Askofu Malasusa aunga mkono ongezeko la ada vyuo vikuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu Malasusa aunga mkono ongezeko la ada vyuo vikuu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Pdidy, Jul 28, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  ndugu watanzania nadhani hivi sasa watanzania tunatakiwa tuanalie na watu wa chini jamani...ufisadi umeanza kufika hadi vyuo vikuu vya dini...tuna mwezi sasa tunaona tangazo la chuo cha tumaini


  **ASKOFU MKUU MALASUSA ANAOMBA WALE WENYE MAPENZI MEMA KUCHANGIA CHUO KIKUU CHA TUMAINI""

  mmmhhh sasa huyu anaomba maskini wachangie chuo wkati huo huo anashabikia ongezeko la ada ya wanafunzi kutoka millin 1.5-2.5...sasa kuna haja ya kuchangia kweli chuo kama hiki...kwa mtaji huu naona hiki watasoma watoto wa mafisadist tu...na sioni kama mkuu wetu ana haki ya kupinga ufisadi kama anasema mwenye uwezo atakuja kusoma.....


  Askofu Malasusa aunga mkono ongezeko la ada vyuo vikuu

  Na Nora Damian

  MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa ametetea mpango wa kuongezwa ada kwa Chuo Kikuu cha Tumaini kwa kuwa mpango huo, una lengo la kuboresha elimu nchini.

  Akizungumza katika kituo cha televisheni cha TBC jana, Malasusa alisema halilengi kuwatenga wanyonge bali linataka kuwawezesha kuwepo kwa shule nyingi kama zilivyo hospitali na huduma zingine za jamii.

  Malasusa aliwataka watu wenye uwezo wawasaidie wanafunzi wasiokuwa na uwezo ili wapate elimu bora.

  “Hata igekuwa shilingi moja lazima watu wakajua msingi wa ada iliyopo na elimu yoyote nzuri lazima igharamiwe,”alisema Malasusa.

  Hivi karibuni chuo hicho, kilitangaza kupandisha ada kwa asilimia 60 kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza na kiwango cha awali kilikuwa Sh 1.5 milioni na kimepanda hadi Sh 2.5 milioni.

  Hatua hiyo ya kupandisha ada imelalamikiwa na baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho na kufafanua kuwa ongezeko hilo ni kubwa.

  Baadhi ya wanafunzi hao wameuomba uongozi wa chuo hicho kufikiria upya ongezeko hilo la ada kwa kuwa wanafunzi wengi wanalipiwa ada na wazazi wao.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  Tunaitaji kuwa makini wakti wa kuruhusu vyuo kama hivi...mwanzo wakati kinaanza kilipendwa sana na hata walezi wake kufikia kusema kimekuja kuwakomboa watanzania wasio na uwezo...he leoo hi kweliiiiiiiiiiiiii kweliiiiiiiiiiiiiii tumainiiiiiiiii mmmmh haya yetu macho....ila sishauri kutoa mchango kwa chuo kama hiki nenda kwenye kambi za watoto yatima ukabarikiwe
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  INATUBIDI TUWE MAKINI SANA...VYUO VINGI VINAANZISHWA KWA MIADILI YA DINI KUSAIIDIA WANANCHI MWISHO WAKE ..........,WANAAMUA KUINGIA RASMI KWENYE BIHASARA HATARISHI....mmhhhhhhhhhh
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ada milioni 2.5 kwa mwaka huu ni ufisadi wa hali ya juu hawa wana fanya biashara sio wanaelimisha jamii.
   
 5. L

  Lukundo Member

  #5
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ikumbukwe kuwa wakati vijana wa mlimani wanapinga mifumo kandamizi ya vyou tanzania, miongoni mwa wanafunzi ambao hawakuungana na matakwa ya wanafunzi wale, walikuwa wanafunzi wa vyuo private, sasa yanawakuta, na kwa sababu hamna umoja, mtalipa tu.
  SAUT wana maandishi katika form zao za matokeo ya maendeleo chuoni, yanasema, NO FEES, NO EDUCATION, Maneno haya hayana dini hata kidogo, na ndio ukweli, elimu ni ghali, na kuendesha vyuo ni ghalama.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sidhani kama wanaweza wakawa wanaongeza ada based on nothing lazima ipo sababu. Tukumbuke gharama za maisha zinapanda kila kukicha na pia fedha yetu inashuka thamani. Tusikimbilie kulaumu tu bila ya kujua sababu. Hivi ktk uendeshaji wa hicho chuo kama kuna nakisi za kiuendeshaji mnadhani nani alipie?
   
 7. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Naomba kuuliza swali kidogo hususan kwa wale wakulima: Bei za gunia moja ya yafuatayo ni kiasi gani?

  1. Mahindi
  2. Maharage
  3. Mchele
  4. Ulezi (mbege)
  5. Viazi vitamu (vingamba)
  6. Viazi mviringo (vitofu)
  7. Karanga
  8. Nyanya
  9. Vitunguu
  10. Mengineyo
   
 8. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa,

  Ada za shule zimepanda kuanzia chekechea mpaka sekondari, shule siku hizi zinatoza ada mpaka milioni 2-3 kwa mwaka sembuse chuo?
   
 9. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ufisadi uko wapi katika vyuo hivi?
  Acha uchafuzi.
   
 10. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Elimu ni ghali mkuu.
  Siyo ufisadi.
   
 11. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Nasubiri watakao attempt kujibu.
   

  Attached Files:

 12. Van Walter

  Van Walter Senior Member

  #12
  Jul 28, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 171
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kama hujui kitu bora unyamaze wewe..malasusa ameingizwa mkenge na viongozi waliopo pale tumaini university..na nawaambieni mtakaochangia pale pesa zitaliwa sana..na huyu malasusa anajidai kama hajatokea umaskini..yeye nilifikiri angekemea hili swala..lkn ye aongea upuuzi..kwakweli hata sadaka sasa mimi binafsi kutoa kanisani napata kigugumizi..kwanin nichangie wkt askofu mkuu mwenyewe hanijali kabisa..malasusa nadhan kazi imemshinda..serikali iingilie kati na kuwafungia tumaini..hawatufai..wao kama watu wanaofaidika na misamaha ya kodi leo wanatutungua miada mikubwa namna hii..mimi sibishi kodi kupanda..ninachobishia ni justification ya kutoka 1.5 mil to 2.5 mil ndiyo hakuna hiyo kitu.
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwa maana hiyo watoto wa mafisadi ndo watakao pata elimu za juu na watoto wa maskini wataishia form six maana mkulima wa alizeti au viazi atazichanga mara ngapi kupata hiyo 2.5m
   
 14. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mkuu hiki Chuo ni private, waache wenye hela hizo wawapeleke watoto wao kusoma huko. Sisi walalahoi kwetu ni SUA, UDOM, UDSM, Mzumbe n.k.
  Ni sawa sawa ukalalamika kuwa St Marys Ada yao kubwa, watakushangaa watu. Kuna shule za msingi Ada zake zinazidi hata hapo Tumaini!
   
 15. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Unadhani ipo transparency inayoeleweka kwenye zile sadaka zetu wanazokusanya kanisani? Kwenye chaguzi za maaskofu nimesikia habari za kutatiza sana. KKKT imekuwa ya ajabu sana hasa inapohusu utoaji wa sadaka.

  Mwezi uliopita, muumini alileta kuku wawili kama sadaka. Nimezoea kuona zaka ikiombewa kwanza kabla ya kuwekwa kwenye mnada, ila mchungaji hakufanya hilo siku hii.
  Mchungaji akawasimamisha wazee/washarika wawili na kuwaita waende mbele. Akawauliza kila mmoja "wewe utatoa shilingi ngapi"? Mmoja akasema elfu 50, mwingine huku akipata tabu ataje nini, akajitutumua akasema 47. Mchungaji akawaambia warudi waende wakaketi. Tulidhani wale wazee kila mmoja angepewa kuku mmoja.

  Mchungaji akatoa maelekezo pale pale kwamba, kuku mmoja ni wa mchungaji na mwingine ni wa mhubiri mgeni aliyefika kuhubiri siku hiyo. Washarika wakashangilia!

  Nilitoka kanisani nimekasirika. Baadae nikajiuliza, kuna faida gani kwenda kanisani halafu baada ya ibada nimetoka nikiwa kwenye hali hii?
   
 16. Van Walter

  Van Walter Senior Member

  #16
  Jul 28, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 171
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hatupingani na kupanda..tumia akili wewe..tunachokibishia hapo ni kutokuwepo na justification ya kutoka mil 1.5 mpaka mil 2.5
  suala la kupanda kwa ada ni la kawaida..sisi tunasema kuwa hakuna justification ya kupandisha ada for over 60%...kutoka 1.5 mil kwenda 1.7 mil angalau ingekuwa justifiable..huo nimetoalea kama mfano tu.lkn huyu malasusa ametuangusha sana na chuo chao cha tumaini kwa upandaji uliokuwa mkubwa namna hiyo.
   
 17. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwa kifupi, HII ADA ITAPANDA SANA, TENA SANA. huu ni mwanzo tu. hiki ni chuo cha private, hakipati pesa za selikali za ruzuku kama vyuo vya selikali. this is a private university. na wanayo haki ya kukupokea au kukukatalia hata kama utakuwa ume meet requirement zote. kimeanzishwa si kwa pesa za selikali, ni za kanisa. kwanza kilitakiwa kisomeshe wakristo tu, hata hivyo wanafanya ubinadamu tu kupokea watu wa kila dini.

  pale wanatakiwa kuwalipa maprofesa mshahara wa kutosha ili pamprof wafundishe vizuri na ili wawavutie maprof na madocta wengi kuomba and kufanya kazi pale, hivyo wanayo haki ya kupandisha ada wapendavyo. selikali haina haki wala sababu yoyote, kwasababu selikali ni masikini, inasubiri mashirika ya dini yawasaidie kujenga vyuo, selikali ni ya kifisadi. mabilion wanayoiba yanatosha kabisa kuwalipia watz maelfu kujiunga na tumaini hata kwa ada ya million tano kwa mwaka. kwahiyo naomba nyie mnaowapinga, fumbeni midomo yenu, nyamazeni, au kaombeni kuingia pale mlimani au mzumbe,hamjalazimishwa kuingia pale. kwanza kile chuo kilianza kama chuo cha biblia, ndo maana wachungaji wengi wanasoma pale iringa. ni chuo cha kanisa. pia nitashangaa kama wenye baragashia watanyoosha midomo hapa wakati wao ndo wanajidai kupambisha kadhi na oic badala ya kujenga vyuo. kaeni kimyaaaa.OK
   
 18. O

  Oshany Member

  #18
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole sana, hujui kuwa kuhani atakula hekaluni? Na KKKT tuna utamaduni wa kuwapa zawadi wachungaji wetu, ndo maana mchungaji hakukuita wewe bali aliwaita ambao wanaelewa kuwa atakapochua kuku hawatalalamika. Washarika wenzako walishangilia, wewe ikaondoka na hasira wakati pesa hukutoa wewe. Narudia kukupa pole. Kuhusu suala la ada kupanda halina kabisa uhusiano na tukio uliloelezea. na baba askofu hawezi kupinga ongezeko la ada kwani uamuzi wa kupanda hutokana na baraza la usimamizi wa Chuo kwa kuzingatia mambo mbalimbali. kama tangazo likitoka maana yake baba askofu kama mkuu wa Tumaini tayari keshashauriwa na kukubaliana nalo. tutafute hoja nyingine na wala sio kumlaumu baba askofu katika hili.
   
 19. kisale

  kisale Senior Member

  #19
  Jul 29, 2009
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  sawa nakubali ni chuo cha private hiki,ambacho kinajiendesha kibiashara,sasa haya mambo yakuja kuchangia biashara za watu yanatoka wapi?St Marys kweli ada yao kubwa ila hawajawahi kutuomba wanainchi tuwape msaada,mimi nafikiri huyu askofu anafikiri Watanzania wote akili hamna,huyu ni mnafiki,sidhani kama kuna wakumpa msaada,mimi mwenyewe nilisoma hapo kama 5yrs ago ila siwezi kumchagia hata shilingi mia mbili kwa sababu huu ni wizi mtupu.akachukue sadaka kanisani huko aendeleze biashara yao hiyo na sio kutusumbua Watanzania.
   
 20. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #20
  Aug 10, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Baba Mwalasusa angalia Watoto wako watashindwa kusoma kutokana na hali ya kiuchumi ya Nchi yetu.Kama mzazi angalia uwezekano wa kupunguza ingalao iwe 1.8 badala ya 2.5.Tunasubiri huruma yako.
   
Loading...