Askofu Manase: Kila kanisa likitoa waraka wake taifa halitakalika

Makanyaga

Platinum Member
Joined
Sep 28, 2007
Posts
11,809
Reaction score
7,561
Na Eliya Mbonea, Arusha

Askofu Mkuu wa Makanisa ya Babtisti Tanzania, Mchungaji Arnold Manase amewataka viongozi wa dini kushauri kwa namna njema bila kutabiria nchi mambo mabaya kwani ubaya huenea haraka kuliko wema.

Aidha, amesema kila dhehebu nchini likisimama na kutoa waraka wake taifa halitakalika.

Askofu Manase ameyasema hayo leo Jumapili Aprili Mosi, jijini Arusha wakati akitoa salam kwenye Ibada ya Pasaka katika Kanisa la Jerusalem Babtisti lilipo Ngarenaro mjini Arusha.

Kupitia Ibada hiyo, Askofu Manase amewaomba wadau wa amani nchini, ikiwamo Serikali kukaa na wadau ili kujadili mustabali wa taifa.

“Tunahitaji kuomba amani ya Mungu itawale, kama ambavyo Yesu Kristo alivyotuachia amani yake.

“Tukiwa kama viongozi wa dini kama kuna mambo tunaweza kushauri basi tuyashauri kwa namna njema tusitabirie nchi mambo mabaya Kwani ubaya unaenea haraka kuliko wema, nawasihi tuhubiri amani,” amesema Askofu Manase.

Pamoja na mambo mengine, Askofu Manase katika Ibada hiyo ameongoza maombi kuomba hekima kwa viongozi wa Serikali, madhehebu yote nchono ili hekima ya Yesu Kristo ikatawale kwenye mioyo yao.

Source:ASKOFU MANASE: KILA KANISA LIKITOA WARAKA WAKE TAIFA HALITAKALIKA
 
Huyu askofu (kama kweli ametamka hayo maneno) basi ana akili fupi sana! Hivi kweli nchi haitatawalika kwa watu kukemea uovu na mauaji? Mimi nadhani tusipokemea ndiyo nchi haitatawalika.
 
Umenena vema Askofu, madhabahu ya Mungu ni madhabahu njema , yenye kuleta uzima na baraka, Mungu akubariki sana mtumishi mwema wa.Mungu
 
Na jaribu kuvuta kumbukumbu angalau nipate mradi wowote wa kijamii kama shule, hospitali, chuo nk. vinavyomilikiwa na kanisa la askofu huyu sioni nisaidieni wadau....
 
Kila Kanisa au dhehebu lina mfumo wake wa kujiendesha. Kuna ambao hutoa nyaraka kuwaongoza waumini wao katika masuala wanayoyaona muhimu kwa wakati huo. Ikiwa Kanisa/dhehebu lako halifanyi hivyo basi usiige.
 
Back
Top Bottom