Askofu Glorious Shoo-Misingi ya Amani inatikiswa

Askofu Glorious Shoo-Misingi ya Amani inatikiswa

Unaweza na ndiyo maana ameweza kuweka bayana kwanini hakubaliani nayo. Na ukisoma mstari kwa mstari Askofu huyu ametumia saikolojia ya hali ya juu kuwaeleza waliokuwa wana muhoji.Nenda taratibu na utajua.
Sisi tuliokuwepo tulitamani angeandika makala kwani hamshambulii mtu bali anatoa hoja nzito zinazoeleweka kwa kila mtu.
Mifano yake Ni rahisi mno kuelewa.
 
Sisi tuliokuwepo tulitamani angeandika makala kwani hamshambulii mtu bali anatoa hoja nzito zinazoeleweka kwa kila mtu.
Mifano yake Ni rahisi mno kuelewa.

Nimeona mahojiana yenu ni mazuri kwa kweli lakini unajua ndugu yangu huku kwetu CHAMA kilichomadarakani hakitaki ukweli,na penye ukweli lazima watatafuta maneno ya ziada.

Mara nyingi naona Mwl.Nyerere aliwaendekeza sana hawa kwa kuwapa ujiko kwenye hotuba zake leo hotuba za Nyerere kwa kiasi kikubwa zinatuaafect mno.

Hasa pale anaposema bila CCM eti NCHI itayumba sidhani kama alijua anachokiongea.Leo tunaCCM lakini uchumi wa nchi unayumba na NCHI ni UCHUMI,HAKI na AMANI.Leo HAKI hatuna je tutakuwa na AMANI?
 
Hapo ndipo sisi waamini tunahitaji kuomba. Japo ni sahihi kwa viongozi wetu kukemea , kuonya na hata kukosoa.
 
KATIKA MAHOJIANO NA ASKOFU GLORIOUS SHOO,
ALICHOKISEMA KUHUSU KATIBA MPYA
1. Amani hudumishwa kama kuna HAKI NA MATUMAINI - Matumaini yalikua Ni kupata katiba Mpya lakini yameondoka kwa kutokuwa NA UPYA KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA
2. Haki haikuwepo katika mchakato wa bunge la katiba , kwenye kutunga KANUNI na hata mchakato wa upigaji kura
3, Bila kujali uzuri wa katiba inayopendekezwa bado upungufu wa kutokuwa NA maridhiano Ni jambo kubwa alifananisha na maskini kujengewa nyumba nzuri kwenye kiwanja chake akiwa hatupo.
4. VIONGOZI wa DINI kujihusisha NA siasa alisema siasa maana yake ni kuwashawishi watu kwenda kwenye jambo Fulani. Hivyo kila mtu ni mwanasiasa kwa namna moja au nyingne
5. Alitahadharisha hatari ya viongozi kuondoa maadili katika katiba inayopendekezwa

Yafuatayo ni mazungumzo kati ya Askofu Glorious Shoo wa TAG Kilimanjaro na baadhi yetu ( Vijana waumini wa kanisa lake) kuhusu mtazamo wake juu ya Katiba Mpya.

Vijana: Baba Askofu nini maoni yako kuhusu Mchakato mzima wa kuandika katiba Mpya yetu?

Askofu: Hitaji la kuandikwa kwa katiba mpya lililetwa na mazingira ya wakati huu yaliyoonyesha wazi uhitaji wa mabadiliko na mambo mapya kupitia katiba MPYA.
Tuna kila sababu ya kumshukuru rais wetu mpendwa aliyeamua kuanzisha mchakato huu wakati ukiwa bado haujakubalika kwa wengi katika chama tawala.

Kuna kanuni ya amani inayoitwa MATUMAINI NA HAKI.
A.) "MATUMAINI" NA B.) "HAKI" kanuni hii ni ile inayojua kuwa amani inaweza kuondolewa na watu waliokosa matumaini au watu wenye hisia za kubaguliwa, kuonewa au kutokutendewa haki.
Kanuni ya MATUMAINI inadai kuwa amani bado yaweza kuwepo hata kama mtu anahisi kuonewa au kuondolewa haki endapo atapewa MATUMAINI YA KUIPATA HAKI HIYO katika muda au kipindi anachoweza kusubiri. (muda usiokuwa mrefu.)
Kitendo cha rais kuanzisha mchakato wa katiba ulikidhi mahitaji ya kanuni hii. HUHITAJI KUWA NABII KUJUA KUWA TANZANIA IMECHAGUA NJIA SAHIHI YA AMANI YA TAIFA KWA KUCHUKUA HATUA SAHIHI.

MATUMAINI makuu ya aina hii huweka taifa katika Amani.
Wananchi walipoona majina ya tume ya kuratibu maoni ya katiba walizidisha Imani yao juu ya udhati wa dhamira ya rais na serikali katika kupata katiba mpya.

DOSARI KATIKA MCHAKATO.

Baada ya kila mtu kuisifia na kuipenda rasimu ya katiba ya kwanza na ya pili, matumaini yaliongezeka.
Mchakato uliingia dosari pale wanasiasa walipoanza kuingiza misimamo ya vyama na maslahi yanayoweza kutafsiriwa kuwa ni ya kibinafsi.

KELELE ZA KUBADILISHWA KWA KANUNI KATIKA BUNGE LA KATIBA.
Ni jambo la kawaida na jema kuangalia kama kanuni mlizo nazo zinakidhi mahitaji yaliyopo. Hili likibidi kufanyika linahitaji heshima, uangalifu na weledi wa kuhakikisha kuwa lengo la mabadiliko ya kanuni sio la kuwanufaisha watunga kanuni. Hilo lisipofanyika ( kuhakikisha wadau wanaielewa nia ya kubadilisha) bila kujali ubora wa kanuni husika siku zote litazaa mgogoro.
Ni kama baba anayetaka familia yake ikae kwa utaratibu mzuri unaoeleweka kisha anaanza na utaratibu unaosema hakuna ruhusa mtu kutoka nyumbani isipokuwa yeye tu ( yaani yeye baba). Hakuna ruhusa kula hotelini isipokuwa yeye tu. Hakuna kuchelewa isipokuwa yeye tu. Lakini kama angeelewesha kuwa hali ya usalama katika eneo lao ni mdogo na hapendi familia yake ipate shida kwani ni yeye tu mwenye silaha na anayeweza kuitumia. Hakuna mwanafamilia angepata shida na utaratibu huo.
Sasa bila hilo kuwa sawa unachezea amani kwa kuwa unavunja msingi mkuu wa amani ambao ni "HAKI".
Ili udumishe amani, matakwa ya kanuni ya haki hayakulazimishi tu kuitoa haki bali yanalazimisha pia wadau waone na kujua umetoa haki.

UZURI WA KATIBA INAYOPENDEKEZWA NA TATIZO LISILOONEKANA KWA WAZI.
Bila kujali katiba inayopendekezwa ni bora na nzuri kiasi gani kuna shida ambayo inawezakana hatujaiangalia vizuri.
Inawezekana sana ina mambo mengi mazuri ya msingi na ya muhimu lakini yanapata dosari kutokana na namna yalivyopatikana.
Mfano mzuri ni kama mkulima maskini sana atembelewe na tajiri mkubwa sana. Kisha baada ya tajiri kuona uduni wa nyumba yake ya manyasi na matatizo mengine anaamua moyoni kuwa atahakikisha anamtuma mhandisi bora kuliko wote kumjengea yule maskini ghorofa nzuri na ya kisasa.
Mhandisi anafika na bila ya kumkuta yule maskini (amesafiri) kisha anachagua mahali bora pa kujenga ghorofa bila mwenyewe kuwepo. Kisha ujenzi unaanza kwa kasi ya ajabu huku vifaa vyote vikiwa vimekamilika na mafundi wengi wa kutosha kukamilisha ujenzi ndani ya muda mfupi.
Ghorofa ikiwa imefika katikati anakuja maskini na kukuta watu wanajenga. Unadhani atafanya nini?

VIJANA: MAJIBU YETU
1. Nadhani atakimbilia polisi kuripoti uvamizi huku akiwa na hofu ya haki kutokutendeka.
2.Pengine atamwaga matusi na kutumia silaha yoyote kuwafukuza.
3. Haijalishi watasema nini kuhusu aliyewatuma na hata nia yao nzuri. Hakuna atakayeiamini nia yao.
4. Maskini atakuwa na hofu kuwa msaada huu lazima una kitu kizito kisichokuwa cha kawaida.
5. Anaweza kudhani ujenzi ukiisha watamtoa kafara.

ASKOFU: "Mmejibu vyema" hata kama atakuja kuambiwa nia yao ni njema na nyumba ni yake. Bado hatakuwa na imani na nia ya wajenzi na hata tajiri kwani hakushirikishwa na hawezi kuelewa sababu ya haraka ya kutokusubiriwa ili kukubaliana na ofa ya mtoaji.
Kazi iliyofanywa na wajumbe wa bunge la katiba ni bora na nzuri lakini kama walivyosema mara kwa mara kuhusu ubinadamu wa tume ya Warioba na uwezekano wa makosa basi hata katiba inayopendekezwa yaweza kuwa na mapungufu mengi yanayotokana na ubinadamu lakini UPUNGUFU MKUBWA ilihitaji maridhiano kuliko jambo lolote. Upungufu wake ni maridhiano. Ambayo ni vyema kutokupuuzwa au kuona sio kitu.

KUACHWA KWA MAMBO YA MSINGI YALIYOWAGUSA WANASIASA.
Bila kujali ubora wa katiba inayopendekezwa lakini kwa kuwa mambo yanayogusa 1. Uwajibikaji wa wanasiasa 2. Elimu ya wanasiasa 3. Mamlaka ya raisi 4. Tunu za taifa nk.
Haya yatamfanya kiongozi ajaye kuwa na mwanya wa kubomoa yoyote yaliyoko kwani hajabanwa ipasavyo na katiba.

VIJANA: UNASEMAJE BASI JUU YA AMANI YA TAIFA KWA MISINGI ULIYOTANGULIA KUITAJA YA MATUMAINI NA HAKI.
Kama nilivyotangulia kusema msingi mkuu wa AMANI ni " matumaini na Haki" haya mawili yakikosekana ni kiashirio cha uvunjifu wa amani. Je tuko wapi katika haya mawili?

MATUMAINI:
Je ni matumaini gani wananchi wa itikadi zote walikuwa nayo?

VIJANA: Ni ahadi ya katiba mpya.

Askofu: 1.KATIBA 2. MPYA
Katika maneno hayo mawili hapo juu "KATIBA MPYA" neno lenye nguvu ni MPYA. Hivyo MATUMAINI yanaletwa na neno "MPYA"
Wanasiasa wengi waliowahi kushinda dhidi ya wapinzani wenye nguvu ni wale walioweza kuwa na agenda ya "mabadiliko" ahadi ya kitu kipya.
Sasa katiba inayopendekezwa itapimwa kama imebeba "mabadiliko" na maudhui ya "mpya".
Mapendekezo ya tume yalijaa matumaini hayo MAMBO MAPYA MAZURI. Ukiyazima ghafla matumaini hayo basi uridhishe wadau kuwa haki imetendeka kufikia maamuzi hayo.

VIJANA: NI HATARI GANI UNAYOWEZA KUONA KWAMBA YAWEZA KUHATARISHA AMANI YA TAIFA ZAIDI YA TULIYOKWISHA KUONA?

Askofu: NI MASHAMBULIZI YA WATU KIBINAFSI BADALA YA HOJA.

Kushambulia watu kwa haiba yao, na nafsi zao sio njia bora na ni jambo hatari kwa mshikamano na hata amani.
Nadhani kuna haja ya kujibu hoja juu ya maswali badala ya kushambulia wanaouliza. Au kushambulia waliohusika.

Kama watu wanasema rasimu hii sio nzuri basi waeleze ubaya wake na sio ubaya wa aliyeileta. Kisha waeleze kwa nini wanadhani mbadala wake ni bora kuliko huo. Wanaolizwa maswali pia waepuke kuwashambulia waliouliza. Au katiba inayopendekezwa mtu akisema sio nzuri atoe hoja na wanaojibu wajibu kwa hoja na kwa ufafanuzi.

Haifurahishi kuona Mheshimiwa Sita na Mheshimiwa Warioba wakishambuliwa. Tushambulie mapungufu na kuonyesha mbadala wake. Ila tusishambulie watu.
Na wakati hoja zikitolewa dhidi ya uelewa na misimamo yetu, basi tujibu kwa hoja juu ya tunachodhani ni bora.

Watu wakisema kura za maoni kidogo namna hii zimechakachuliwa basi tueleze kwa uwazi mambo yalivyokuwa na kuthibitisha ukweli wa namna 2/3 ilivyopatikana hata ikibidi kuorodhesha majina ya wajumbe wa Zanzibar kwani sio wengi wala vigumu kuonyesha orodha Mdogo hiyo. La sivyo tukubali na kukiri kuwa tumekosea au tumelazimisha ushindi. Vinginevyo tunyamaze na kusubiri jamii iamue ukweli uko wapi. Ni fedheha na aibu viongozi wakifanya mambo kwa namna ya kutokujali haya. Ni kuwadhalilisha wenye hekima katika nchi yetu.
Tutafute kila njia ya kuwapa watu matumaini na kutenda mambo kwa uwazi na kwa haki ili kulinda amani ya taifa hili. Misingi ya Amani ni Haki na matumaini. Ni afadhali kukubali kushindwa kibinafsi au kichama kwa faida ya amani ya taifa.

VIJANA: UNASEMAJE KUHUSU VIONGOZI WA DINI KUJIHUSISHA NA SIASA?

ASKOFU SHOO:
Ukitafuta maana ya siasa hata kwenye Wikipedia utapata Politics (from Greek: politikos, meaning "of, for, or relating to citizens") is the practice and theory of influencing other people on a global, civic or individual level.
Kwa tafsiri isiyo rasmi maana ya neno politikos ni (" ya, kwa ajili ya.., kuwahusu raia") ni mwenendo au dhana ya kuwahamasisha au kuwashawishi watu duniani au raia au kumwamasisha mtu kibinafsi (kuwa na mwelekeo fulani.)
Kwa tafsiri hii kila raia siasa inamhusu.

Mara nyingi hoja hii ya kutokuhusisha SIASA NA DINI hutolewa na wanasiasa na kwa bahati mbaya huwa inatolewa pale tu ushauri, maoni au mawazo au hoja za viongozi wa dini zinapokinzana na matakwa ya wanasiasa. Lakini viongozi wa dini kuna wakati wamesema wanasiasa fulani ni chaguo la Mungu. Kwa bahati mbaya hilo halikemewi sana. Sasa kama VIONGOZI WA DINI wakitusemea vizuri na tukakubalika kwa jamii na kuona ni sawa basi tuwe tayari pia kusemwa tofauti au kukosolewa.

VIJANA: KWA KWELI TUNASHUKURU TUNAOMBA UANDIKE MAKALA AU TURUHUSU SISI TUITUME KWA JAMII.
ASKOFU: MNARUHUSIWA KUFANYA HIVYO KAMA HAMTAONGEZA LOLOTE AMBALO SIKULISEMA.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Haya maneno ni ya hekima sana. Wenye ufahamu wachache watakubaliana na Askofu. May the Lord God open the eyes of our Leaders to see where our country is heading.
 
Hapo ndipo sisi waamini tunahitaji kuomba. Japo ni sahihi kwa viongozi wetu kukemea , kuonya na hata kukosoa.

Shida imekuja baada ya viongozi wetu wa dini kujali pesa za michango toka kwa viongozi wasio waadilifu kuwa ndiyo wageni rasmi kwenye hafla za makanisa au misikiti.Leo ukija na kuwakemea unadhani watakusikia?Lakini kama toka mwanzo wangekuwa firm na hawa wezi wa raslimali zetu,hata kukemea kwao kungesikika.!

Wanaona kama wenzao waliokuwa wanakula nao,na ndiyo maana ikija wakati wa kukemea wanakemewa pia kwamba msiingilie SIASA.

Leo Afrika ya Kati vita kati ya waislamu na wakristu viongozi wote wa siasa wamekimbia wamewaacha wananchi na viongozi wao wa dini.Nina uhakika wakati wanasiasa hawa wakikemewa!waliwakemea pia viongozi wa dini kuwa wasiingie kwenye siasa.Vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaletwa na wanasiasa na hasa vyama tawala.
 
miongoni mwa mambo aliyosema Askofu Shoo wakati anaongea kuhusu DINI NA Siasa Ni mfano uliowahi kutolewa NA viongozi wa dini kuwa. Mkiwa mko kwenye meli kisha MMOJA wenu akawa anatoboa, unapomuuliza anasema sio juu yako. Haikuhusu. ( HATUWEZI KUWAACHA WANASIASA WAKAHARIBU TAIFA NA NCHI YETU HUKU WAO WAKIJARIBU KUTUNYAMAZISHA.)
 
Hawa viongozi wa dini wakiacha kuwaalika hawa wanasiasa kwenye hafla za kujengea majengo ya kanisa kuwa wageni rasmi ndipo wataanza kuheshimiwa,vingine heshima haiwezi kuja maana wote wanakuwa sawa,huyu FISADI anapeleka RUSHWA yake kanisani na Kiongozi anaibariki unategema nini hapo?

Viongozi hawakemei na wakikemea wanatingisha kibiriti kwani atarudi kujisafisha kupitia michango ya kanisa akiwa mgeni rasmi.Na waumini tunapiga makofi na vigelegele.Umeiona hii lakini?
 
Kuna ukweli mkubwa hapa.
 
Nimeipenda namna alivyojibu maswali toka kwa vijana hao. Ukisoma kwa makini maelezo/majibu yake imeonesha competence, busara na uelewa wa mambo na siyo kukurupuka. I LIKE IT!
 
Nimeipenda namna alivyojibu maswali toka kwa vijana hao. Ukisoma kwa makini maelezo/majibu yake imeonesha competence, busara na uelewa wa mambo na siyo kukurupuka. I LIKE IT!
tunamshukuru Mungu kuwa na watu wenye hekima ya kimungu.
 
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Haya maneno ni ya hekima sana. Wenye ufahamu wachache watakubaliana na Askofu. May the Lord God open the eyes of our Leaders to see where our country is heading.[/QUOTE]
Kwa kweli tuliliona hilo ndio maana tukaamua kuleta hii hoja hapa.
 
Tunapaswa kuliombea taifa hili kwani HAKI na MATUMAINI vimeondolewa na watawala na baadhi ya vyombo vya dola.
Kwa kuwa Mungu hujali sana HAKI basi yeye uhukumu sana kwa HAKI kila uonevu, ubabe na kiburi.
 
Miongoni mwa mambo aliyoendelea kufafanua ni haya yafuatayo:
TATIZO HALIPO KATIKA UBORA WA YALIYOMO KATIKA "Katiba inayopendekezwa" Hakuna ubishi kuwa mambo Mengi ni bora sana kwa yale yaliyomo. TATIZO NI MAMBO MAKUBWA YA MSINGI YALIYOONDOLEWA. Itakuwa ni kucheza na akili za watu kama tunajadili KATIBA INAYOPENDEKEZWA badala ya kujadili mapendekezo ya wananchi yaliyoachwa.
Ni kama mtu anakupa jengo zuri ambalo KWA nje halionekani kuwa na shida, kumbe msingi wake sio imara na halitadumu.
Jengo hilo ni hatari na laweza kukuporomokea. Maadili YALIYOONDOLEWA yanafanya Uwajibikaji na usimamizi wa katiba kuwa mgumu.
 
put urs which u think gonna be richest!!!! teh!
Tulicho hitaji hapa ni nini maudhui ya ujumbe wake.
sasa wewe kama ulitaka aandike kama "foot note" hilo bado lipo ndani ya uwezo wako mpaka sasa kufanya vivyo.
Ushauri ulizingatiwa.
 
Back
Top Bottom