimwengu wa diplomasia. Haya ya kufutiana Ubunge ni mikakati ya kisiasa ambayo haiwezi kumzuia Rais wa Nchi katika kutimiza majukumu yake katika kuliunganisha taifa.

Mheshimiwa Rais, ninapenda kurudia tena rai yangu ya kuomba na kushauri viongozi wa vyama vya upinzani kufutiwa kesi za uchochezi. Kama hili limeweza kuwezekana kwa watuhumiwa wa uhujumu uchumi ninaamini linawezekana pia kwa viongozi wa vyama vya siasa na Waandishi wa Habari wanaotuhumiwa kwa uchochezi. Mambo hayo mawili hapo juu yakifanyika ndio kile ambacho Waingereza wanakiita "reaching out to the opposition" kitendo ambacho wanaweza kufanya viongozi majasiri tu duniani.

Mheshimiwa Rais, mimi ni mzaliwa wa Nchi hii na ndio maana najisikia fahari kumshauri Rais wangu yale ambayo nayaona kuwa yanabeba maslahi mapana ya taifa na Ufalme wa Mungu ninayemtumikia.

Mheshimiwa Rais, miradi uliyoianzisha ni mikubwa na inahitaji sana utulivu wa kisiasa na amani ndani ya Nchi katika kuitekeleza. Ni dhahiri kuwa jamii iliyogawanyika haiwezi kutekeleza kwa ufanisi mkubwa miradi kama hiyo. Kwa vyo vyote vile, ikiwa sehemu ya jamii ye yote imo katika maumivu au chuki au uhitaji basi ushiriki wake katika maendeleo ya pamoja hautakuwa wa kuridhisha.

Ni matumaini yangu kuwa Mheshimiwa Rais utaongozwa na Roho wa Mungu katika kupambanua nia njema iliyomo katika waraka huu kama sio sasa basi katika siku za usoni. Ninaamini na ni maombi yangu kuwa Mheshimiwa Rais hatakwazwa na ushauri huu wa Kichungaji ambao unatolewa kama sehemu ya Askofu katika kutii na kutimiza wajibu wake. Ninakutakia heri na baraka unapoendelea kutimiza majukumu yako ya u-Rais. Ninakuomba ukipata nafasi uweze kutafakari Zaburi 1 na Zaburi 101 hasa kila unapotaka kuteua au kutengua wasaidizi na washauri wako.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duaniani (World Fellowship of Moravian Revival Churches)
Amekusikia sina hakika km atakuelewa
 
Ungeamua kitu kimoja kama dini au siasa, Acha kutumia dini vibaya
 
Back
Top Bottom