Uchaguzi 2020 Askofu Bagonza: Uchaguzi Mkuu au Utekaji Mkuu au Ujazaji fomu Mkuu?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,109
UCHAGUZI MKUU

au

UTEKAJI MKUU

au

UJAZAJI FOMU MKUU

Kutokana na vyombo vingi vya habari kuwa likizo katika msimu huu, jamii inakosa habari muhimu. Magazeti mengi, TV na Redio vimepelekwa likizo kwa muda mpaka mwezi Novemba. Vyombo vichache vilivyobaki vina matatizo makubwa shingoni. Vinabaki vimeangalia upande mmoja maana vikigeuza shingo ili kuangalia upande mwingine, vinasikia maumivu makali. Matokeo yake, matukio mengi yamehamia upande wa pili wakati shingo limeendelea kuangalia eneo lisilo na matukio.

Kuna mtafaruku. Wengi tuliamini huu ni msimu wa UCHAGUZI MKUU. Taarifa za vyombo visivyo rasmi zinadai ni msimu wa UTEKAJI MKUU. Na vyombo visivyo na usajiri wa TCRA vinasema huu ni msimu wa UJAZAJI FOMU MKUU. Ipo haja ya kushtuka:

1. Wanaozusha kutekwa na wanaoteka kweli wajue, haiwezekani kuteka mapenzi ya watu. Hakuna adhabu kubwa kwa kiongozi kama kuongoza miili tu huku mioyo iliongozwa na waliotekwa.

2. Kujaza fomu si mtihani wa taifa. NEC inunue mifuto ya kutosha. Wananchi wanataka mtu awaongoze, si fomu iliyojazwa vizuri au vibaya. Mnanibishia? Nendeni muwaulize. Wagombea pia ni wapiga kura. Taarifa zao mnazo zote kupitia kadi zao za NIDA na NEC.

3. Mpaka sasa, vyama vya siasa havina shida baina yao . Wanachama wanajuana mambo yao. Ndo maana mmoja anakatwa huku, kesho yake anachukua fomu kule. Tatizo ni vyombo vya serikali. Nani avifundishe kuwa ugomvi wa Baba wa Mama usiingiliwe na watoto?. Wachukue mpira wakacheze uwanjani. Wakirudi jioni watakuta Baba na Mama tayari wanacheka na mdogo wao amezaliwa.

4. Kuna uhusiano mkubwa kati ya UHURU na UCHAGUZI MKUU. Hakuna uhusiano kati ya UTEKAJI MKUU na maendeleo. Wala hakuna uhusiano wowote kati ya UJAZAJI FOMU MKUU na Utawala Bora. Cha msingi ndani ya UCHAGUZI MKUU kuna Uhuru, Maendeleo, Utawala Bora ambavyo vikiungamishwa vinakomesha UTEKAJI MKUU na kuboresha UJAZAJI FOMU MKUU.

Nawasihi wanaopongeza, wanaokosoa, wanaofoka foka, wanaotafuta wasio raia, waliokwepa kodi na wachochezi, wasihangaike kutumia dawa ya bei mbaya. Dawa kuu ya kukomesha hayo yote ni UCHAGUZI MKUU, si UTEKAJI MKUU wala UJAZAJI FOMU MKUU.
UCHAGUZI MKUU uliofanyika kwa haki na kwa Uhuru unatibu magonjwa hayo.

Askofu Bagonza
 
Huyu askofu genius sana

Asante baba askofu
Watanzania wenye upeo wa namna hii na wako tayari kusema bila kuogopa ni wachache sana. Ebu ona hizi busara hapa: ''Wanaozusha kutekwa na wanaoteka kweli wajue, haiwezekani kuteka mapenzi ya watu. Hakuna adhabu kubwa kwa kiongozi kama kuongoza miili tu huku mioyo iliongozwa na waliotekwa''.
 
Huyu si aliambiwa na mkuu wake askofu Shoo kwamba wajitenge na siasa?
Anajitengaje wakati..
1. Naye ni mpiga kura?
2. Naye ataishi maisha yote yanayoamuliwa na siasa?
3. Naye ataongozwa na rais atakayetokana na chama cha siasa?
4. Naye ataongozwa na mbunge atakayetokana na chama cha siasa?
5. Naye ataongozwa na diwani atakayetokana na chama cha siasa?
 
Kabisa Mkuu wahuni hawa wanajua fika kwamba hawana ubavu wa kushinda uchaguzi kihalali hivyo wameamua kutumia njia haramu ili kung’ang’ania madarakani.

Safari hii itawatokea puani na ndiyo itakuwa mara yao ya mwisho kufanya uhuni wao wa kubaka haki na uhuru wa Watanzania katika kuchagua Wabunge na Rais.


Hili taifa limeharibiwa na CCM
 
Watu wazima wamejifungia wiki na zaidi sasa wakitafuta njia ya kukata jina la Tundu Lissu bila kuacha alama...

Ni vigumu mno kuamnini kama haya yote yanaweza kutendeka ndani ya Tanzania hii hii ya Mwalimu Nyerere.

Taifa la kutafutiana makosa na kujeruhiana kama wanyama wa msituni...hapa ndipo tulipofikia kwa sasa!!

Siasa za vitisho; siasa za vita; adui ni yeyote yule anayemkosoa mtukufu.
 
Back
Top Bottom