SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 49,974
- 75,056
Suala la kushambuliwa kw Dr. Mokiwa siyo la kidini wala uamsho hawahusiki, wahusika wakuu ni walewale watesi wa Dr. Ulimboka na Absalom Kibanda.Hawa watu ni wataalamu wa kusoma alama za nyakati kisha kufanya tukio na baadae kulioanisha na mazingira waliyoyatengeneza wenyewe ili kukwepa kushukiwa. Walianza kwa kutengeneza mgogoro hewa ndani ya Chadema na kumgombanisha Marehemu Chacha Wangwe na mgogoro uliposhika kasi wakamuua Chacha Wangwe wakiamini kuwa jamii yote itawanyoshea mkono viongozi wa Chadema jambo ambalo lilishindikana. Wamechukulia kuondoka kwa Kibanda Freemedia kama kigezo kuwa alikuwa na ugomvi na mwajiri wake, haraka haraka wakafanya jaribio la kumuua kisha wakaanza kusamabaza uongo wao hata hapa jamvini kuwa mwajiri wake wa zamani ana mkono katika shambulio hilo.Kutokana na tishio la wana uamsho kwa viongozi wa dini ya Kikristo wakaona ni wakati muafaka wa kummaliza Dr. Mokiwa wakiamini kuwa mshukiwa mkuu atakuwa uamsho.IKumbukwe kuwa Dr. Mokiwa ni moja wapo wa viongozi wachache wa dini ambao ni majasiri kuikosoa serikali hadharani. Tusidanganyane hapa, uamsho katika hili la Mokiwa hawahusiki.