Askofu Gwajima: Asante Rais kwa kumtumbua Prof. Muhongo.

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Askofu Gwajima amempongeza Rais Magufuli kwa kumtumbua Prof. Muhongo na kusema liwe ni funzo kwa wale wanaodhani nafasi zao katika madaraka zitakuwa niza milele.

Gwajima amesema, ''Muhongo amekomeshwa vizuri sana kwa sababu wakati ule watu wananunua vitalu vya gesi na wazawa wa Tanzania wakataka wanunue yeye anawaambia hela zenu niza kufungia maandazi''.

Gwajima alienda mbali zaidi na kusema, ''Maandazi yamemfunga yeye badala ya watanzania aliokuwa anawaambia wana pesa za kufungia maandazi''.

Gwajima amemuomba Rais Magufuli asilegeze kamba kuhusiana na suala la maliasili za taifa.

Alisema, ''Namuombea Rais akaze hapohapo, yaani itabidi niombe maombi maalum ili roho yake iwe ngumu akaze hapohapo, hayaendi makontena pamoja na kwamba kuna baadhi ya watu wanapiga kelele eti atashitakiwa''.

''Eee mtashitakiwa, hayaendi makontena, eee mtapelekwa arbitration, hayaendi hayaendi makontena mpaka mzungu atoe macho awe mwekundu kabisa, hayaendi makontena''. Alisema.

Aliendelea kusema, ''Huu sio wakati wa kupiga porojo na kuanza kum-criticize Rais na kusema unajua Rais ameamua vibaya, angefuata process''.

Gwajima alienda mbali zaidi na kusema, ''Yaani wanataka Rais afuate process huku madini yetu yakiendelea kuondoka, ningekuwa mimi ni Rais ningefanya zaidi ya alichokifanya Rais''.

Kwa alichokisema Gwajima angalia video:

VIDEO:


 
Kaongea ukweli kabisa tuna wasomi wengi lakini wanaishia kwenye research na makaratasi ila utekelezaji zero kabisa!!!! sasa muhongo na CV yake nzito ya mambo ya miamba alishindwa kujua tunaibiwa all along???? Dah kaz kwelikweli
 
Kumbe Mzungu ndiye anayetuibia ?
Ni hatari kuamini hivyo !

Njia hii sio sahihi sana .!
Nchi inaongozwa Kwa sheria
Na haijengwi na MTU mmoja wala haiongizwi Kwa kutumia akili za MTU mmoja.

Tuombe njia hii isiwe chaguo la kudumu
 
Kwa hiyo huenda ndoa ya Gwajima na Chadema ndio imekufa au.?

Japo kwa jicho langu la rohoni nimeona kama Gwajima akimnanga Rais......
 
Ameavuta ngada huyo kaanza kuropoka!
Alikuwa wapi kumshauri toka mwanzo?
 
Huyo ni kichaa mwingine anatumia madhabahu kufanya ukichaa wake

Kichaa ni wewe usiejielewa hata kama una cv ya namna gani kuwaona wenzio vichaa, kama huwezi kusaidia nchi yako wewe ni zaidi ya kichaa! Mhongo alishindwaje pamoja na cv yake kubwa kuona kwamba tunaibiwa, ama zile tetesi kwamba ni waziri aliyekuwepo kwenye pay roll ya siaiei ndo tuamini! Ni kweli nchi hii tumerogwa, tukarogeka, mijitu iliyosoma mapema itukomboe, ndio yameuza nchi kwa kipande cha shuka, hivi tofauti ya nyoka wa makengeza, liprof Muongo, et all na Mangungo ni ipi! Shame on us Tanzanian! Wapi adhabu ya kifo kwa wahujumu wa uchumi wetu!!!???
 
Back
Top Bottom