PostGE2025 Askofu Bagonza: Maridhiano au maviziano?

PostGE2025 Askofu Bagonza: Maridhiano au maviziano?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mwizukulu wa Buganda

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2024
Posts
665
Reaction score
1,809
Hili ni gumu kuliko yote. Kuna watu wameanza kumharibia Mama wakati ana uwezo wa kujiharibia. Wanazuia miili ya waliokufa isitolewe, wanazuia takwimu za waliopotea zisijulikane. Wanatisha madaktari, wauguzi, madereva, familia nk. Ili taifa lipone na kuanza kufikiria maridhiano:

- Idadi ya waliokufa ijulikane

- Idadi ya waliojeruhiwa

-Idadi ya waliopotea na haijulikani kama wamekufa au wako hai.

-Waliotekwa wapatikane

-Kesi za uhaini zifutwe

- Mali zilizoharibiwa zijukikane

- Kamata kamata ikomeshwe. Kama ni lazima, tukamate siyo kuteka (Aliyeanzisha wazo la kuteka afanyiwe ibada maalum).

-Waliokimbia warudi nyumbani

- komesha mateso wakati wa kuhoji. Siku tusiyoijua, hili litatugharimu. Tunasomesha wataalam ili wapate ushahidi bila kutesa watu.

- Hekima itumike kushughulika na tishio
jingine la maandamano. Wateule
wenye hulka “mpasuko” wawekwe
uani.

-Vyombo huru vya habari viwe huru
kweli; vilivyokuwa huru wakati vingine
vimenyamazishwa, sasa vinyamaze ili
vifaidi matunda ya kutunyima habari
za kweli. Uhuru na ukweli ni dawa.

Tusipofanya haya ya namba 10, tutakuwa TUNAVIZIANA siyo KURIDHIANA.

MWISHO:
Gen Z, ni kunguru asiyefugika. Wako vyama vyote, dini zote, makabila yote, familia zote na matabaka yote ya kiuchumi. Kutoka Bunge hili la chama kimoja na lililochaguliwa siku ya msiba wa Gen Z, sioni Waziri wa Gen Z. Lakini tukiacha kutumia nguvu, vikosi kazi na mitutu, twaweza kufanikiwa. Bado Gen Z ni muhimu kuwa Ikulu zote nchini.

Nimewakera? Nisameheni ili niwakere tena.
 
Nimewakera? Nisameheni ili niwakere tena. 😀
 
Askofu wa ukweli. Ngoja wale jamaa wa shughuli waje kusema rais akiwa muisilamu anaandamwa.
 
Back
Top Bottom