Askofu Mokiwa wa Anglikana agoma kujiuzulu baada ya kuvuliwa Uaskofu

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Screen-Shot-2017-01-08-at-4.24.38-PM.png

Sakata la Mgogoro wa Kanisa Anglikana Tanzania Dayosisi ya Dar es salaam,linazidi kuchukua sura mpya,kufuatia Askofu wa Dayosisi hiyo,Dokta Valentino Mokiwa,kugoma kujiuzulu na kustaafishwa kwa manufaa ya Kanisa hilo kama alivyotakiwa na Mhasham Askofu wa Jimbo kuu la Tanzania,Dokta Jacob Erasto Chimeledya.

Hatua ya Dokta Mokiwa,kutakiwa kufanya hivyo,ni agizo la nyumba ya maaskofu la kuundwa tume ya Askofu Mkuu wa Kanisa hilo,kuchunguza tuhuma kumi zilizokuwa zinamkabili Dokta Mokiwa,pamoja na nyinginezo, za ukosefu wa maadili,ikiwemo kufuja mali za kanisa na kuingia mikataba kiholela yenye viashiria vya rushwa katika maeneo ya Buza,ikiwemo pia kutoa daraja la Ushemasi,Upadre,na Ukanon,kwa katibu wa Dayosisi,Mkristo ambaye ametengana na mkewe na kuoa mke mwingine kiserikali kinyume na kanuni ya kanisa kuhusu ndoa.

Waandishi wa Channel Ten,wamefika katika nyumba zinazodaiwa kutelekezwa na Dokta Mokiwa ikiwemo Silver Oak ya Upanga,na ya Mtaa wa Uganda Ostabei, ambapo imedaiwa kuwa ameiacha na kwenda kupanga huku kanisa likimlipa pango la shilingi milioni 3 kwa mwezi miaka zaidi ya miaka sita.

Dokta Mokiwa jana aligoma kupokea barua yake kutoka kwa Dokta Jacob Erasto Chimeledya,na baadhi ya waamini wa kanisa hilo katika nyakati tofauti,wamezungumzia hatua ya kutakiwa kujiuzulu na kustaafishwa Dokta Mokiwa.

Katika hatua nyingine,Dokta Valentino Leonard Mokiwa,kupitia kwa Afisa habari wake,Yohana Sanha,amedai kuwa mchakato uliotumika kumuhukumu ni batili na kwamba bado yeye ni Mkuu wa Dayosisi ya Dar es salaam kwa hiyo hataachia ngazi hiyo ya Uaskofu.

Source: Channel Ten
 
Baada ya Mfalme Henri wa Nane (King Henry VIII) alipoamua kujiondoa katika kanisa la kikatoliki ikiwa ina maana hata ufalme na miliki zake zote zikajitoa baada ya Baba Mtakatifu Innocent III (not sure kama ni wa tatu au la!) kugoma kuidhinisha talaka kwa mkewe Mfalme Henry, Catherine wa Aragon ambaye kiasili alikuwa mhispania na kwamba ilidaiwa na Henry kwamba mkewe wakati anamuoa hakuwa Bikra, alikuwa tayari ameposwa kwa kaka yake ambaye alifariki kabla hajawa mfalme na kwamba sababu ya hizo sababu hapo juu ndo maana hakuweza pata mtoto wa kiume bali wa kike ambaye alimuita Mary (alikuja kuwa Malkia Mary I maarufu kama Blood Mary) basi yeye solution yake ikawa kuvunja ndoa yake na ilipokataliwa aliamua kujtenga na kanisa Katoliki kwa mantiki kwamba yeye Henry "Been Noble and Royal by Birth, Prince of the realm by grace of God and by right, he has no authority to answer but most higher, God"

so akaanza mipango ambayo ilifanikiwa kujitoa katika kanisa ambapo wale wote walio watawaliwa wake wanatakiwa kufanya hivyo na kukumbatia mabadiliko ya kievengelisti hasa yaliyoenezwa na Martin Luther na wengineo na yeye akawa mkuu wa kanisa la England au kisaizi linaitwa Anglican ambapo kwa mamlaka hayo akaitisha baraza la maaskofu na wakamdispense na talaka kwa Catherine of Aragon na kutangaza kwamba mfalme au malkia wa uingereza lazima awe Protestant na daima sio mkatoliki...ikithibitika hivyo basi automatically haki yake ya kurithi inakuwa imemtoka na kumwendea nduguye au ukoo wa karibu kidamu wa kiprotestant.

hii haikudumu sana kwani Mwanae Mary alipokuwa malkia alijaribu kurudisha ukatoliki ikashindikana sababu aliktawala miaka mitano akapokewa na mdogo wake, Elizabeth I ambaye ndo alichangia sana kuusimika uAnglicana kwa maneno kama "i see n do nothing" kwani hakuwa mkali kama baba yake, kaka yake wala dada yake katika utawala...lakini hali ya kuihitaji ukatoliki ikajirudia tena pale ambapo James II (am not quite sure) au James the second of House Stuart alipotawala alikuwa mkatoliki lakini wale washauri wake wakapanga fitna na kumpindua kupitia binamu zake waliokuwa wantawala amsterdam wa protestant wa kiCalvin William of Orange katika mapinduzi yajulikanayo kama Glorious revolution (Mapinduzi matukufu)...etc etc

point ni kwamba, kanisa la Anglican lina historia moja kubwa sana ambayo hadi linasambaa duniani ni ya muda mrefu sana tangu 1500s huko...haya ya Tanzania ni matokeo ya power struggles ambazo zipo tangu muda ingawa pia madhehebu mengine yapo pia.
 
Screen-Shot-2017-01-08-at-4.24.38-PM.png

Sakata la Mgogoro wa Kanisa Anglikana Tanzania Dayosisi ya Dar es salaam,linazidi kuchukua sura mpya,kufuatia Askofu wa Dayosisi hiyo,Dokta Valentino Mokiwa,kugoma kujiuzulu na kustaafishwa kwa manufaa ya Kanisa hilo kama alivyotakiwa na Mhasham Askofu wa Jimbo kuu la Tanzania,Dokta Jacob Erasto Chimeledya.

Hatua ya Dokta Mokiwa,kutakiwa kufanya hivyo,ni agizo la nyumba ya maaskofu la kuundwa tume ya Askofu Mkuu wa Kanisa hilo,kuchunguza tuhuma kumi zilizokuwa zinamkabili Dokta Mokiwa,pamoja na nyinginezo, za ukosefu wa maadili,ikiwemo kufuja mali za kanisa na kuingia mikataba kiholela yenye viashiria vya rushwa katika maeneo ya Buza,ikiwemo pia kutoa daraja la Ushemasi,Upadre,na Ukanon,kwa katibu wa Dayosisi,Mkristo ambaye ametengana na mkewe na kuoa mke mwingine kiserikali kinyume na kanuni ya kanisa kuhusu ndoa.

Waandishi wa Channel Ten,wamefika katika nyumba zinazodaiwa kutelekezwa na Dokta Mokiwa ikiwemo Silver Oak ya Upanga,na ya Mtaa wa Uganda Ostabei, ambapo imedaiwa kuwa ameiacha na kwenda kupanga huku kanisa likimlipa pango la shilingi milioni 3 kwa mwezi miaka zaidi ya miaka sita.

Dokta Mokiwa jana aligoma kupokea barua yake kutoka kwa Dokta Jacob Erasto Chimeledya,na baadhi ya waamini wa kanisa hilo katika nyakati tofauti,wamezungumzia hatua ya kutakiwa kujiuzulu na kustaafishwa Dokta Mokiwa.

Katika hatua nyingine,Dokta Valentino Leonard Mokiwa,kupitia kwa Afisa habari wake,Yohana Sanha,amedai kuwa mchakato uliotumika kumuhukumu ni batili na kwamba bado yeye ni Mkuu wa Dayosisi ya Dar es salaam kwa hiyo hataachia ngazi hiyo ya Uaskofu.

Source: Channel Ten
Kweni katiba inasema nn juu ya askofu mkuu kumfukuza askofu wa jimbo? Na je kama waumini wataskilizwa kwa maneno yao hawamtaki askofu huyu au yule unazani maaskofu wangapi watabaki haohao waangerikana hawamtaki askofu wao wa mwanza tena wachagizaji ni wachungaji lkn wanajua hawana mamlaka hayo?ila MUNGU tu lkn hawa maaskofu wamechaguliwa na nani?nazani ni tamaa na kuzani kuwa mambo ya mungu ni kama siasa lkn pia wakumbuke kuna laana juu ya tabia hiyo ya kuwa fukuza hata kuwapiga wapakwa mafuta wa mungu laiti wangerijua wala hawana mamlaka hayo.
 
Mkuu ukiona tai wengi wamekusanyika mahali jua kuna mzoga hapo.

Ulaji unawasumbua sana viongozi wetu hawa, hawezi kuachia ngazi kuacha ulaji mnono ulioko pale, japo ana tuhuma nzito sana hata kuziandika mtandaoni ni aibu.

Ni aibu kubwa sana.
 
Back
Top Bottom