Askofu Kilaini achemsha kwa ushauri huu!

kilio changu pia ni kwa wananchi wetu ambao wanadhani kutofanya kazi na kwenda ktk makanisa basi maisha yatanyoka. Jamani tuwaelimishe kwa sababu wanadanganywa sana na akina kakobe.
Simulations nyingi zinawarubuni watu na kudhani kila kinachohubiriwa na hawa watu ni kweli.
 
Kwangu mimi huu ni Ushauri wa hovyo na wa hatari kwa nchi iliyojiwekea misingi ya uhuru wa kuabudu kwenye katiba yake. Yaani watz 200 wakitaka kuabudu wasihalalishwe kuabudu! Idadi gani ni halali?

Jamani hata kama mwanzishaji wa kikanisa ni aina ya kibwetere basi serikli iache tu...hapana. Vikanisa vingi ni feki na inasemekana baadhi ya waanzilishi ni majambazi wa kutumia silaha au wana wahifadhi majambazi.
 
Serikali inatumia vigezo gani kutambua makanisa? Mtu au watu wakitaka kuanzisha kanisa na kwenda kujisajili serikalini wana takiwa kutimiza vigezo gani? Katika katiba ya nchi Kanisa hasa ni nini kutokana na definition ya katiba?

Mimi nadhani kama serikali imeweka utaratibu mzuri au katiba inaorodhesha vizuri nini kigezo cha kuhesabika na kutambulika kama kanisa basi sidhani kama mtu yoyte au kikundi chochote tu kinaweza kuanzisha kanisa. Tatizo bongo usanii tupu na sito shangaa kusikia kuna viongozi serikalini wana hisa katika hayo "makanisa".
 
Wako watu wanadanganya wao ni Kanisa na kwa hivyo wasamehewe kodi. Hao serikali isiwape msamaha wa kodi.

There are con men who couldn't care less about God, but want tax exemption. So, they start a "Church" for the specific purpose of cheating on taxes. Sasa Kama Baba Askofu anataka wathibitiwe kuna mbaya gani?[/QUOTE]

Nadhani hakuna ushauri wa hovyo. Kuna mambo mengine ambayo yanatumia akili ya kuzaliwa tu na sio lazima uwe na madigrii. Kuna mambo ya wzi, ni kweli makanisa yanaanzishwa mengi sana sasa hivi. lazima tuangalie ni yapi yana lengo la kuabudu kweli. Kuna kanisa Ubungo juu ya TANESCO, anawaambia waumini wake kuwa " ilibakia kidogo amfufue kidogo amina chifupa" lakini akaponyoka, ila sio muda mrefu atamfufua. Sawa uhuru wa kuamini, kuabudu, jamani na hili tulikubali!!!!! TUSICHUKUE TAHADHALI YA AKINA KIBWETERE KWA KUWA KUNA UHURU WA KUABUDU!!!!!
 
na mbona maandiko yanasema mpeni kaisari yaliyoyake kaisari au andiko hili limekwishafutwa na hapo makanisa yanatufundisha nini kwasababu kodi ni kwa maendeleo ya nchi na nchi ndiye kaisari mwenyewe
 
Kusema kweli ni jambo gumu sana kujua kanisa hasa ni lipi na lipi si kanisa halali. Wajibu wa serikali si kuweka vigezo vya kujua lipi kanisa si halali na lipi ni halali. Itakuwa rahisi sana serikali kutumbukia katika kuingilia haki na uhuru wa kuabudu. Makanisa mapya yataendelea kuzaliwa kila siku na ni kweli vile vile kuwa wapo watu wanaoyatumia makanisa na watakaoendelea kuyatumia makanisa kwa shughuli au mambo binafsi.

Kwenye suala la misamaha ya kodi serikali inachoweza kufanya ni kubainisha aina ya shughuli zinazoweza kuangukia kwenye msamaha wa kodi. Shughuli hizo iwe ni za utoaji wa huduma za jamii au kuabudu ni lazima ziwe zinakuwa closely monitored na responsible agencies kama TRA. Hata hivyo kazi yenyewe ya kuzi-monitor shughuli hizo zinazoombewa misamaha inaweza ikawa ngumu na ya gharama kubwa kwa sababu level ya utapeli na uongo katika nchi yetu iko juu sana. Ndiyo maana nimekuwwa na msimamo kuwa tukiwatoza wote kodi kwa kila kitu, hakutakuwa na tatizo lolote.

Utapeli na uongo ni mojawapo ya mambo yanayofanya cost of doing business in Africa na hasa Tanzania iwe juu sana. Na hili ni jambo ambalo lazima tupambane nalo. Ukitoa misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini, ukweli halisi wa nchi zetu ni kuwa kila mtu atajaribu kutumia window hiyo kwa kutumia hila na mbinu mbali mbali. Matokeo yake ni kudorora kwa mapato ya serikali inayosababisha serikali izidishe kodi katika maeneo ambayo ni rahisi kuzikusanya kama kwenye viwanda na kadhalika. Vile vile ukwepaji wa kodi kwa njia hii inasababisha kuwe na unfair business environment inayofanya wale wanaofanya biashara halali kushindwa kuendelea na kupata hasara.

Kutokana na ugumu wa serikali kuamua ni taasisi ipi itambuliwe kama kanisa na ni ipi isitambuliwe kama kanisa, bado kutakuwa na ugumu mkubwa sana katika kutawala na kudhibiti hii misamaha ya kodi. Tunachoweza kuangalia ni level ya misamaha hii tu. Je imefikia kiwango cha kuathiri mapato ya serikali? Ni asilimia ngapi ya mapato yetu yanaangukia kwenye misamaha hii? Kwa hali ilivyo sasa inaonekana hali inaanza kuwa mbaya. Lakini eneo linaloongoza kwa misamaha si kwenye taasisi za dini, ni katika migodi. Kwa hiyo misamaha inayotuathiri zaidi kimapato ni ile ya migodi na bahati mbaya sana hii imefungwa kwenye mikataba ambayo iko juu ya katiba yetu na sheria zetu zote.

Kwa hiyo suala kubwa hapa si kuangalia taasisi za dini na kuanza kuchambua ipi ni kanisa na ipi si kanisa. Tatizo pana zaidi ni concept nzima ya kutoa misamaha ya kodi kama incentive. Hivi hakuna aina nyingine ya incentive tunazoweza kutoa mbali na misamaha ya kodi? Mimi nadhani kwa mfano kwenye madini, tukifuta kabisa hii kitu kinaitwa mrabaha (tuwaachie wachukue kila kitu) ila tuhakikishe kodi zote wanalipa, bado ni incentive ya kutosha na watalipa zaidi kuliko wanavyolipa kwenye hiyo mirabaha.

Hizi taasisi za kidini, hata zinazotoa social services, kwan nini wasiangalie kodi kama sehemu ya gharama halali? Hao donors wanaotoa misaada ambao hawataki misaada yao iingie katika mapato ya serikali si donors halali. Ikiwa hivyo vitu vinavyoagizwa ni kwa kutumia hela ya michango ya waumini wa makanisa au dini hizo kwa nini wasijue kutokea mwanzoni kuwa kodi ni gharama halali? Tumeshajenga utamaduni wa kodi kuonekana kuwa ni kitu kisichokubalika, na hili ni tatizo!

Au tuseme tatizo pana zaidi ni jinsi ya kushughulikia huu utapeli na uongo ambao umekuwa ndio "characteristic" ya society yetu? Law enforcement iko madhubuti kiasi gani? Hivi hata hizi sheria zilizopo zinafuatwa?

Yaani kadri unavyozidi kuzama ndiyo unavyozidi kuona mtandao wa matatizo yanayoingiliana na hii ndiyo changamoto kubwa. Hata tukiweka sheria ya kuwa so and so isisajiriwe kama kanisa, bado kuna uwezekano mkubwa wa makanisa ya kukwepea kodi kusajiriwa kwa mlango wa nyuma.

Kwa hiyo suluhisho ya tatizo lote ni kuweka kodi ya viwango vinavyokubalika. Lakini kusiwe na sababu ya so and so kupewa msamaha wa kodi. Wote tulipe kodi! Mbunge, rais, askofu, mchungaji, n.k.
 
Mi ninafikiri kwanza kuwa kijikanisa leo inaweza kukufanya miaka 50 ijayo uwe kanisa kubwa. Kama tungetumia jugdement anayotaka Kilaini na Gamanywa itumike miaka 100 iliyopita basi labda madhehebu makubwa kama RC, LUTHERAN nk yasingekuwepo leo. Je uhalali wao ni kwa vile wao walianza zamani au tuweke vigezo vya kupima mwelekeo wa kiimani na baraka yake kwa waabudu? Kama Martin Luther na Reformers wengine wangepimwa wakati wa vuguvugu la mabadiliko na kukosoa yaliyokuwa yamepinda yangeachwa mikononi mwa mapapa wa kikatoliki wangesemaje juu ya Reformers hawa? Bila shaka wangesema wauawe mara moja bila shaka. Je tunataka kurudi huko?
Pili ningependa kuuliza, kuna uhusiano gani kati ya kusajili kanisa na msamaha wa kodi. Maana si kila kanisa lililosajiliwa linapata msamaha wa kodi automatically. Kama kuna sababu yoyote ya kupata msamaha kwa ajili ya huduma unayoitoa kwa kawaida unaomba msamha for that particular issue. Hakuna kibali general cha msamaha wa kodi ambacho mtu anatembea nacho. Ili kupata msamaha lazima ueleze unachotaka kufanya au kununua au kuingiza nchini. Lazima useme huo mradi au shughuli unaifanyia wapi. Lazima mkuu wa wilaya husika athibitishe kuwa ni kweli uko katika wilaya yake na unayfanya unayodai kuyafanya. Wakati mwingine TRA watetembelea site ya shughuli hiyo na kuandika recommendation kabla ya kamishna kutoa huo msamaha. Sasa swala la usajili wa kanisa hapo linaingiaje?
 
Sasa hivi nilikuwa nikipitia website ya cbn news nikakuta rais wa Iran anapata shida sana ya si na makanisa established ya zamani lakini kutoka kwa home churches ambayo ni movement mpya.

TEHRAN, Iran -- Speculation is growing that the Iranian government may soon resort to violence to bring an end to pro-democracy protests. At the same time, the Islamic regime is finding it's incapable of reversing the rapid spread of Christianity there.

CBN News Chief International Correspondent Gary Lane visited the country last year to get an exclusive look at the Iranian church. ........

But 30 years on, the revolution is faltering and many Iranians are disillusioned. They've taken to the streets to protest a stolen election and government corruption...........
But it's not established churches that the Iranian government fears most, but the rapid growth of unregistered churches.
President Mahmoud Ahmadinejad is so concerned that he has made it his aim to stop the house church movement, declaring: "I will stop Christianity in this country.”

Tunajua watu wengi wako fed up na mambo ya wakristo kwa vile kumekuwa na mifano mingi mibaya ya watu wanaojiita wakristo lakini maisha yao hayana nuru. Unafiki, uongo, magomvi, ufisadi vinatokea humo humo makanisani. Mafisadi wanabarikiwa kwa kutoa sadaka nzuri tena wengine walisomea shule hizo hizo za kanisa lakini hawakubalika. Tabia chafu, maadili duni na heshima kubwa mbele ya wanadamu. Mi nadhani tunahitaji tena chachu mpya katika kambi ya wakristo. Na usifikiri old guards popes and bishops will take it on a silver plate. Mi nadhani ziwepo sheria ziwabane wote mkongwe na mchanga. RC akia buse asulubiwe, Kakobe aki abuse asulubiwe Anglican aki abuse asulubiwe Bakwata waki abuse wasulubiwe. Acheni kuonea wadogo. Katika mifumo mingine ya demokrasi wachache wadogo ndio wanapewa special rights maana ni rahisi kuwaonea. Wapya na wageni wana miradi gani mikubwa ya kusababisha hasara ya kodi kwa serkali. Watu walio na credibility ya kudai misamaha ya mabilion ni wale established ambao wamekuweepo tangu zamani.
 
Ni wazi anachosema ni hiki: Wako watu wanadanganya wao ni Kanisa, na kwa hivyo wasamehewe kodi. Hao serikali isiwape msamaha wa kodi.

There are con men who couldn't care less about God, but want tax exemption. So, they start a "Church" for the specific purpose of cheating on taxes. Sasa Kama Baba Askofu anataka wathibitiwe kuna mbaya gani?

Mpendwa kipimo kipi kitatumiwa na serikali kujua hili kweli kanisa na lipi si kanisa? Je idadi ya watu ndo calibration ya hiyo meter itakayopima hayo makanisa? Nadhani hayo yatakuwa si makanisa kwa maana ya kanisa bali NGOs, CBOs, or any other organizations. Jaribu kukubali ukweli bila kuweka hisia. Huoni kuwa Askofu Kilaini na Gamanywa hapo anatetea uhai wa Kanisa lake kwani serikali kutoa democracy ya kuamini chochote inawapa freedom wakatoliki na wapentekoste kuhama ukatoliki au upentekoste kwenda kwingine? Ndo maana siamini katika dini kabisa maana binadamu wachache wana monopolise dini kwa faida binafsi na kuacha agenda ya Mungu nje yaani Imani. Kama kweli Kilaini anaamini katika roho mtakatifu yeye anashida gani? maana Yesu alisema hataliacha kanisa mpaka ukamilifu wa dahari meaning anauwezo wakulilinda lisifutike sasa hilo lake mbona anataka kulilinda kwa nguvu ya kidunia badala ya kimungu? Kama Mungu yupo pamoja nae nani atakua kinyume nae? Na kama issue ni kodi kwani hata kanisa likiwa na watu milioni thelathini matapeli je hawata kwepa kulipa kodi? Je hata kama hao milioni thelathini ni waaminifu Askofu wao akawa tapeli je hilo kanisa halitakwepa kulipa kodi?

Kama mkristo na utata na hiyo kauli kama inatakia mema wakristo na aliye kinyume chetu ni adui yetu; kama imani yangu inavyonituma basi aelewe kuwa kuutumia ukristo kupinga ukristo ni kupinga nguvu za kristo mwenyewe na kwasababu hiyo sina wasiwasi roho mtakatifu atawashughulikia kwa haki kabisa na kama nia yao ni kupinga injili yakristo basi itadhihirika muda si mrefu. maana injili ni habari njema kwa watu wote tena inanguvu hata kuleta uwokovu kwa yeyote aaminie kwa Myunani kwanza na kwa mataifa mengine pia. Hii inamaana ya kuwa yeyote mwenye habari njema ya upendo wa Mungu wa kweli haijalishi unajina gani Juma, Rajul, Tsetung, Masanja, etc huo ujumbe wako uta prevail no matter what maana unapeleka upendo wa Mungu kwa wasioujua huo upendo bila kujali umesoma, hujasoma, mfupi, mweusi, mweupe mnene, mwembamba, unaheshimiwa, unadharauliwa etc. Na habari njema ni hii kuwasaidia maskini, kuwatetea wanyonge, kuwafungua waliofungwa na nguvu za giza kama ufisadi, uchawi, uzinzi, ulevi etc, kuwapa matumaini waliokata tamaa na kutangaza nguvu za Mungu jinsi zinavyoweza kuondoa yote hayo. Ila kuna ziada katika kufanya hilo uwe na ile nguvu ndani yako yaani ukisema umaskini kesho utakwisha Tanzania na iwe kama utakavyosema bila hivyo wewe ni mwongo na unambeba shetani ndani yako kwakujua au kutokujua na kazi ya huyo ni kuiba, kuharibu na kuua.

So kanisa la leo la kristo kama ninavyoamini mimi wewe linaanzia kwa mtu binafsi meaning number sahihi ya kanisa ni mtu mmoja, akitokea mwenye mawazo kama yako anakuwa wapili and so on ili mpeleke hiyo habari njema hapo juu mkipata msamaha wa kodi Mungu ashukuriwe msipopata hewala, mmepewa sadaka asante Yesu mmenyimwa Mungu abarikiwe yaani mtumwa asie na faida ukiona mnaanza kugombana kwaajili ya kodi na sadaka na namba za watu mjue hapo wala hakuna injili kuna njaa tu na nibora mkafanye kazi mpate uhalali wakula vyakwenu kwakujinafasi.
 
Last edited:
Mi ninafikiri kwanza kuwa kijikanisa leo inaweza kukufanya miaka 50 ijayo uwe kanisa kubwa. Kama tungetumia jugdement anayotaka Kilaini na Gamanywa itumike miaka 100 iliyopita basi labda madhehebu makubwa kama RC, LUTHERAN nk yasingekuwepo leo. Je uhalali wao ni kwa vile wao walianza zamani au tuweke vigezo vya kupima mwelekeo wa kiimani na baraka yake kwa waabudu? Kama Martin Luther na Reformers wengine wangepimwa wakati wa vuguvugu la mabadiliko na kukosoa yaliyokuwa yamepinda yangeachwa mikononi mwa mapapa wa kikatoliki wangesemaje juu ya Reformers hawa? Bila shaka wangesema wauawe mara moja bila shaka. Je tunataka kurudi huko?
Pili ningependa kuuliza, kuna uhusiano gani kati ya kusajili kanisa na msamaha wa kodi. Maana si kila kanisa lililosajiliwa linapata msamaha wa kodi automatically. Kama kuna sababu yoyote ya kupata msamaha kwa ajili ya huduma unayoitoa kwa kawaida unaomba msamha for that particular issue. Hakuna kibali general cha msamaha wa kodi ambacho mtu anatembea nacho. Ili kupata msamaha lazima ueleze unachotaka kufanya au kununua au kuingiza nchini. Lazima useme huo mradi au shughuli unaifanyia wapi. Lazima mkuu wa wilaya husika athibitishe kuwa ni kweli uko katika wilaya yake na unayfanya unayodai kuyafanya. Wakati mwingine TRA watetembelea site ya shughuli hiyo na kuandika recommendation kabla ya kamishna kutoa huo msamaha. Sasa swala la usajili wa kanisa hapo linaingiaje?

Kusajili kanisa na misamaha ya kodi kuna uhusiano kwa sababu makanisa ni beneficiary wa misamaha ya kodi. Vile vile huo utaratibu unaouzungumzia upo lakini imethibitika kuwa utaratibu huo kuna watu wanaukiuka ndo maana Mkulo akafikiria kuifuta hii misamaha. Watu wanamwambia kwa nini asiwakamate hao wanaoutumia vibaya utaratibu huo au wasizuiwe kufaidika? Tatizo ni gharama za kuziba mashimo ambayo unajua kila ukipita leo mwenzio anapita kesho kuchimba mashimo.

Suluhisho si kuendelea kuziba mashimo; ni ama upambane na anayeyachimba au utengeneze kiasi kwamba hawezi kuchimba! Naamini kuzuia kabisa matumizi yasiyo halali ya misamaha hii, ni kuiondoa kabisa isiwepo. Full stop. Misamaha ikiendelea kuwepo, kila mtu atajiuliza afanyeje ili kunufaika na misamaha hiyo? Ndo issue ya usajili wa makanisa inapokuwa issue.

Pendekezo la wengi ni kujaribu kuziba mianya inayotumiwa na watu kunufaika na misamaha ya kodi isivyo halali. Lakini uzoefu wetu kama nchi unaonesha kuwa kitu hicho ni kigumu mno. Kila unapoweka taratibu, wenzio wanafikiria jinsi ya kuzivunja.

Njia bora kabisa ni kusema kila mtu na alipe kodi!! Kila mtu na ajue kodi ipo na itabidi ilipwe. Kama anatoa msaada na huo msaada hawezi kuutoa ikiwa atalazimika kulipa kodi, na aache!! Hilo itakuwa rahisi kulisimamia kwani kutolipa kodi kwa aina yoyote itakuwa ni kuvunja sheria. Kodi itaheshimiwa na kila mtu.

Kuwepo kwa utaratibu ambao baadhi ya watu au taasisi zinazoonekana kuwa ni safi kustahili kulipa kodi, ndo kunafanya tutunge sheria zinazowaondoa viongozi kwenye wigo wa kodi. Maana yake kodi inaonekana ni kitu wanachostahili kulipa watu wachafu tu. Watu wakubwa kama wabunge na marais, malipo wanayopewa mengi yasikatiwe kodi.

Tulipe kodi wote na tulipe!
 
Biashara nyingi sana mjini zinaendeshwa kama taasisi za dini na wakati hakuna dini iliyopo.

Ila hili sio tatizo la haya makanisa ni tatizo la TRA, ni wajibu wao kitengo hiki kujua kinamsamehe nani kodi kwa ajili ya nini. Na wakigundua kwamba msamaha husika haukutumika kama ulivyoombwa wangetoa adhabu zinazostahili hili tatizo lingepungua au kwisha. Sasa hii ya kukurupuka na kutaka kufweka wote halafu wameshindwa serikali inaleta kinyaa.

Ila hakuna haja ya kuwapangia wananchi kuanzisha dini yao wakifuata sheria za nchi hata kama wako sita, kama sheria zinaruhusu ni haki yao.
 
Tatizo ni moja. Kufukuzana na wakwepa kodi kwa kutumia mianya iliyopo ni ngumu sana na ni gharama ku-enforce. Hilo tunaonekana kutolizingatia. Hatuwezi kufanikiwa asilimia mia moja hata tukisema kodi ni compulsory. Lakini tunapunguza uwezekano wa watu kuibua visingizio hivi na vile. Tena inakuwa rahisi na cost effective kunapokuwa na sheria rahisi ya kodi.

Unapoanza kuweka taratibu hizi na zile za kuwaepusha baadhi ya watakatifu na balaa la kodi hapo ndo unapoanza kuharibu. Kwanza tatizo litaanzia hapo hapo, tafsiri halisi ya nani anastahili kupewa misamaha hiyo na kwa shughuli gani. Haya yote yanafanya zoezi zima la utozaji wa kodi kuwa complicated na la gharama pia.

Ndo maana naona wote tuguswe na mkono wa kodi. Hao ng'ombe wasiochinjika ndo tatizo.
 
Mpendwa kipimo kipi kitatumiwa na serikali kujua hili kweli kanisa na lipi si kanisa? Je idadi ya watu ndo calibration ya hiyo meter itakayopima hayo makanisa? Nadhani hayo yatakuwa si makanisa kwa maana ya kanisa bali NGOs, CBOs, or any other organizations. Jaribu kukubali ukweli bila kuweka hisia. Huoni kuwa Askofu Kilaini na Gamanywa hapo anatetea uhai wa Kanisa lake kwani serikali kutoa democracy ya kuamini chochote inawapa freedom wakatoliki na wapentekoste kuhama ukatoliki au upentekoste kwenda kwingine? Ndo maana siamini katika dini kabisa maana binadamu wachache wana monopolise dini kwa faida binafsi na kuacha agenda ya Mungu nje yaani Imani. Kama kweli Kilaini anaamini katika roho mtakatifu yeye anashida gani? maana Yesu alisema hataliacha kanisa mpaka ukamilifu wa dahari meaning anauwezo wakulilinda lisifutike sasa hilo lake mbona anataka kulilinda kwa nguvu ya kidunia badala ya kimungu? Kama Mungu yupo pamoja nae nani atakua kinyume nae? Na kama issue ni kodi kwani hata kanisa likiwa na watu milioni thelathini matapeli je hawata kwepa kulipa kodi? Je hata kama hao milioni thelathini ni waaminifu Askofu wao akawa tapeli je hilo kanisa halitakwepa kulipa kodi?

Kama mkristo na utata na hiyo kauli kama inatakia mema wakristo na aliye kinyume chetu ni adui yetu; kama imani yangu inavyonituma basi aelewe kuwa kuutumia ukristo kupinga ukristo ni kupinga nguvu za kristo mwenyewe na kwasababu hiyo sina wasiwasi roho mtakatifu atawashughulikia kwa haki kabisa na kama nia yao ni kupinga injili yakristo basi itadhihirika muda si mrefu. maana injili ni habari njema kwa watu wote tena inanguvu hata kuleta uwokovu kwa yeyote aaminie kwa Myunani kwanza na kwa mataifa mengine pia. Hii inamaana ya kuwa yeyote mwenye habari njema ya upendo wa Mungu wa kweli haijalishi unajina gani Juma, Rajul, Tsetung, Masanja, etc huo ujumbe wako uta prevail no matter what maana unapeleka upendo wa Mungu kwa wasioujua huo upendo bila kujali umesoma, hujasoma, mfupi, mweusi, mweupe mnene, mwembamba, unaheshimiwa, unadharauliwa etc. Na habari njema ni hii kuwasaidia maskini, kuwatetea wanyonge, kuwafungua waliofungwa na nguvu za giza kama ufisadi, uchawi, uzinzi, ulevi etc, kuwapa matumaini waliokata tamaa na kutangaza nguvu za Mungu jinsi zinavyoweza kuondoa yote hayo. Ila kuna ziada katika kufanya hilo uwe na ile nguvu ndani yako yaani ukisema umaskini kesho utakwisha Tanzania na iwe kama utakavyosema bila hivyo wewe ni mwongo na unambeba shetani ndani yako kwakujua au kutokujua na kazi ya huyo ni kuiba, kuharibu na kuua.

So kanisa la leo la kristo kama ninavyoamini mimi wewe linaanzia kwa mtu binafsi meaning number sahihi ya kanisa ni mtu mmoja, akitokea mwenye mawazo kama yako anakuwa wapili and so on ili mpeleke hiyo habari njema hapo juu mkipata msamaha wa kodi Mungu ashukuriwe msipopata hewala, mmepewa sadaka asante Yesu mmenyimwa Mungu abarikiwe yaani mtumwa asie na faida ukiona mnaanza kugombana kwaajili ya kodi na sadaka na namba za watu mjue hapo wala hakuna injili kuna njaa tu na nibora mkafanye kazi mpate uhalali wakula vyakwenu kwakujinafasi.

Pamoja na kukubaliana na wewe kwa asilimia mia, kwa hayo niliyo ya bold niko na wewe na nakubaliana nawe kwa asilimia 300.:D
 
Kusajili kanisa na misamaha ya kodi kuna uhusiano kwa sababu makanisa ni beneficiary wa misamaha ya kodi. Vile vile huo utaratibu unaouzungumzia upo lakini imethibitika kuwa utaratibu huo kuna watu wanaukiuka ndo maana Mkulo akafikiria kuifuta hii misamaha. Watu wanamwambia kwa nini asiwakamate hao wanaoutumia vibaya utaratibu huo au wasizuiwe kufaidika? Tatizo ni gharama za kuziba mashimo ambayo unajua kila ukipita leo mwenzio anapita kesho kuchimba mashimo.

Suluhisho si kuendelea kuziba mashimo; ni ama upambane na anayeyachimba au utengeneze kiasi kwamba hawezi kuchimba! Naamini kuzuia kabisa matumizi yasiyo halali ya misamaha hii, ni kuiondoa kabisa isiwepo. Full stop. Misamaha ikiendelea kuwepo, kila mtu atajiuliza afanyeje ili kunufaika na misamaha hiyo? Ndo issue ya usajili wa makanisa inapokuwa issue.

Pendekezo la wengi ni kujaribu kuziba mianya inayotumiwa na watu kunufaika na misamaha ya kodi isivyo halali. Lakini uzoefu wetu kama nchi unaonesha kuwa kitu hicho ni kigumu mno. Kila unapoweka taratibu, wenzio wanafikiria jinsi ya kuzivunja.

Njia bora kabisa ni kusema kila mtu na alipe kodi!! Kila mtu na ajue kodi ipo na itabidi ilipwe. Kama anatoa msaada na huo msaada hawezi kuutoa ikiwa atalazimika kulipa kodi, na aache!! Hilo itakuwa rahisi kulisimamia kwani kutolipa kodi kwa aina yoyote itakuwa ni kuvunja sheria. Kodi itaheshimiwa na kila mtu.

Kuwepo kwa utaratibu ambao baadhi ya watu au taasisi zinazoonekana kuwa ni safi kustahili kulipa kodi, ndo kunafanya tutunge sheria zinazowaondoa viongozi kwenye wigo wa kodi. Maana yake kodi inaonekana ni kitu wanachostahili kulipa watu wachafu tu. Watu wakubwa kama wabunge na marais, malipo wanayopewa mengi yasikatiwe kodi.

Tulipe kodi wote na tulipe!

Kipimapembe,
Omulangi yuko sahihi na sijui nini unachopinga hasa kwa mada yake.
Yeye ameweka bayana kwamba kusajili kanisa ni jambo moja.
Na misamaha ya kodi ni jambo lingine.
Na ameeleza wazi kwamba kanisa linaweza kuwa limesajiliwa na lisiombe misamaha ya kodi. Lakini likifanya hivyo ni jukumu la serikali kutoa msamaha wakati imejiridhisha kuwa ni kweli. Na kaeleza na baadhi ya procedures zinazofanyika.
Ukisema kwamba hiyo imeonekana kushindwa mimi sikuelewi maana unaitukana serikali kwa kushindwa kufanya kazi yake. Au niseme serikali hiyo unayosema inakuwa ni nzembe sijui kiasi gani. Maana inakuwa inajua nini kinaendelea na inashindwa kuchukua hatua ili iweje?
Na kwa kweli hayo unayojaribu kuita pendekezo la wengi kuhusu kutotoa msamaha wa kodi si la kweli. Ni pendekezo lenu wachache. Wengi wamelipigia kelele hili na serikali imekubali kukosea, wakabatilisha msimamo wao.
After all watu wote tunalipa kodi in one way or the other. Uwe Kadinari, askofu, Padri, mchungaji n.k. wote hawa wakienda kituo cha mafuta wanalipa kodi. Wakinunua bia wanalipa kodi, wale wavutaji sigara wanalipa kodi, soda wanalipa kodi. Hivyo utagundua ni maeneo machache ambako kanisa halilipi kodi.
Nitakuelewa tu pale utakapo muuliza Mkullo mbona makampuni ya madini hayalipi kodi za mafuta wakati wewe unalipa? na hapo hapo wanakupa 3% ya mauzo yao ya dhahabu na vito? Unashikia bango hivi vikodi na kuacha kushikia bango makodi?!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Tatizo ni moja. Kufukuzana na wakwepa kodi kwa kutumia mianya iliyopo ni ngumu sana na ni gharama ku-enforce. Hilo tunaonekana kutolizingatia. Hatuwezi kufanikiwa asilimia mia moja hata tukisema kodi ni compulsory. Lakini tunapunguza uwezekano wa watu kuibua visingizio hivi na vile. Tena inakuwa rahisi na cost effective kunapokuwa na sheria rahisi ya kodi.

Unapoanza kuweka taratibu hizi na zile za kuwaepusha baadhi ya watakatifu na balaa la kodi hapo ndo unapoanza kuharibu. Kwanza tatizo litaanzia hapo hapo, tafsiri halisi ya nani anastahili kupewa misamaha hiyo na kwa shughuli gani. Haya yote yanafanya zoezi zima la utozaji wa kodi kuwa complicated na la gharama pia.

Ndo maana naona wote tuguswe na mkono wa kodi. Hao ng'ombe wasiochinjika ndo tatizo.

Kipimapembe.
Usitake kutushangaza kwa mawazo yako.
Hivi kufuatilia nani kalipa kodi na nani hakulipa ni kufukuzana na walipa kodi?
Hujui kwamba ni kazi ya TRA kufuatilia na kuhakikisha kuwa kodi zinalipwa na walipa kodi wote na kuwachukulia hatua wasiolipa?
Kwa taarifa yako ni kwamba suala la kodi ni tete sana duniani kote tangu kuumbwa kwa dunia hii. Na hakuna anayependa kulipa.
Lakini pia tunajua hata ukiondoa exemption wakwepa kodi hawatakwisha maana wengi uanzia TRA kwenyewe.
Kama kuna wanaopoteza pesa ya serikali kwa njia ya kodi na TRA wenyewe. Upokea rushwa kwa kiwango kikubwa sana na ku cheat sana viwango ambavyo walipa kodi wanatakiwa kulipa.
Hivyo basi. Ufuatiliaji wa ulipaji kodi ni lazima wala hautakwisha eti kwa sababu umeondoa suala la tax exemption. Unless uniambie serikali imelala.
 
Hayo makanjanja yako mengi na yanaibuka kama uyoga. Eti nabii! Wizi mtupu! Mnataka watu waongee kwa mafumbo hadi lini? Kilaini kasema kweli. Kuna makanisa ya ajabu, toka jan 2 dec ni huyohuyo mimbarini. Nani asojua kuwa makanisa mengi ni ngo za watu? Muwe mnaangalia vya kutetea.
 
Subirini tu hao wafuasi ya hayo makanisa watakapo amua kumfanyia maombi kilaini.
 
Cynic am sorry kusema kuwa umekuwa bias na kuaundermine uhuru wa mtu kutoa maoni,Kilaini ametoa wazo kama mtu mwingine alivyo na uhuru wa kutoa maoni.
Au unaogopa kwa kuwa ni mtu mkubwa kidogo basi serikali itakurupuka kuutekeleza bila kuwa na analysis.
If you belong to the so called churches with 200 WAUMINI WORRY NOT kuwa na amani ya roho na mwili bwana yale ni maoni yake kama mtanzania.
Kumbuka akili ni nywele kila mtu ana zake.
Afterall serikali imesema itajipanga to dig deep into that
 
Back
Top Bottom