Askofu Bagonza: Ni Nyerere tu!

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,009
NI NYERERE TU..

Leo ni siku ya NYERERE. Jina hili ni fursa kwetu sote.
Amani na umoja wetu ni matunda ya ubongo na mikono yake.

Mapema mwaka 1996 nilifika Kijijini Butiama kwa kazi maalum ya maandalizi ya masomo yangu ya juu nchini Marekani.

Majira ya saa 4 asubuhi nilipokelewa na kusubirishwa kuonana naye. Yeye alikuwa na maongezi watu wengine wanne walioonekana walikuwa wamelala hapo nyumbani. Niliwatambua watatu: Makongoro Nyerere, Masumbuko Lamwai na Mabere Marando. Hawa walikuwa ni wabunge machachari wa chama Cha upinzani cha NCCR-Mageuzi na mmoja wao akiwa ni mtoto wake wa kuzaa.

Katika uchanga wa demokrasia ya vyama vingi wakati ule, tulikuwa na Baba wa Taifa aliyewapokea nyumbani kwake wapinzani, wakalala kwake, wakala naye, wakazungumza naye na wakaendelea kukipinga na kukikosoa chama alichokiasisi. Kwenye kampeini za 1995, Vijana hawa walikuwa wamempa taabu Baba wa Taifa wakati akimnadi mgombea wa CCM (Hayati Mkapa) wakati wao wakimnadi Mzee Lyatonga Mrema.

Kwenye mitihani ya darasani tunapoulizwa kwa nini Tanzania tuna amani, huwa tunadai kuwa ni sababu ya lugha moja, kutoruhusu ukabila na udini, na program maalum za kuunganisha watu kama JKT.

Tunasahau kuwa nchi kadhaa za kiafrika zenye mifumo ya kijamaa na za kibepari, zenye lugha moja, zenye dini moja au nyingi nk, hazina umoja wala amani. Kwa nini Tanzania?

Mimi nasema ni kwa sababu ya Mwalimu Nyerere. Nchi hizo zilikuwa na kila kitu tulicho nacho lakini hazikuwa na Mwalimu Nyerere. Yeye alikuwa mwana CCM na Mpinzani hapo hapo. Hakuabudu vitu, aliabudu utu. Hakuabudu watu aliabudu utu. Hakuabudu taasisi yoyote, aliabudu sera na maono (aliwahi kusema CCM si mama yake), hakuleweshwa na sifa alizopewa, aliwahoji wanaomsifia. Alikuwa mtetezi wa HAKI ndani na nje. Alichukia ubeberu si kuchukia rangi ya ngozi yao. Kama ubeberu ungekuwa ni rangi asingekuwa na karani mzungu ofisini kwake (Mama Joan Wickens). Aliamini binadamu wote ni sawa na kulitetea hilo.

ILI kuonyesha uumini wake katika umoja wa kitaifa, alipoona mnyukano wa matokeo ya Uchaguzi wa Zanzibar mwaka 1995, alipendekeza kwa mara ya kwanza uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa. Alipuuzwa wakati huo, akakubaliwa baadaye.

Kama Mwalimu ni kipimo chetu, tukubali tumerudi nyuma. Hatuna amani tuna utulivu. Hatuna HAKI tuna uvumilivu. Hatuna matumaini, tuna dukuduku.

Inawezekana sana, HATUMJUI MWALIMU.

Happy Nyerere Day.
 
Wapo Watu waliona mbali na sio urefu wa Pua pamoja na ukubwa wa Madaraka waliyo kuwa nayo ,Mwalimu alifanya mengi mazuri sana ila siwezi kuacha kumlaumu kwa kutuachia Katiba ambayo hata yeye mwenyewe aliiona uhatari (mapungufu) wake kama Nchi ikishikwa na Kichaa.
 
Tumuombe Mwenyezi Mungu Mkuu 🙏🏾🙏🏾🙏🏾 tofauti ya Lissu na huyo Kaburu itakuwa ni kubwa sana. Kutakuwa hakuna hofu tena ya aina yoyote ile. Tutakuwa na uhuru wa kuikosoa Serikali vyombo vya habari vitakuwa huru kuripoti chochote bila wasiwasi wa kufungiwa. Bunge, mahakama na katiba vitaheshimiwa. Wanachi wote wataheshimiwa na kuwa na haki sawa na siyo kuishi kwa hofu kama vile ni Wakimbizi. Furaha ya Watanzania iliyopotea itarudi tena mtaani.
Kuna ombwe kubwa la uongozi ambao Lissu anakuja kiliziba
 
Huyu mzee ni mtu mhimu sana.

Nashauri baada ya uchaguzi awezeshwe ili kipaji chake kitusaidie kama taifa.

Namuona kama presidential material.
Nashauri 2025 atie nia kupitia chama popular cha wakati huo .
Hapana.
Anafaa kuwa mshauri wa rais

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Hapana.
Anafaa kuwa mshauri wa rais

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app

Kwanini HAPANA?

Kua Mshauri nadhani ndio
njia mojawapo ya Kuwezeshwaa kwenyewe niliko kuzungumzia, nikiwa na maana kua azoee mazingira na mifumo ya kiutawala

Baada ya hapo atie nia.

Case study...... Mrithi wa Shizo Abe...japan.
 
Huyu Askofu anafaa kabisa kuwa mshauri wa raisi,uanaijua vizuri nchi hii zaidi sana aone inavowezekana aingie kwenye siasa
 
Naam Baba wa Taifa alifanya mengi mazuri sana lakini kosa lake kubwa ni la kutuachia katiba ambayo alijua fika kwamba ilikuwa ilimpa madaraka makubwa sana na akiingia madarakani kaburu basi ataitumia vibaya. Sasa maneno yake yametimia.
Wapo Watu waliona mbali na sio urefu wa Pua pamoja na ukubwa wa Madaraka waliyo kuwa nayo ,Mwalimu alifanya mengi mazuri sana ila siwezi kuacha kumlaumu kwa kutuachia Katiba ambayo hata yeye mwenyewe aliiona uhatari (mapungufu) wake kama Nchi ikishikwa na Kichaa.
 
Kama Mwalimu ni kipimo chetu, tukubali tumerudi nyuma. Hatuna amani tuna utulivu. Hatuna HAKI tuna uvumilivu. Hatuna matumaini, tuna dukuduku.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom