Askofu Laiser: Taifa bila haki ni taifa la kuangamia

Askofu Laiser: Taifa bila haki ni taifa la kuangamia

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Askofu Dkt. Isaac Kissiri Laiser wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Magharibi Kati Tabora, ametoa wito kwa Watanzania kusimama imara kutetea haki, akisisitiza kuwa bila misingi ya uadilifu na usawa taifa haliwezi kusonga mbele.

Akihubiri Agosti 24, 2025 katika ibada maalum mkoani Tabora, Askofu Laiser ameeleza kuwa haki si neno la kisheria pekee, bali ni nguzo inayojumuisha uaminifu, usawa, uadilifu na maisha yanayolingana na mapenzi ya Mungu.

Soma pia: Taifa ni muhimu kuwa na watu jasiri kama Askofu Gwajima, kwa ajili ya kutetea haki



Kwa mujibu wake, Taifa linainuliwa si kwa nguvu za kijeshi wala utajiri wa kiuchumi, bali kwa wingi wa watu wanaotenda mambo kwa uadilifu.

Askofu Laiser ameonya kuwa kupuuzwa kwa haki kumechangia kuongezeka kwa vitendo vya rushwa, uporaji, utekaji na kupotea kwa watu, huku jamii ikibaki kuimba amani bila kusimamia misingi yake.

Amesema hali hiyo ni kielelezo cha taifa linalosinzia na kushindwa kukabiliana na uovu, jambo linaloacha mianya kwa viongozi wabinafsi na wahujumu uchumi kupenya kwenye nyanja mbalimbali za uongozi.

Katika ujumbe wake, Askofu Laiser amewataka wananchi kutambua kuwa ukimya mbele ya uovu ni mchango mkubwa katika kuangamia kwa taifa. Amesisitiza kuwa hofu na mazoea ya kutozungumza ukweli vinawanyima Watanzania uwezo wa kujenga mustakabali thabiti wa nchi.

Askofu huyo ameongeza kwa kuwataka Watanzania wote, bila kujali nafasi zao, kuhakikisha wanasimamia misingi ya haki na uadilifu katika maisha ya kila siku, ili kulinda heshima ya taifa na mustakabali wa vizazi vijavyo.

“kwa kadiri tunavyokaa kimya tunazidi kuruhusu vitendo viovu na uvunjifu wa haki utawale kwenye taifa…na tunaporuhusu wahuni na wezi wanaoiba na kutumia madaraka vibaya kuingia katika ngazi zote, uwe na hakika taifa letu linaangamia,” amesema Askofu Laiser.
 
Ila Kuna watu humu wamekosa vyote; akili na busara..........niishie hapo tu.
 
Back
Top Bottom