Askofu Mokiwa atupa kombora, awaponda wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu Mokiwa atupa kombora, awaponda wabunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Apr 24, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  SIASA zisizozingatia thamani ya utaifa zimetajwa kusababisha baadhi ya wanasiasa kutolewa kafara na wananchi kushawishika kuamini kwamba wanasiasa hao ndiyo wabaya wakati watu wanaofanya mambo mabaya nchini ni wengi.

  Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Askofu Dk. Valentino Mokiwa,amesema, kukosekana kwa siasa zinazozingatia utaifa, kumesababisha watu kutukanana, kuchimbana na kunyosheana vidole, huku kundi la wachache likionekana ndilo lenye watu wabaya katika jamii.

  “Mfano hivi sasa neno ufisadi limegeuka kuwa silaha ya baadhi ya watu kupigana; wabaya wako wengi, lakini kuna watu wamepandikizwa kuonekana ndiyo wabaya miongoni mwa jamii.

  Kumbuka hata asiyefanya kazi ni mtu mbaya, mwizi ni mtu mbaya, wabaya ni wengi tu, lakini wachache ndiyo wamefanywa kuwa wabaya,” alisema jana wakati anazungumza na HABARILEO. Askofu Mokiwa alisema hayo wakati akizungumzia ujumbe wake wa Pasaka mwaka huu.

  Alisema, Tanzania limekuwa Taifa la wavivu, lakini lenye watu wasemaji sana na wajuzi wa kunyoosheana vidole, kwa sababu kuna baadhi ya watu wajanja ambao wanavuruga amani kwa kujiona ni bora zaidi ya wengine na kugeuza wenzao wabaya katika jamii.

  Askofu Mokiwa alisema, yote haya yanatokana na Taifa kukumbwa na msongo wa mawazo, ambao unaonekana kuongezeka kwa kasi na matokeo yake ni kuwa na nchi inayoamini demokrasia lakini ikipoteza mwelekeo wa demokrasia.

  “Hivi sasa tuna viongozi ambao hawaongozi, kwa sababu wana mamlaka, lakini wanategemea kuongozwa na wengine na kama hali itaendelea hivi, Taifa litakuwa likielekea pabaya,” alisema.

  Alisema, pia kutokana na Taifa kuwa na msongo wa mawazo, gharama za maisha zimekuwa zikiongezeka, ingawa kuna wachumi wengi lakini hawajui wanachokifanya na kuongeza kuwa kilichobaki ni kumwomba Mungu.

  Kwa mujibu wa Askofu Mokiwa, hali ilivyo sasa, Watanzania wamekuwa wakifikirishwa na vyombo vya habari na wanasiasa, na kueleza kuwa hiyo ni dalili mbaya kwa Taifa na kulielekeza tukio lililotokea hivi karibuni bungeni, kuwa ni mfano halisi wa mwelekeo wa kutetereka kwa Taifa.

  Alikuwa akimaanisha wabunge kuzomeana na baadhi yao kutaka mlango ufungwe ili wapigane kutokana na kutofautiana juu ya masuala mbalimbali, ambapo alisema ni jambo la aibu.

  Askofu Mokiwa alisema, wakati Watanzania wakisherehekea Pasaka, wanapaswa kubadilika kwa kupunguza kusemana na kunyoosheana vidole na kuwataka kuacha tabia ya kujichukulia sheria midomoni kwa kuhukumu wengine, ili nchi isielekee kubaya.

  Alisema dhambi ya kusema sana na kunyoosheana vidole, imekuwa shida kubwa, kwani imeingia hata makanisani na kusababisha kukosekana kwa amani. “Waumini hawana amani, viongozi wa dini hawana amani, kwa sababu kila mmoja anaona ndiye bora kuliko mwingine.

  “Tujiheshimu, tuache dhuluma, wanaotuongoza wasiwe wavivu na wasimame katika nafasi zao … tuishi kwa umoja na kuthamini utaifa wetu, kwani ndicho chanzo cha amani,” alisema.

  Akitoa mtazamo wake wa kidunia, alisema amani imechafuka ndiyo maana maeneo ya Mashariki ya Kati, viongozi wanaondolewa madarakani, lakini wanaowaondoa hawajui nani wa kuwaweka badala, huku mataifa ya Magharibi nayo yakiendelea kuonesha ubabe na vitisho dhidi ya mataifa mengine.

  Wakati huo huo, Askofu wa Kanisa la Amani Christian Center la Tabata, Dar es Salaam, Lawrence Kameta, alisema Watanzania wanatakiwa kusherehekea sikukuu ya Pasaka kwa kutambua kusudi la Bwana Yesu ambaye alikuja duniani kuwaletea wanadamu uzima na amani katika maisha.

  “Tunatakiwa kujua Yesu alikuja ili wanadamu tupate uzima na amani katika maisha kwa njia ya kumrudia Mungu kiroho … na kumrudia kiroho ni mabadiliko ya ndani ambayo matokeo yake yanamfanya mtu kuwa mwadilifu kwa Mungu na wanadamu,” alisema.

  Hata hivyo alisema mabadiliko hayo hayawezi kupatikana bila kumkubali Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha ya mtu binafsi na kwamba watu wote wakipokea Pasaka kwa njia hiyo itakuwa haina maana ya kuendelea kuishi maisha ya uovu na kuonewa na ibilisi.

  Aliitaka jamii isherehekee kwa kuchukua hatua ya kuyatenda na kutambua kusudi la Yesu katika sikukuu ya Pasaka.

  Habari Leo
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Askofu awaonya wanasiasa, viongozi mafisadi
  ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Dodoma, Mhashamu Gerson Nyaisonga amewaonya viongozi wa serikali na wanasiasa nchini kuacha tabia ya kujitafutia umaarufu binafsi kwa njia za kifisadi huku wakitishia kutumia gharama yoyote hata ikibidi kupoteza uhai wa wengine wasio na hatia ili kukidhi mahitaji yao.

  Kiongozi huyo wa dini mkoani Dodoma alitoa changamoto hiyo wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu ambapo aliwaonya pia watumishi wa umma wanaosimamia haki za raia katika vyombo vya Dola kuacha vitendo vinavyokwenda kinyume cha mapenzi ya Mungu.

  “Tunaosimamia haki tusiwabambikize watu makosa kwa kuwasingizia na kuwaweka katika mazingira ya kulaumiwa wakati siyo makosa yao.

  Mara nyingi yametokea makosa ya kuwataja watu kwa makusudi na kuhusishwa na makosa ambayo hawakuyatenda na kulazimika kupokea adhabu zenye mateso makali bila hatia,” alisema Askofu Nyaisonga.

  Alitoa mfano kuwa, Askofu James Sangu wa Jimbo la Mbeya ambaye kwa sasa ni marehemu, aliwahi kutembelea magereza na kumkuta mwanamke aliyehukumiwa kifungo cha maisha kwa kusingiziwa kosa la kumuua mumewe, lakini baada ya kufuatilia yeye mwenyewe kwa kushirikiana na vyombo vya haki kwa makini ilithibitika alifungwa kwa makosa na kuachiwa huru kwa kukutwa hana hatia.

  Alifafanua kuwa watu wengi wasiojua sheria wamekuwa wakishindwa kujitetea na kutoa ushahidi wa kutosha mahakamani na hivyo, kuwapa fursa walalamikaji wenye hila kuweka ushahidi wa uongo.

  Habari Leo
   
 3. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Maoni ya Dr Mokiwa ni ya maana kabisa, huyu kijana amewahiwa tu na watu wa dini lakini ni kati watanzania wenye elimu nzuri toka marekani, lakini pia hapa alipo atashauri nchi vema akiwa Baba Mtakatifu.
  kina Sitta wanatoa hewa ovya juu ya kina Lowassa, ok, Lowassa amedhubutu kuvunja amri ya Misri kwamba atakaechota maji ya ziwa Victoria watamshambulia kwa madege ya kivita, eti maji mto nile anoanzia Mwanza yanamilikiwa na Misri na Sudan, Lowassa kapeleka maji mikoa ya kanda ya ziwa akiwa waziri,
  yeye Sitta? maslahi yetu EAC yanazidi kushuka tu, yeye anasema ovyo akitafuta sifa, mwakyembe si anamiliki kampuni ya kifisadi singida? ilichota hela za umma mwaka 2004 kama sijakosea, ili itengeneze nishati ya hewa, sijui hewa itoke tumboni kwake?
  Watanzania wanadanganywa tu, na hii sumu haitatoka ya wachache kuonekana wabaya, wakati wanaosema ndio wauwaji wa nchi.
  Asante Baba Askofu Mokiwa
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Haya mahubiri ya dini wakati wa pasaka kuwa siasa sijui yatatupeleka wapi?..
  Kifupi mimi sijamwelewa hata mmoja wao kwani wao wanalaumu watu wengine wakati wao wakifanya hayohayo - KALAUMU baadhi ya WATU..
  Maaskofu/Masheikh, fundisheni dini na sii kutazama watu wanafanya nini ili mpate kufundisha. mafundisho ya dini yameandikwa ktk vitabu vitakatifu na ndio elimu mnayotakiwa kuwapa wananchi sii kutazama wanafanya nini ndio mmpate somo la kufundisha. kazi ya zimamoto sii dini wala kazi yenu bali unawafunza wananchi kujikinga na moto..
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mkandala tukupe darasa kidogo.
  Viongozi wa dini wanahudumia na kuwalea wananchi wote wanasiasa wakiwa ni moja ya waumini wao kimwili na kiroho. Kwa vile roho hatuioni kwa vile ni nguvu ya kimungu ndani ya miili ya watu, viongizi hao wa dini wanawahudumia binadamu wenye mwili na roho.

  Ni wajibu wa viongozi wa dini kuonya na kutoa tahadhari katika mambo ya msingi kiroho, kisiasa, kimaadili na kiuchumi kwani yote hayo ndiyo yanayomsibu binadamu. Katu binadamu hatakuelewa mhubiri wakati amezungukwa na matatizo chungu nzima.

  Mkandala mbona hulalamikii huduma za kimwili zitolewazo na mashirika ya dini kama elimu, afya nk. ila wanapoonya ndo unalalamika, au ni mmoja wapo wa mafisadi?

  Hawa watatu Lowasa, Rostam na Mzee wa Vijisent wametolewa Kafara baada, wakati hao walitumiwa kwa manufaa yao waliopo madarakani. Bora safu yote ijisafishe vinginevyo ni kuruka jivu na kukanyaga moto.
   
 6. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Sijakuelewa kuwa unamaanisha pesa ya kifisadi ni ikiwa nyingi au ni upatikanaji wake? Mokiwa sawa lakini wewe sijakuelewa mahali fulani kuhusu Mwakyembe! Fafanua pls
   
 7. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Nadhani na wewe ni mmoja umepotea, hata mifano iliyoko ktk vitabu vitakatifu inahusu matendo ya watu. Watu wakemewe waache uovu, isipokuwa wasitumie nafasi hiyo kutugawa ktk misingi ya dini, ukabila na rangi. Wasichochee vurugu wala chiki، unaonekana mgeni na maandiko matakatifu mkuu.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tusichanganye ufisadi na jitihada binafsi za mtu kiuchumi, vinginevyo kale katabia ka wivu kataota mizizi
   
 9. Mushobozi

  Mushobozi JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2011
  Joined: Aug 20, 2007
  Messages: 542
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  <p>
  </p>
  <p>&nbsp;</p>
  na kale ka tabia ka uvivu katafuatia.
   
 10. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Wengine huku tumetumwa ujue! Watu wanafanya kazi kwa kujaribu kuchafua watu wema wakidhani kwa njia hiyo, wanasafisha uchafu wa waliokwisha chafuka
   
Loading...