Ndugu zangu Watanzania,
Namshauri sana Askofu Gwajima atoke hadharani aombe msamaha kwa yale yote aliyoyafanya. Amuombe msamaha Rais wetu Mpendwa ambaye Ni Mama mwenye huruma na Upendo , Ni Mama mwenye Kujali watu wake na msikivu.
Mama yetu Mpendwa na kipenzi chetu watanzania amesamehe wengi sana ,amewafungulia wengi sana milango ,amewasikiliza wengi sana . Ni mama wa upatanisho, ni Mama wa Amani ,Ni Mama wa huruma ,Ni Mama wa Wote ,Ni Mama wa watanzania wote. Ni Mama mcha Mungu ,Ni Mama mwenye hofu ya Mungu,Ni Mama ambaye hachoki kusamehe ,ni Mama ambaye kwake kutoa msamaha siyo jambo gumu.
Ni Mama ambaye ni msikivu ,ni mama wa Imani. Ni Mama mwenye kuachilia msamaha siku zote. Ndio maana kuna watu wamemtukana sana ,kumdhalilisha sana ,kumsengenya ,kumsaliti lakini wote amewasamehe na kuwafungulia ukurasa mpya wa amani na upendo. Ndio Maana ya kuja na 4R zake.
Hivyo basi askofu Gwajima kwa kutambua makosa aliyoyafanya anapaswa kutoka hadharani kwa hekima , unyenyekevu na upole wa hali ya juu sana kuliomba msamaha Taifa ,kumuomba msamaha Rais wetu,Kuomba msamaha kwa chama chetu cha Mapinduzi na watanzania wote kwa ujumla wake.kwa maneno,matamshi na kauli ambazo alizitoa kwa waandishi wa habari pamoja na madhabahu ya kanisa lake.
Aombe msamaha na kukiri makosa yake na kuahidi kutorudia tena makosa yake. Ya kugeuza madhabahu kuwa uwanja wa kueneza chuki , uchonganishi na mtafaruku. Lazima aombe msamaha kwa kutoa maneno na matamshi yenye kumshambulia Rais na taasisi ya Urais na hivyo kuishushia heshima na kuifedhehesha pamoja na kuichafua kwa maneno yasiyo na ukweli wale ushahidi wa aina yoyote ile.
Kuna sheria na kuna busara na hekima. Kwa magoti na kujutia ajitokeze hadharani na ikiwezekana atafute wazee wa kumsindikiza kuomba msamaha kwa watanzania na kwa Rais wetu Mpendwa.
Ifahamike ya kuwa kanisa la askofu Gwajima limefungwa na sheria na siyo mtu binafsi au au taasisi fulani. Ikumbukwe ya kuwa kila kitu kuongozwa kwa mujibu wa sheria ,kanuni ,katiba na miongozo. Hivyo ifahamike ya kuwa kanisa la askofu Gwajima lilifungwa kwa kukiuka mambo hayo yenye kuongoza uendeshaji wa ibada ambao unakataza mambo ya kuchanganya siasa na Dini hususani mahubiri yenye kuchochea chuki na kuleta uchonganishi pamoja na kuwagawa watu..
Kwa hiyo ifahamike kuwa kanisa halijafungwa na Rais Samia na serikali yake bali limefungwa kwa Mujibu wa sheria, miongozo na kanuni za uendeshaji wake. Lakini pamoja na kufungwa huko kwa kukiuka sheria bado kuna nafasi mbele ya moyo wa Rais wetu ambaye ni msikivu na mwenye moyo wa huruma ,upendo na kusamehe.
Rais wetu Ni mwanadamu na anayependa sana kuona amani na upendo vikitawala huku watu tukisameheana. Naamini askofu Gwajima akikiri na kuomba msamahama atasamehewa na kufunguliwa kanisa lake ili ibada za kweli na zenye kuhubiri neno la Mungu ziweze kuendelea kama kawaida na watu waendelea kuabudu.
Inawezekana askofu alidanganywa au kushawishiwa na watu au kupotoshwa na kupewa taarifa za uongo. na yeye kuamua kubeba bila kufanya utafiti wa kina kupata ukweli. Naamini anayo nafasi ya pili kama mwana mpotevu kurejea kwa Mama yetu kipenzi kuomba msamaha na kufungua ukurasa mpya.
Mama yetu ninayemfahamu mimi kwa siku nyingi tangia nimeanza kufuatilia siasa naamini atamsamehe na kutoa maagizo.
Askofu Gwajima rudi kwa Mama ,rejea kwa unyenyekevu. Na uombe msamaha na utasamehewa tu.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.