Askofu Kyando: Awaonya wanaojaribu kuwagawa wakatoliki asema HATUGAWANYIKI

Askofu Kyando: Awaonya wanaojaribu kuwagawa wakatoliki asema HATUGAWANYIKI

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
15,505
Reaction score
27,501
Askofu wa Jimbo Katoliki Njombe, Mhashamu Eusebio Kyando, ameonya kuwa Waumini wa Kanisa Katoliki hawagawanyiki, akieleza kuwa katika siku za karibuni kumejitokeza jitihada za baadhi ya watu wanaolenga kuwagawa waumini hao, akisisitiza kuwa juhudi hizo hazitafua dafu

Askofu Kyando amesema hayo jana Januari 1, 2026 wakati wa adhimisho la Misa Takatifu ya kuukaribisha Mwaka Mpya, akisema Kanisa Katoliki limejengwa juu ya misingi imara ya umoja ambayo haiwezi kuvunjwa wala kugawanyika.

“Sisi hatugawiki. Sisi ni kama namba witiri; huwezi kugawa namba witiri ukapata matokeo sahihi. Kanisa Katoliki si namba shufwa. Namba yetu haigawanyiki kirahisi,” alisema Askofu Kyando akitumia lugha ya mfano kufafanua msimamo wa Kanisa.

Aliongeza kuwa Kanisa Katoliki ni Kanisa Moja, Takatifu, Katoliki na la Kitume, akionya kwamba mtu yeyote anayejihusisha au kutumiwa katika njama za kuwagawa waumini hujiingiza katika matatizo ya kiroho na laana ya bure

Aidha, Askofu Kyando aliwahimiza waumini kuendelea kudumisha umoja na mshikamano, akisisitiza kuwa Mkatoliki wa kweli anayelipenda Kanisa lake hawezi kufikiria kuligawa, bali hufikiria namna ya kulijenga na kuimarisha umoja uliowekwa na Yesu Kristo mwenyewe.

“Hatugawanyiki. Mtu akisema amefanikiwa kuligawa Kanisa Katoliki, ukweli ni kwamba amejitenga mwenyewe na kuasi. Hajagawanya Kanisa, bali ameanzisha mwelekeo wake binafsi. Wanaodhani wanaweza kutugawa wanapoteza muda, kwa sababu Kanisa Katoliki haligawanyiki wala haliwezi kugawanyika,” alisisitiza.
 
Pongezi nyingi kwao maaskofu na TEC kiujumla wamejitahidi kusimama na watanzania katika vipindi vyote vigumu tulivyopitia.
 
Lengo lao kubwa ni kuwatoa watu kwenye reli kwa kuhamisha mjadala (deflection). Wanataka Watanzania watumie muda wao mwingi kujadili viongozi wa dini badala ya kujadili maovu ya Serikali ya CCM.
 
Chawa wamekuwa wakijitahidi kutofautisha TEC na Katibu wao mbaya zaidi kwa tamaa za utawala hadi viongozi wa juu wa inchi hii ambao ni Christian nao wanafanya ujinga huu.
 
Na wao walishawahi kutoa tamko kuhusu hili ?

1767307263060.png
 
Mentality ya kijinga sana kudhani kanisa ni sawa na chama cha siasa kama chadema na act wazalendo unaweza kuwagawanya utakavyo. Lile ni kanisa ni ngumu kuligawa kindezi
 
Back
Top Bottom