Askofu Mokiwa avamiwa, mlinzi wake taabani!

Askofu Mokiwa avamiwa, mlinzi wake taabani!

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,159
Reaction score
162,578
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk. Valentino Mokiwa, amevamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake, Mbezi Luis, eneo la Mashirikiano, jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya kumkosa walimjeruhi mlinzi wake.

Taarifa za uhakika zilizolifikia gazeti hili, na kuthibitishwa na Askofu Mokiwa mwenyewe, zinaeleza kuwa watu hao watatu ambao mpaka sasa hawajafahamika, walifika nyumbani kwake hapo juzi majira ya saa tisa usiku wakitaka kumuona askofu huyo.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili, mmoja wa watu wa karibu na askofu Mokiwa alisema watu hao walifika kwa lengo la kutaka kuingia ndani ili waweze kumuona, hali iliyomfanya mlinzi kuwazuia.

“Wale watu walipofika kwa mlinzi walimuuliza kuwa askofu yupo.. mlinzi akawajibu kuwa hayupo, wakamuuliza tena mama je (mke wa askofu), akawajibu kuwa wote hawapo, baada ya kujibiwa hivyo walianza kumpiga mlinzi kwa madai kuwa hataki kuonyesha ushirikiano, walimpiga na kumjeruhi vibaya kwa mapanga na hadi sasa amelazwa katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha,”,kilisema chanzo hicho.

Alisema mlinzi huyo aliyetambulika kwa jina la Fred, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 45, alipigwa hadi kuzimia kabla ya watu hao kutokomea kusikojulikana.

Habari zilizothibitishwa na mtu mmoja wa karibu na Askofu huyo zinaeleza kuwa, mlinzi huyo aligoma kuwaambia ukweli watu hao kwa sababu alikwishaonywa kuwa makini na wageni wa aina yoyote wanaofika nyumbani hapo kumuulizia Mokiwa.

Mtoa habari wetu huyo aliliambia gazeti hili kuwa wakati mlinzi huyo akivamiwa na kucharangwa mapanga, Askofu Mokiwa pamoja na mke wake walikuwemo ndani ya nyumba lakini hawakuweza kusikia lolote, kutokana na lango la kuingia nyumbani kwake kuwa mbali na nyumba.

“Askofu alishamtahadharisha mlinzi kwa sababu wiki mbili zilizopita alishatoa taarifa polisi kuhusiana na vitisho alivyokuwa akipewa na watu wasiojulikana, kikubwa kilichosaidia ni kwamba nyumba ya askofu iko umbali kidogo, lakini wangemdhuru,” alisema mtoa taarifa wetu huyo.

Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Dickson Chilongani, alisema wamepokea taarifa hizo kwa masikikito na kwamba wanasubiri taarifa rasmi kutoka kwa askofu ili wazifanyie kazi.

“Tayari tumepata taarifa, lakini nimejaribu kumtafuta askofu Mokiwa nimeambiwa kwamba anahojiwa na vyombo vya usalama, tunasubiri amalize tuzungumze naye ili tulifuatilie kwa ukaribu suala hili, kwani ni tukio la kushtusha,” alisema Chilongani.

MTANZANIA Jumapili lilimtafuta Askofu Mokiwa kwa njia ya simu ambapo alithibitisha juu ya habari za kuvamiwa nyumbani kwake na akamtaka mwandishi wa gazeti hili amtafute baada ya dakika 40.

Mwandishi wa gazeti hili alimtafuta tena Mokiwa baada ya dakika 40 kupita simu yake, iliita bila mafanikio na alipotumiwa ujumbe mfupi wa kumkumbusha aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu kuwa ana ugeni wa serikali na kulitaka gazeti hili limpigie baada ya dakika 45.

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyella, alisema amesikia taarifa hizo, lakini hajazipokea rasmi ofisini kwake.

“Ni kweli hata mimi nimesikia, lakini hazifafika ofisini kwangu rasmi, nitafute baadaye naweza kuwa na taarifa sahihi, kwa sababu wao wako Mbezi, inawezekana hizo taarifa zipo huko Mbezi katika kituo cha polisi cha Mbezi kwa Yusuph,” alisema Kamanda Kenyella.

Baadaye Kamanda Kenyella alipotafutwa kuthibitisha tukio hilo, simu yake iliita bila kupokelewa, ambapo MTANZANIA Jumapili ilipata taarifa kwamba wapelelezi wakiongozwa na Kamanda Kenyella, walikwenda nyumbani kwa Askofu Mokiwa kwa ajili ya kufuatilia tukio hilo.

CHANZO:MTANZANIA JUMAPILI.
 
Hii ndo amani na utulivu tulionao ! Watanzania amkeni usingizini hapa hamna amani wala utulivu, ukiachilia mbali matukio makubwa ya Ulimboka, Kibanda na wengineo nina marafiki zangu wengi ambao usiku hawalali kwa uwoga wakiofia usalama wao, alafu wanakuja wanasiasa wanaimba wimbo walioukariri wa amani na utulivu. Shame on them!
 
Aaaah wakuu Sasa hii ni noma. Tunahitaji Watanzania tulindwe na majeshi ya ECCOWAS?
 
Hakika zile SMS za matamko ya kuwaondoa katika sura viongozi wa dini hakika naanza kuziamini!! Katika vipeperushi na sms zilea walitaja mokiwa, Malasusa, Pengo, na wengine!!! Kaeni Chonjo na kama serikali inataka amani ya nchi hii iendelee basi viongozi wote wa dini za kikristu wapatiwe ulinzi wa serikali. Wakati huo huo ule udini uliolelewa kwa awamu ya nne basi kabla haijamaliza muda wake waone ni namna gani ya kumaliza tatizo lao walilolilea.
 
Hii ni nchi ya ajabu sana, nikiwa natokea mikoani nikiingia jijini DSM nakaribishwa na kanda zinazohubiri chuki za udini pale ubungo, tena wameweka kipaza sauti ! najiuliza hivi nchi hii ina uongozi au hakuna. Kama alivyowahi kueleza mwandishi Johnson Mbwambo inaonekana nchi iko kwenye automatic pilot, yaani inajiendesha kila mmoja anafanya analotaka bila governance!!!
 
ebr13.6"hata twathubutu kusema,bwana ndiye anisaidiye,sitaogopa;mwanadamu atanitenda nini?"mungu awasambaratishe kwa njia saba maadui wote...!
 
Hakika zile SMS za matamko ya kuwaondoa katika sura viongozi wa dini hakika naanza kuziamini!! Katika vipeperushi na sms zilea walitaja mokiwa, Malasusa, Pengo, na wengine!!! Kaeni Chonjo na kama serikali inataka amani ya nchi hii iendelee basi viongozi wote wa dini za kikristu wapatiwe ulinzi wa serikali. Wakati huo huo ule udini uliolelewa kwa awamu ya nne basi kabla haijamaliza muda wake waone ni namna gani ya kumaliza tatizo lao walilolilea.

watakuwa ni waislamu kwasababu hata mtu akigombana na mke wake ni waislamu UKITAKA KUMUUA MBWA MPE JINA BAYA!sema ana kichaa atauwawa
 
Kazi ipo Kiwete, Kinana na CCM kwa ujumla hamwezi kukwepa kikombe hiki coz ndio waanzilishi wa Single ya UDINI karibu tunapata ALBUM kamili. Nahofia hatuweiz kufika uchaguzi ujao tukiwa salama kama SERIKALI hawatachukua hatua stahiki. Ni mbaya sana hii lakini yote yana mwisho
 
"...For your sake we are killed all day long; We are accounted as sheep for the slaughter." Yet in all these things we are more than conquerors through Him who loved us.
For I am persuaded that neither death nor life, nor angels nor principalities nor powers, nor things to come, nor height nor depth, nor any other created thing, shall separate us from the love of God which is in
Christ Jesus Our Lord."
 
ebr13.6"hata twathubutu kusema,bwana ndiye anisaidiye,sitaogopa;mwanadamu atanitenda nini?"mungu awasambaratishe kwa njia saba maadui wote...!
 
Mwamsho kazini sasa wamehamia bara.. Baada ya fbi kuzingira z'bar.
Ni mwamsho tu hakuna wengine ushahidi wa vipeperushi upo.

Ewe sheikh Ilunga vijana wako hao, haya bwana tumalize uishi wewe na watukufu wenzako Tanzania hii..
 
Vyombo vya usalama havina kazi hapa tanzania! Ndio maana tunatumia CIA!
 
Kuna vijamaa vina kanzu chafuuuu huku mbagala, tandika na buguruni wanauza kanda za uchochezi kila siku lakini nashangaa kova hawakamati au ndio wanatafuta askofu wa kubalance kama kule geita.
 
watakuwa ni waislamu kwasababu hata mtu akigombana na mke wake ni waislamu UKITAKA KUMUUA MBWA MPE JINA BAYA!sema ana kichaa atauwawa

Nikianza ku-connect dot kuanzia Zanzibar mauaji ya Padre na kumuumiza mwingine kwa risasi (alikuwa afe siku zake hakizikuwa zimetimia) halafu eti wahusika hawakukamatwa!!!! Wale waliokamatwa juzi wakiwa na document kibao cha kukachifu dini, na yale ma cd na vipaaza sauti vya kuhubiri udini na kutukana pale ubungo na manzese darajani!! Basi ninasema Mbwa huyo jina lake ni baya sana anazidi yule mwenye Rabbies na inatakiwa auawe!!
 
Mabifu ya Uongozi Kanisani mwao bado yanaendelea! apa hakuna cha uamsho wala nini...wanajuana wenyewe na 10% za miradi yao
 
Kuna vijamaa vina kanzu chafuuuu huku mbagala, tandika na buguruni wanauza kanda za uchochezi kila siku lakini nashangaa kova hawakamati au ndio wanatafuta askofu wa kubalance kama kule geita.

Asante sana mkuu kwa kusema ukweli. Sasa je hii nchi haina usalama wa Taifa? Si tunaishi nao kwenye jamii zetu kuanzia uswazi (mainfoma wapo), wauza mchicha, wapiga viatu rangi, wauza kahawa, wauza bidhaa za mkononi kwenye mabaa huku wamevalia suti kali kabisa!! Hawa wote hawana taarifa za mipasho hiyo ya kidini? Au wakipelea taarifa hazifanyiwi kazi kwa kuwa eti mnataka kutuletea mambo ya udini? Ingekuwa ni Wakristu wanapiga kelele kama mbwa mwitu kutukana na kukachifu dini za wengine basi ungeone kivumbi? Wakati wa Nyerere na Mkapa mbona sikuona wakristu wakiamka na kuanza kujirusha kwa CD chafu za uchochezi? Hawa mambo tuliyashuhudia wakati wa Mwinyi (kumbukeni sekeseke la Mwembechai Magomeni na kwinginezo, msikiti wa kwamtoro), leo hii yakaibuka tena awamu ya nne!!!! Sasa tuseme nini sasa!!Political and Religion analysts hebu tusaidieni hapa!!
 
Back
Top Bottom