KATIBU Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Pentekoste Tanzania (PCT), Askofu Dk. David Mwasota amesema Mungu amemvisha Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete joho la ufahamu na ujasiri kumuwezesha kupambana vita ya kukisafisha chama hicho na Serikali yake.
Askofu huyo alisema hayo baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujivua gamba hivi karibuni. Amesema Rais Kikwete na CCM mpya ndio watakaoibuka washindi katika vita hiyo inayoendelea sasa baina yake na wanachama waliopewa siku 90 kujiondoa katika nafasi zote
za uongozi kutokana na kutajwa kuhusika na vitendo vya ufisadi.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na HABARILEO Jumamosi mjini Dar es Salaam, Askofu Dk. Mwasota alisema Rais Kikwete atashinda vita hiyo kwa vile maaskofu hivi sasa wanakesha kumuombea kwa Mungu ashinde ili kukirejesha chama hicho kikongwe katika mikono ya wanyonge.
"Kama kuna kipindi Rais Kikwete ametufurahisha maaskofu basi ni kipindi hiki. Hatuna sababu ya kupata tafsiri ya nini maana ya kujivua gamba, lakini kitendo alichokifanya hivi karibuni cha kusimamia mabadiliko makubwa ndani ya CCM ili kukiosha chama hicho dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi ni cha kijasiri.
"Kugundua uovu na kupambana nao ni hekima inayotokana na Mungu. Mungu amempa ufahamu na ujasiri wa kuanza kuchukua hatua.
Mwanzo tulikuwa na shaka kama anafahamu mambo yanayoendelea, baadaye tukalaumu kwa kushindwa kuchukua hatua hata pale tume anazounda zinapomweleza hali halisi ilivyo, sasa amechukua hatua nashangaa na nasikitika sana kuona kuna watu wanalaumu na kubeza hatua hiyo tena," alisema.
Askofu Dk. Mwasota alisema maaskofu pia wameridhishwa na ahadi kwamba hatua kama zilizochukuliwa na Rais Kikwete kwenye chama, zitachukuliwa pia kwa viongozi wa serikali wanaotajwa kuhusika na vitendo vya rushwa na ufisadi.
"Sasa Rais wetu amevalishwa na Mungu, joho la ufahamu na ujasiri, ingawa vita ni kali, lakini atashinda. Ni kupitia kwa Rais Kikwete ndio nchi itatakasika kutokana na maombi, na Biblia inasema hivyo kwamba Rais wa nchi ndiye atakayeifanya nchi kutakasika au la, kutokana na kutokumbatia dhambi."
Askofu David Mwasota kwa hili na hii kauli itakubidi utoke nje kwa jamii ya waaminio na kutubu kwao kuwa umewakwaza kwa maneno yako na kuwasababisha wamkosee Mungu kwa manung'uniko. Ndiyo utaendelea kunung'unukiwa na kuipoteza heshima yako.
Je! Tukiwauliza maaskofu wote wa Kipentekoste watakubaliana na kauli yako? Je! Tukiwauliza wachungaji wote (maana nawe ni Mchungaji kihuduma, uaskofu ni cheo tu cha kuchaguliwa) wa Kipentekoste unafikiri ni asilimia ngapi watakuwa upande wako? Kwa washirika sifiki kwasababu itakuwa
AIBU.
Unaposema
"Mungu amemvisha Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete joho la ufahamu na ujasiri kumuwezesha kupambana vita ya kukisafisha chama hicho na Serikali yake." una maana gani na umeweka msingi gani katika hizo kauli zako? Ngoja tuzichambue kidogo kwa jicho la kithiolojia yenye mtazamo wa imani ya kikristo:-
1.
Mungu -> Mungu gani unayemtaja hapa maana inajulikana kuna miungu mingi. Mungu mwenye mapenzi na chama cha siasa , ndiyo mungu mwenye mapenzi na CCM pamoja dhuruma yote waliyoifanya kwa waja wake watanzania.
2.
amemvisha joho la ufahamu na ujasiri-> ili Mungu mwenye enzi, YEHOVA, amviku mtu joho la utukufu kwa kazi yake au kusudi lake mtu muhusika inabidi aweje? Ama atengenezwe vipi? Soma kitabu cha Mithali sura 1-4 halafu utueleze ili mtu apate ufahamu ni jambo gani muhimu kufanyika. Halafu tulinganishe Kikwete analo? Na itakapotokea kuwa matokeo ya maamuzi yaliyochukuliwa yakawa na madhara makubwa kuliko ilivyosasa utakubali kusema alivikwa roho/joho ya upumbavu na woga? Napata shida sana na kauli hizi.
3.
kupambana vita vya kukisafaisha CCM na serikali ...ingawa vita ni kali, lakini atashinda->
Hivi CCM ikisafishwa YEHOVA atakuwa ametukuzwa ama watu wakisafishwa mioyo yao ndipo atakapokuwa ametukuzwa? Je! CCM ni takatifu kwa BWANA Mungu?
Hivi Kikwete anapamabana vita ya haki ama anakazana kuona
hila (conspiracy) inatimia? Ninyi maaskofu mmewauliza waumini wenu ili mkajue kuwa hii ni vita ya haki ama mna hila? Vema, labda pengine umekataa kuiita hila ni hila.."Do not call conspiracy everything this people calls a conspiracy;" Isaiah 8:12a. Tukilipa muda suala hili, na ikatokea akashindwa kukisafisha chama na serikali yake yake mtasema nini? Maana umekwisha hitimisha atashinda.
4.
Rais Kikwete atashinda vita hiyo kwa vile maaskofu hivi sasa wanakesha kumuombea kwa Mungu ashinde->
Sambamba na hoja ya hapo juu, atakaposhindwa Kikwete katika "hila" hii, tukisema mlikuwa mnamwomba Shetani mtakataa? Tukisema maaskofu ni waongo hamjui kuomba mtabisha? Mkisema hayakuwa mapenzi ya Mungu kujibu kwa wakati huu aliliruhusu hili lipite; tutawaambia wanafiki ninyi, maana mliomba kwa tamaa zenu na si sawa na mapenzi ya BWANA Mungu ndiyo maana hamkupata.
Hivi mambo yote mazuri yenye kumpa Mungu utukufu katika Tanzania yanatukia
kwasababu Maaskofu wameombea?
Behold, "kiburi hutangulia maangamivu".
Maaskofu, zichambueni sana kauli zenu kabla ya kuzitoa. Inatuuma pale/kutokana na ukweli uliopo, kauli zenu kuitwa ni
uropokaji[/B; hivyo ninyi kuitwa waropokaji. Kwa uchache ona kauli zenu zinavyoligharimu kanisa;
"Hata watanzania wote wakiihama, mimi nitabakia kuwa mwana-CCM''..Kulola
"Jakaya Kiwete ni chaguo la Mungu"...Kilaini
" Mungu amemvisha Rais Jakaya Kikwete joho la ufahamu na ujasiri kumuwezesha kupambana vita ya kukisafisha CCM na Serikali yake"...Mwasota.
Mnatukwaza sana. Mnatuuumiza sana.
Mnafanya tushambuliwe sana kutokana na kauli zenu.
Ninyi ni viongozi.
Nimeyaandika haya kwasababu najua kuna waumini,wachungaji na maaskofu wengi wanasoma JF na wengine ni members.