Sidhani kama wanaweza wakawa wanaongeza ada based on nothing lazima ipo sababu. Tukumbuke gharama za maisha zinapanda kila kukicha na pia fedha yetu inashuka thamani. Tusikimbilie kulaumu tu bila ya kujua sababu. Hivi ktk uendeshaji wa hicho chuo kama kuna nakisi za kiuendeshaji mnadhani nani alipie?
Ada milioni 2.5 kwa mwaka huu ni ufisadi wa hali ya juu hawa wana fanya biashara sio wanaelimisha jamii.
Naomba kuuliza swali kidogo hususan kwa wale wakulima: Bei za gunia moja ya yafuatayo ni kiasi gani?
1. Mahindi
2. Maharage
3. Mchele
4. Ulezi (mbege)
5. Viazi vitamu (vingamba)
6. Viazi mviringo (vitofu)
7. Karanga
8. Nyanya
9. Vitunguu
10. Mengineyo
Elimu ni ghali mkuu.
Siyo ufisadi.
Kwa maana hiyo watoto wa mafisadi ndo watakao pata elimu za juu na watoto wa maskini wataishia form six maana mkulima wa alizeti au viazi atazichanga mara ngapi kupata hiyo 2.5m
kama hujui kitu bora unyamaze wewe..malasusa ameingizwa mkenge na viongozi waliopo pale tumaini university..na nawaambieni mtakaochangia pale pesa zitaliwa sana..na huyu malasusa anajidai kama hajatokea umaskini..yeye nilifikiri angekemea hili swala..lkn ye aongea upuuzi..kwakweli hata sadaka sasa mimi binafsi kutoa kanisani napata kigugumizi..kwanin nichangie wkt askofu mkuu mwenyewe hanijali kabisa..malasusa nadhan kazi imemshinda..serikali iingilie kati na kuwafungia tumaini..hawatufai..wao kama watu wanaofaidika na misamaha ya kodi leo wanatutungua miada mikubwa namna hii..mimi sibishi kodi kupanda..ninachobishia ni justification ya kutoka 1.5 mil to 2.5 mil ndiyo hakuna hiyo kitu.
Unadhani ipo transparency inayoeleweka kwenye zile sadaka zetu wanazokusanya kanisani? Kwenye chaguzi za maaskofu nimesikia habari za kutatiza sana. KKKT imekuwa ya ajabu sana hasa inapohusu utoaji wa sadaka.
Mwezi uliopita, muumini alileta kuku wawili kama sadaka. Nimezoea kuona zaka ikiombewa kwanza kabla ya kuwekwa kwenye mnada, ila mchungaji hakufanya hilo siku hii.
Mchungaji akawasimamisha wazee/washarika wawili na kuwaita waende mbele. Akawauliza kila mmoja "wewe utatoa shilingi ngapi"? Mmoja akasema elfu 50, mwingine huku akipata tabu ataje nini, akajitutumua akasema 47. Mchungaji akawaambia warudi waende wakaketi. Tulidhani wale wazee kila mmoja angepewa kuku mmoja.
Mchungaji akatoa maelekezo pale pale kwamba, kuku mmoja ni wa mchungaji na mwingine ni wa mhubiri mgeni aliyefika kuhubiri siku hiyo. Washarika wakashangilia!
Nilitoka kanisani nimekasirika. Baadae nikajiuliza, kuna faida gani kwenda kanisani halafu baada ya ibada nimetoka nikiwa kwenye hali hii?
Mkuu hiki Chuo ni private, waache wenye hela hizo wawapeleke watoto wao kusoma huko. Sisi walalahoi kwetu ni SUA, UDOM, UDSM, Mzumbe n.k.
Ni sawa sawa ukalalamika kuwa St Marys Ada yao kubwa, watakushangaa watu. Kuna shule za msingi Ada zake zinazidi hata hapo Tumaini!