Huyo si mtumishi wa Mungu bali pandikizi la ibilisi lililopata cheo kanisaniUnamkana mtumishi kisa CDM!!!
Kwa waislamu nadhani watakikumbuka kisa cha ABUJAHAL kupitia maneno yako aisee.
maaskofu wa kweli hawaropoki ,wanasikia,wanatafakari na kutoa hoja .Kwa vyovyote vile kondoo wamepotezwa hapa.Ni katika ibada ya leo!
Askofu wa KKKT dayosisi ya Iringa Dr. Mdegela alipoamua kuwaambia waumini wake kuhusu kilichotokea bungeni tarehe 06/sept/2013 kama ifuatavyo:
anaanza "... ndugu zangu leo ngoja niwaambie kilichosababisha vurugu za juzi bungeni.... najua humu ndani (kanisani) kuna watu wa upinzani, lakini nawaambia tu kuwa WApINZANI WAMEKOSEA SANA... siku ile nami nilikuwa Dodoma na niliongea na waziri mkuu na baadae yake nikaongea na Mhe. Rais wakaniambia kila kitu! ... wapinzani walidai CCT (jumuiya ya kikristo Tanzania) hatujashirikishwa katika mchakato wa ule muswada; huo ni uongo kabisa! mimi Askofu jina langu limetajwa katika repoti ile pia na wenzangu watatu wakiwemo, sasa CCT haijashirikishwa kivipi!"
anaendelea " ... unajua mule bungeni watu wana sifa tofauti tofauti, kuna washamba na wa mjini, kuna wenye elimu na wajinga... sasa kilichotokea pale ni ujinga mtupu, na nyie wakristo tunawaambia fanyeni uchaguzi wa busara! ... manake sisi hatujawatuma kwenda kugeuza pale kuwa uwanja wa masumbwi...! ... ukiangalia waliofanya vurugu pale ni wale waliotoka shule za kata na walipata sifuri, wao ni kutumia nguvu tu badala ya akili na wanaenda kuwakilisha itikadi zao tu....! sasa nawaambia wakristo tuombee taifa letu na tuombee waliopo madarakani wamalize salama ndipo tuandae mchakato sasa, manake kilichotokea pale ni mchakato tu..." amemaliza kuongea, misa inaendela!
wana JF hayo katika nukuu ni baadhi ya maneno ya Askofu Dr. Mdegela! na katika alama hizo ( ... ) za muendelezo ni sehemu alizoniacha katika kumnukuu!
my take! kwa mimi sijaona Askofu akielezea chanzo cha vurugu husika, na pia amesema ameongea na Waziri mkuu na Mhe. Rais lakini sijaskia akisema ameongea na upande wa pili yaani upinzani ili kukidhi misingi ya kusikiliza pande zote kabla ya hukumu (audi arterum patem =right to be heard)!
karibuni tena mezani wana JF.
Hivi shule za kata zilianza mwaka gani?
sasa nitasali vp wakati msalishaji mwenyewe amegeuza kanisa kama uwanja wa kumwaga oil chafu! kuwaletea habari hapa naamini Mungu atanibariki zaidi, manake silipwi na mtu yeyote!mkuu wewe kwanza mbea sana, kwahiyo, hilo limekuchoma hukusubiri mpaka misa iishe unapost umu JF, tubu kwanza dhambi ya uchochezi maana wewe hukwenda kusali bali kusikiliza vya kupost humu jf.
wewe hujui hata baraka zinatafutwa vipi, ungetumia huo muda vizuri kumsikiliza mtumishi wa Mungu kuliko kuja kutuletea umbea, ona sasa umepata laana ya aibu..sasa nitasali vp wakati msalishaji mwenyewe amegeuza kanisa kama uwanja wa kumwaga oil chafu! kuwaletea habari hapa naamini Mungu atanibariki zaidi, manake silipwi na mtu yeyote!
mkuu wewe kwanza mbea sana, kwahiyo, hilo limekuchoma hukusubiri mpaka misa iishe unapost umu JF, tubu kwanza dhambi ya uchochezi maana wewe hukwenda kusali bali kusikiliza vya kupost humu jf.