Askofu Kilaini: Ndugai jibu hoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu Kilaini: Ndugai jibu hoja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 6, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,681
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Askofu Kilaini: Ndugai jibu hoja
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 05 January 2012 21:04
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Waandishi Wetu
  Mwananchi

  ASKOFU Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Mhashamu Methodius Kilaini, amemshangaa Naibu Spika Job Ndugai kwa kile alichoeleza kuwa amekwepa kujibu hoja ya msingi ya Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye inayohusu nyongeza ya posho za wabunge, badala yake, ameshambulia kiongozi huyo kama mtu binafsi.

  "Sumaye kama mwanadamu anaweza akawa na upungufu mwingi, lakini alichokisema kuhusu posho tujihoji kina ukweli gani? Hilo ndilo la msingi. Alichotakiwa Ndugai ni kufafanua uhalali wa posho na sio kusema aliyetoa hoja hiyo, hana usafi wa kuhoji."

  Katika kuonesha kukerwa na kauli ya Ndugai, kiongozi huyo wa kiroho alikemea kauli za baadhi ya wanasiasa kutotaka kukosolewa hata pale wanapofanya makosa na kutaka watu waachwe waseme ukweli bila kuzibwa midomo wala kubezwa.

  "Watu waachwe waseme kweli wasibezwe. Kwamba naye (Sumaye) alijiongezea posho, hilo ni jambo lingine ambalo kama anataka (Ndugai), alianzishe mjadala watu wajadili. Lakini sasa tunazungumzia suala la posho za wabunge ambazo sote zinatukera,"alisema Kilaini.

  Kwa mujibu wa Askofu Kilaini, si sahihi mtu kujadili hoja aliyoanzisha mtu kwa kuangalia udhaifu wa mtoa hoja. "Hakuna hoja ya msingi katika kumshambulia mtu anayetoa hoja kwa kutumia udhaifu wake, kwani ukweli utaendelea kuwa ukweli na udhaifu wa mtu ni jambo lingine."

  Askofu Kilaini alisema: "Nataka watu wajue kwamba hakuna mtakatifu hapa, wote tuna udhaifu, lakini kama mwenzetu kasema ukweli tujadili hoja yake kwa moyo mkunjufu na sio kumpuuza kwa sababu tu eti aliyeongea ana upungufu fulani."

  Aliongeza; "Ndugai lazima asome alama za nyakati. Huu sio wakati wa kutetea posho kwani hakuna atakayemwelewa. Watanzania wa matabaka yote wamezipinga sasa yeye akianza kuzitetea atabaki peke yake."

  Wanasheria
  Kauli hiyo ya Askofu Kilaini, iliungwa mkono na baadhi ya wanasheria waliozungumzia hoja hiyo jana ambao kwa nyakati tofauti walisema kitendo cha Ndugai kuponda maoni ya Sumaye, kimeonyesha kuwa si mtu makini.
  Wakili wa kujitegemea, Lupia Augusto alihoji kama Ndungai alikuwepo bungeni wakati sheria ya kupandisha posho za viongozi wastaafu zilizomwezesha Sumaye kujiandalia uzee mwema, kwanini hakupinga. "Iweje aje na hoja hiyo leo?"alihoji.

  Augusto alisema tabia aliyoionyesha Ndugai inatakiwa kutafsiriwa kama hakujua majukumu ya ubunge wake wa kuhoji na badala yake, alijua itamnufaisha.Alifafanua kwamba kitendo alichokifanya Ndugai ni ishara kwamba maoni yake yamekumbatia kujinufaisha na sio kunufaisha wananchi.

  Alisema Ndugai ameanika udhaifu wake kwani hakuna rekodi zinazoonyesha kwamba alipinga hoja ya kupitisha posho ilipoletwa wakati Sumaye alipokuwa Waziri Mkuu.Augusto alisema kuna kila dalili kwamba kuna mambo mengi yanayofanywa kwa siri kwa maslahi ya wachache na kwamba wanapopingana ndipo mambo hayo hujitokeza wazi.

  "Wananchi wajiulize alifanya nini kupinga, maana hapa anaazisha malumbano yasiyokuwa na tija baada ya watu kupinga posho ambazo wabunge wamejipandishia bila kuweka uzalendo mbele,"alisema


  Awakera wananchi
  Baadhi ya wananchi nao wameeleza kukerwa na kauli ya Ndugai dhidi ya Sumaye na kwamba ni mbinu za kuwatisha viongozi wastaafu wasitetee maslai ya Umma.

  Mkazi wa Dar es Salaam, Kimazi Totera alisema Ndugai anatumia Bunge kama sehemu ya kutetea matakwa yake binafsi kwa kuziua kauli za viongozi wastaafu pale wanapotetea maslai ya Umma.

  Fatma Haji alisema Ndugai ana siri kubwa kutokana na kuyajua mazingira ya uongozi ya awamu ya tatu kwa kudai Sumaye alijiwekea sheria ya viongozi wa juu wastaafu kulipwa asilimia 80 ya mshahara.
  "Yeye kama kiongozi alikuwa wapi kupinga sheria ya viongozi hawa kulipwa kiwango hicho cha pesa ina maana naye ana chuki binafsi, tungemwelewa kama angesema mapema,"alisema Fatma.

  Alichosema Sumaye
  Jana alipotakiwa kuzungumzia hoja za Ndugai jana, Sumaye alisema," No comment," nataka kusoma na kuelewa vizuri alichokisema kwa hiyo unitafute kesho (leo)."

  Kilichoamsha hasira za Ndugai ni kauli ya Sumaye alioyoitoa kupitia kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, kwamba ongezeko la posho za wabunge linaweza kuchochea makundi mengine kudai kama Wanajeshi, Polisi, Mahakama na walimu nao kutaka nyongeza, hivyo kumweka Rais katika wakati mgumu kufanya uamuzi.

  "Mwanasiasa mzuri akifanya jambo akiona limewaudhi wananchi anatakiwa aliache, lakini pia kwenye hili huu mkanganyiko wa Spika na Katibu wake na huu ukimya wa Ikulu ni tatizo, tungependa waseme ili umma ujue hali ikoje,"
  alisema Sumaye.

  Alisema hatua ya Bunge kujipandishia posho ya kikao kutoka 70,000 hadi 200,000 kwa siku haliingii akilini na kwamba, inakiuka utaratibu uliowekwa na serikali katika kulipa gharama kwa maofisa wake ikiwa ni pamoja na gharama hizo za fedha za kujikimu.

  "Siyo kwamba napinga posho, wabunge wanastahili posho, lakini kwa kweli kujiongezea kutoka 70,000 hadi 200,000 siyo sahihi," alisema Sumaye.

  Alisema wakati yeye alipoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kwa awamu ya pili kushika wadhifa wa Waziri Mkuu, aligoma kwa sababu alikuwa amekwaruzana na wabunge kuhusu nyongeza ya posho.

  "Nilimwambia wabunge watanikataa kwa sababu nimegombana nao sana juu ya suala la posho lakini akasema lazima uwe na mimi ndipo nikakubali, lazima hili suala liangaliwe mara mbilimbili…, leo wabunge mmejiongezea kesho jeshi, polisi na walimu nao watataka, tutafanyaje tusifanye mambo ambayo yatamuweka Rais pabaya," alisema Sumaye.

  Alisema posho ni jambo ambalo kwa sasa limekuwa tatizo kwa serikali na kwamba imefika wakati ofisi za serikali zimehamia hotelini, lengo likiwa ni watumishi wa umma kutafuta mwanya wa kulipana posho.

  "Ndiyo maana watu wa TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) wanakusanya fedha nyingi lakini ni fedha kidogo sana zinakwenda kwenye huduma za jamii, nadhani hili ni tatizo na ni utawala mbaya kabisa, lazima kuwepo mabadiliko kama kweli tunataka kuisafisha nchi yetu," alisema Sumaye

  Habari hii imeandaliwa na Daniel Rutoryo, Keneth Goliama, Freddy Azzah

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. C

  Chintu JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 3,403
  Likes Received: 857
  Trophy Points: 280
  Ndugai na mwenzake dr Bana nadhani genetically ni ndugu. Maana uwezo wao wa kuchambua hoja unafanana kweli!
   
 3. R

  Rutatinisibwa Senior Member

  #3
  Jan 6, 2012
  Joined: Aug 22, 2011
  Messages: 105
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mhashamu Askofu waitu shumalamu! kasinge akagambo kae karungi muno!
   
 4. C

  Chintu JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 3,403
  Likes Received: 857
  Trophy Points: 280
  Accidents zingine bwana. mpaka wakati mwingine najiuliza hivi tumemkosea nini Mungu?
  Spika - Bi kiroboto
  Naibu - Ndugai
  Halafu pale juu Mzee wa maswahiba.
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Mhashamu Methodius Kilaini

  ASKOFU Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba,
  Mhashamu Methodius Kilaini,

  amemshangaa Naibu Spika Job Ndugai kwa kile alichoeleza kuwa amekwepa kujibu hoja ya msingi ya Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye inayohusu nyongeza ya posho za wabunge, badala yake, ameshambulia kiongozi huyo kama mtu binafsi.

  "Sumaye kama mwanadamu anaweza akawa na upungufu mwingi, lakini alichokisema kuhusu posho tujihoji kina ukweli gani? Hilo ndilo la msingi. Alichotakiwa Ndugai ni kufafanua uhalali wa posho na sio kusema aliyetoa hoja hiyo, hana usafi wa kuhoji." Katika kuonesha kukerwa na kauli ya Ndugai, kiongozi huyo wa kiroho alikemea kauli za baadhi ya wanasiasa kutotaka kukosolewa hata pale wanapofanya makosa na kutaka watu waachwe waseme ukweli bila kuzibwa midomo wala kubezwa. " Watu waachwe waseme kweli wasibezwe. Kwamba naye (Sumaye) alijiongezea posho, hilo ni jambo lingine ambalo kama anataka (Ndugai), alianzishe mjadala watu wajadili. Lakini sasa tunazungumzia suala la posho za wabunge ambazo sote zinatukera,"alisema Kilaini.

  Kwa mujibu wa Askofu Kilaini, si sahihi mtu kujadili hoja aliyoanzisha mtu kwa kuangalia udhaifu wa mtoa hoja. "Hakuna hoja ya msingi katika kumshambulia mtu anayetoa hoja kwa kutumia udhaifu wake, kwani ukweli utaendelea kuwa ukweli na udhaifu wa mtu ni jambo lingine." Askofu Kilaini alisema: "Nataka watu wajue kwamba hakuna mtakatifu hapa, wote tuna udhaifu, lakini kama mwenzetu kasema ukweli tujadili hoja yake kwa moyo mkunjufu na sio kumpuuza kwa sababu tu eti aliyeongea ana upungufu fulani."

  Aliongeza; "Ndugai lazima asome alama za nyakati. Huu sio wakati wa kutetea posho kwani hakuna atakayemwelewa. Watanzania wa matabaka yote wamezipinga sasa yeye akianza kuzitetea atabaki peke yake."


  Wanasheria

  Kauli hiyo ya Askofu Kilaini, iliungwa mkono na baadhi ya wanasheria waliozungumzia hoja hiyo jana ambao kwa nyakati tofauti walisema kitendo cha Ndugai kuponda maoni ya Sumaye, kimeonyesha kuwa si mtu makini. Wakili wa kujitegemea, Lupia Augusto alihoji kama Ndungai alikuwepo bungeni wakati sheria ya kupandisha posho za viongozi wastaafu zilizomwezesha Sumaye kujiandalia uzee mwema, kwanini hakupinga. "Iweje aje na hoja hiyo leo?"alihoji.

  Augusto alisema tabia aliyoionyesha Ndugai inatakiwa kutafsiriwa kama hakujua majukumu ya ubunge wake wa kuhoji na badala yake, alijua itamnufaisha.Alifafanua kwamba kitendo alichokifanya Ndugai ni ishara kwamba maoni yake yamekumbatia kujinufaisha na sio kunufaisha wananchi. Alisema Ndugai ameanika udhaifu wake kwani hakuna rekodi zinazoonyesha kwamba alipinga hoja ya kupitisha posho ilipoletwa wakati Sumaye alipokuwa Waziri Mkuu.Augusto alisema kuna kila dalili kwamba kuna mambo mengi yanayofanywa kwa siri kwa maslahi ya wachache na kwamba wanapopingana ndipo mambo hayo hujitokeza wazi.

  “Wananchi wajiulize alifanya nini kupinga, maana hapa anaazisha malumbano yasiyokuwa na tija baada ya watu kupinga posho ambazo wabunge wamejipandishia bila kuweka uzalendo mbele,”alisema


  Awakera wananchi

  Baadhi ya wananchi nao wameeleza kukerwa na kauli ya Ndugai dhidi ya Sumaye na kwamba ni mbinu za kuwatisha viongozi wastaafu wasitetee maslai ya Umma. Mkazi wa Dar es Salaam, Kimazi Totera alisema Ndugai anatumia Bunge kama sehemu ya kutetea matakwa yake binafsi kwa kuziua kauli za viongozi wastaafu pale wanapotetea maslai ya Umma.

  Fatma Haji alisema Ndugai ana siri kubwa kutokana na kuyajua mazingira ya uongozi ya awamu ya tatu kwa kudai Sumaye alijiwekea sheria ya viongozi wa juu wastaafu kulipwa asilimia 80 ya mshahara. “Yeye kama kiongozi alikuwa wapi kupinga sheria ya viongozi hawa kulipwa kiwango hicho cha pesa ina maan
  a naye ana chuki binafsi, tungemwelewa kama angesema mapema,”alisema Fatma.

   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Tangu lini Ndugai kaweza kujibu hoja mtasubiri mpaka mtachoka huyu naibu Spika ni aina ya wanasiasa wanaotakiwa kuondolewa haraka katika safu za uongozi wa nchi yute ikiwa tutafanikiwa kutunga katiba nzuri.
   
 7. kombati

  kombati Member

  #7
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ndugai???..ajibu hoja gani ili hali ni mmoja ya wanafiki wanaotambua nini kinachoendelea huko jikoni kila siku tunaletewa chakula kibichiii
   
 8. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kanisa limekuwa mstari wa mbele sana ngoja tuone mwisho wake si bure...
   
 9. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  ndugai alijishusha hadhi kwa alichozungumza,angekiongea Malaria Sugu ningemwelewa
   
 10. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Inaniwia vigumu sana kumtofautisha Ndungai, na Jenister Mhagama, na Sophia Simba kiupeo wa kufikiri, wote huwa ni wakurupukaji na wapenda mipasho. Shame on them.
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Unamkumbuka Askofu Desmon Tutu wa Afrika Kusini alivyosaidia kusambaratisha siasa za ubaguzi, akina Martin Lutter King ni katika mkondo wa dini aliweza kutetea unyanyaswaji wa waafrika nchini Marekani, na wengine wengi tu, utetezi wa hoja yako umesimamia wapi ndugu?
   
 12. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Halafu bosi wake ndio matoto ya njiwa!!!Loooooo!
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Badala ya kujibu hoja yeye anaanza kumshambulia mtu binafsi hapo ndipo udhaifu wa viongozi wetu wengi walivyo.
   
 14. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Maaskofu wanaowashambulia viongozi wanaochemsha ndani ya Serikali nadhani wako sahihi! ila sikubaliani nao pale wanaposhabikia na kutetea kauli za baadhi ya viongozi wa chama kimoja cha upinzani wakati nchi hii ni kuna vyama vingi vya kisiasa! hapa Maaskofu wanaonyesha unafiki kwa kushabikia Chadema tu!!

  Tumeshuhudia kila anapoongea kiongozi wa Chadema kumlaumu Kiongozi Serikalini na kujibiwa basi anaefuata kutetea kauli za kiongozi huyo wa CDM anakuwa ni Askofu!!!

  Sasa nauliza Maaskofu wao wameamua kushabikia na kutetea Chadema? jee, Mashehe na Maimamu nao wakiamua kuwa upande wa NCCR au TLP itakuwa ni kosa!

  Ushauri wangu wa bure kwa Mababa Askofu nawaomba wabaki Makanisani kuchunga Kondoo wao kwani siasa imewashinda kwa kuamua kuwa wasemaji na watetezi wa Chadema!!!
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ni kawaida walioshika hatamu za kuongoza nchi ndio tunaowaona, na hawa wa vyama vingine watakapopata nafasi ya kushika hatamu za kuongoza nchi watafanyiwa viyo hivyo.

  Utawalaumu vyama vingine vya siasa visivyoshika serikali kwa lipi wakati majukumu na utendaji umeshikwa na chama tawala? Tungekuwa na serikali ya mseto kama Zenj ningekuelewa.
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
   
 17. bona

  bona JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  i am always against viongozi wa dini kujiingiza kwenye siasa hata kama anachokizungumza kina ukweli ndani yake!
   
 18. Titans

  Titans JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 867
  Likes Received: 1,073
  Trophy Points: 180
  Sijakuelewa kidogo..kwa hiyo Askofu kilaini amemtetea Sumaye ambaye yupo chadema??au Sumaye ambaye yupo CCM..mi naona kama umekurupuka vile ku analyse..mana aliye comment kuhusu posho ni Sumaye mwana CCM damu damu...biased.
   
 19. m

  matawi JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  usizunguke sema tu mawazo yake hayatokei ubongoni yanatokea masaburini yake
   
 20. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #20
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280

  Mkuu nilifikiri na wewe unaunga mkono huu wizi wa mchana unajulikana kwa kutetea magamba'askofu ana hoja ya msingi'tusiangalie udhaifu wa mtoa hoja bali tuipime hoja yake'naunga mkono
   
Loading...