Askofu Munga: Ukitaka kuwatawala watu basi wanyime Elimu na wachimbie shimo la ujinga na elimu mbovu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
UMUHIMU WA KUJENGA UELEWA WA WATU: ELIMU NI UKOMBOZI

Lengo kubwa la elimu ni kuweka huru fikra na kufungua uwanja huru wa uchaguzi katika maisha. Elimu sio itikadi fulani bali ni nyenzo ya kuhoji na kukosoa itikadi na kupambanua mambo katika safari ya uchambuzi na hatumaye kufanya uchaguzi uliojengwa katika misingi ya maarifa. Elimu ni nyenzo ya kuhoji kulingana na falsafa ya elimu tangu mwalimu Socrates alipotufahamisha hivyo. Elimu isiyoweka uhuru wa fikra huru na badala yake inajikita katika mwelekeo mmoja wa mtazamo huishilia kuwa taaluma ya utumwa. Profesa wangu alinifundisha kwamba elimu mbovu na nusu elimu ni hatari kuliko ujinga. Mwana taaluma anayesaliti taaluma yake hana tofauti na mtu mjinga.

Elimu na taaluma ina misingi yake ambayo yeye aliyeishikilia hayumbi na hawezi kuisaliti hata kama itamgharimu maisha yake kama ilivyokuwa kwa mwalimu Socrates mwana falsafa. Wenzangu mliotunukiwa PHD katika maisha yenu sijui kama mlikula kiapo hicho wakati wa kuhitimishwa. Mimi nilipoapishwa (Doctoral promotion) niliapishwa kwamba mimi ni nuru ya maarifa na mwalimu wa kufumbua fahamu za wajinga. Kamwe sitathubutu kusaliti kweli ya maarifa na kupotosha maarifa yaliyohakikiwa kuwa kweli na ambayo binafsi nimeyahakiki. Kiapo hicho pamoja na kiapo changu cha kichungaji ( ambacho huimarisha hicho cha kitaaluma) vimeyakamata kabisa maisha yangu.

Elimu ni muhimu katika maeneo yote ya maisha kwa sababu ndiyo inayoondoa ujinga. Ujinga ni adui mkubwa wa maisha binafsi lakini pia adui mkubwa wa maendeleo ya jamii. Hakuna taifa au taasisi inayoweza kuzungumza maendeleo pasipo kung'oa ujinga toka vichwa vya watu wake. Ujinga ni utumwa na ukitaka kuwatawala watu vizuri basi wachimbie katika shimo la ujinga au wapatie elimu mbovu. Hii ndio sababu tunakazia sana mafundisho hata katika taasisi za kiimani. Ndio sababu ya Bwana Yesu kuagiza Mitume wake na kanisa kuhubiri na KUFUNDISHA wote wanaoamini.

Elimu ni ukombozi wa fikra na ni elimu nzuri tu inayoweza kumuweka huru mtu kutoka utumwa na utegemezi wa fikra za watu wengine. Elimu inapandikiza uwezo wa kuhoji mambo yasiyoeleweka. Hata katika siasa dhana nzima ya demokrasia ina maana pale ambapo watu wanao ufahamu wa kutosha juu ya maisha yao, mahitaji yao, muelekeo wao kama mtu mmojammoja na jamii kwa ujumla. Watu walioelimika wanajipangia mambo yao na kamwe hawapangiwi. Kwa hiyo ni muhimu siku zote kuelimisha jamii juu ya mambo yanayogusa jamii yao badala ya kuwaamulia. Zaidi sana, kwa watu wenye ufahamu, ukiwapigisha kura juu ya maisha yao watafanya uchaguzi sahihi. Tofauti na hivyo, ukiwapigisha kura watu wajinga juu ya mambo yahusuyo maisha yao ili kufanya uchaguzi sahihi wa muelekeo wa maisha hayo watafanya uchaguzi mbaya na mbovu.

Je, unajua kwamba hata pale unapowapa nafasi watu kuchagua pasipo kuwa na ufahamu wa yanayoyachagua wanaweza kuchagua kitu kibovu? Uhuru wa kuchagua una faida kwa mtu binafsi na manufaa kwa jamii pana ikiwa watu wanao ujuzi wa kutosha juu ya mambo wanayoyachagua. Ukiwapa nafasi watu wajinga kuchagua baina ya vitu wasivyovijua wataishilia kuchagua kitu kibaya na kukushinda katika nia yako njema.

Usimlaumu mtu mjinga anapofanya uchaguzi mbaya bali ujilaumu wewe ambaye hukujitaabisha kumuelimisha na kuongeza ufahamu wake. Tuelimishe watu wetu ili wafanye uchaguzi sahihi kwa mambo muhimu ya maisha yao. Hakuna dhambi kubwa ya kijamii kama kutumia ujinga wa watu ili kujinufaisha binafsi. Sera ya elimu (tena iwe elimu bora) kwa watoto wote TZ itusaidie kututoa katika dhambi hii pasipo kusahau ushiriki wa wadau mbalimbali, zikiwemo asasi za kiraia, katika kuelimisha jamii juu ya mambo muhimu kwa maisha yao.

Hata dhana ya demokrasia ina faida kwa jamii yenye ujuzi wa kutosha juu ya demokrasia. Vinginevyo demokrasia isiyo na ufahamu wa watu yaweza kuwa maangamizi kwa jamii. Rais Lincolin wa Marekani aliwahi kusema kwamba, iwapo atapewa masaa nane kuangusha mti, basi atatumia masaa matano kunoa shoka na matatu kuukata mti. Tutumie masaa mengi zaidi kunoa shoka, yaani kuelimisha watu wetu, ili tutumie masaa machache kuangusha mti, yaani kutatua matatizo yanayotusibu kama jamii. "Inawezekana, timiza wajibu wako!" = "It can be done, play your part!" (Mkazo wa Baba wa Taifa).
 
Kuna watu wakiongea unaweza dhani umeingia choo Cha shimo. Hakikufunikwa
 
Elimu ilikua enzi za Makweta, akaja Mkenya mmoja naye kuichezea elimu ya nchi hii kwa kuchanganya kemia na fizikia masomo ambayo tokea dunia kuumbwa hayajawahi kuchanganywa eti kisa kurahisisha Mtaala, bidii iwepo pia katika somo la uraia watu watambue haki na wajibu wao, naunga mkono
 
Mimi nilifikiri Sasa tumepata mtu mwenye PhD nikajua sasa nchi itaendeshwa kistaarabu, duuh nilipomsikia anasema anatamani malaika washuke wazime mitandao yote, nikajua hapa Tanzania imepata galasha
 
Hakusema kama Mbowe hana elimu na anamuongoza na yeye askofu

State agent
We kibwengu bila shaka una elimu ya kaptula. Takwim za kitaalam zinaoneshà CCM inapendwa na watu wasio na elimu (Mostly who have never seen a blackboard,).
 
We kibwengu bila shaka una elimu ya kaptula. Takwim za kitaalam zinaoneshà CCM inapendwa na watu wasio na elimu (Mostly who have never seen a blackboard,).
Kweli kabisa
1572191515842.jpeg
 
Back
Top Bottom