Askofu Bagonza: Hili la Dr Bashiru na matumizi ya Dola inamanisha Hata tukipiga tusipopiga kura bado dola itaamua nani mshindi

Mkiambiwa watu wagumu kuelewa mnapanik kisa tu kaongea mtu anae ipongeza ccm hakuna sehem amesema kwamba kwa kutumia dola watatawala milele ila kasema kwa kutumia dola atafanya mambo mengi Mazur IL ccm ibak madarakan hata kama kusema atatumia dola hakwenda moja kwa moja kwamba hata kwenye uchaguz dola ndio inaamua Nan apite wapinzani izi sio hoja za kuwaokoa tafuten NJIA ambayo itawasaidien

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngoja nikuulize sawali dogo tu, ni kwanini huyo Katibu mkuu alisema wazi kuwa wao CCM hawatakubali yaliyowapata KANU ya Kenya na UNIP ya Zambia........

Kama hakumaanisha kuwa chama tawala ni lazima kitumie dola kubaki madarakani?
 
Ningekuwa mimi ni katibu mkuu nisingesema hayo maneno. Hata kama Askofu asingesema alichosema, wengi tuna ufahamu wa kutosha sana.

Kilichopo ni kuwaona raia hawana wanachoweza kuwaza wala kutenda.

Unajiuliza, kwanini aseme hivyo? Asingesema angepoteza nini? Alichokisema kinamsaidia nani hasa sasa na hapo baadaye?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wachache wenye madaraka wanaamua kutumia vyombo vya dola kulinda vyeo vyao kupitia mgongo wa chama tawala.
CCM kinataka kulinda maslahi yao kupitia mtutu wa bunduki.
Wanawachonganisha wananchi na vyombo vyao vya dola mana watoto wao hawana shida zaidi ya kuogelea kwenye mahela ya walipa kodi na kula raha kama yule RC.
Ndio maana hata Bashiru ameamua kuwatupa wananchi wapiga kura na kuvuruga Misingi ya demokrasia na utawala bora ili tu kulinda nafasi yake ya ukatibu mkuu.
Bashiru Yupo tayari kuona damu za watoto wa taifa hili wakiumizwa na kuteshwa hata kuuawa kwa sababu tu ya kulinda ukatibu wake na chama chake.
Imani na dini amevitupilia mbali kwa sababu ya madaraka amesahau kabisa kuwa yeye ni mwanadam ; kuna leo na kesho, kuna kujibu mbele za Hakimu wa wote kule ahera.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaandika Baba Askofu Dk Bagonza kutokea Dayosisi ya KKKT Karagwe Kagera.

Dr. BASHIRU NA MATUMIZI YA DOLA.

Duh!! Najua hili limegusa sana. Kila gazeti litaandika na sisi "mashabiki waandamizi" hatukosi cha kuchangia. Dr. Bashiru ni mtu makini, hawezi kukosa ufafanuzi. Anapojiandaa kufanya hivyo, ajue matamshi yake yanaweza kumaanisha moja ya haya au yote kwa pamoja:

1. Wapiga kura hawaamui mshindi, dola ndiyo inaamua ( Wananchi mpige kura, msipige, mtupatie kura au mtunyime, haisaidii lolote).

2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi siyo huru na haina lolote. Dola ndiyo inaamua mshindi.

3. Chama tawala hakina uwezo kuliko dola na hakishiki hatamu. Dola ndiyo imeshika hatamu.

4. Dola haina uhuru wa kujiamulia, bali inaagizwa na chama tawala (inatumiwa).

5. Hata wabunge na madiwani wa upinzani walioshinda, ni kwa fadhila za dola.

6. Tunapoteza raslimali kuendesha uchaguzi uliokwishaamuliwa na dola.

7. Kwa kuwa dola ndiyo inaamua, siku ikiamua vinginevyo, chama tawala kitaondoka madarakani.

Naamini sivyo alivyomaanisha lakini masikioni ndivyo alivyosikika. Kuna haja ya kujisikiliza kabla hujasikilizwa.
Hii ndiyo hasara ya viongozi waropokaji wa awamu hii, hawapimi kwanza hata athari ya kauli zao. Hata yale mambo ya sirini huropoka tu kutokana na ulevi wa madarakani. Hongera Dk. Bagonza kwa kuliona jambo hili lenye ukakasi mwingi na kulitolea kauli iliyojaa hekima nyingi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna matatu kuhusu Askofu, inawezekana:

1. Hajamuelewa katibu mkuu

2. Kamuelewa lakini kaamua kupotosha

3. Ni kweli Katibu mkuu ameeleweka Kama Askofu alivyomuelewa.

Ili kujua hayo matatu:

1. Katibu mkuu aombwe kutoa ufafanuzi wa kauli hiyo

2. Tusiwe wepesi kutafsiri tusivyoelewa

3.Tukubali kueleweshwa pale tusipojua

Kama Askofu kamuelewa Katibu mkuu na kaamua kupotosha: je, ni Nani anamtuma? Anamtuma kwa lengo gani? Kwa Nini kakubali kutumika hivi? Je Hana Roho wa Mungu wa kumfunulia ili aelewe?
KARLO MWILAPWA, kama unaamini Dr Bashiru hakueleweka vizuri, mshauri hasiwe anaongea na watanzania kama alivokua anafunsisha wanafunzi wake pale UD asitumie nadharia za kitaaluma ilihali akijua anaongea na watanzania wenye elimu na wasio na elimu.
Atume lugha na nadharia inayoeleweka kisawasawa bila tashwishwi na utetezi eti hajaeleweka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaandika Baba Askofu Dk Bagonza kutokea Dayosisi ya KKKT Karagwe Kagera.

Dr. BASHIRU NA MATUMIZI YA DOLA.

Duh!! Najua hili limegusa sana. Kila gazeti litaandika na sisi "mashabiki waandamizi" hatukosi cha kuchangia. Dr. Bashiru ni mtu makini, hawezi kukosa ufafanuzi. Anapojiandaa kufanya hivyo, ajue matamshi yake yanaweza kumaanisha moja ya haya au yote kwa pamoja:

1. Wapiga kura hawaamui mshindi, dola ndiyo inaamua ( Wananchi mpige kura, msipige, mtupatie kura au mtunyime, haisaidii lolote).

2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi siyo huru na haina lolote. Dola ndiyo inaamua mshindi.

3. Chama tawala hakina uwezo kuliko dola na hakishiki hatamu. Dola ndiyo imeshika hatamu.

4. Dola haina uhuru wa kujiamulia, bali inaagizwa na chama tawala (inatumiwa).

5. Hata wabunge na madiwani wa upinzani walioshinda, ni kwa fadhila za dola.

6. Tunapoteza raslimali kuendesha uchaguzi uliokwishaamuliwa na dola.

7. Kwa kuwa dola ndiyo inaamua, siku ikiamua vinginevyo, chama tawala kitaondoka madarakani.

Naamini sivyo alivyomaanisha lakini masikioni ndivyo alivyosikika. Kuna haja ya kujisikiliza kabla hujasikilizwa.
Pamoja na usomi wake Dr Bashiru has stooped too low,hawajiamini na hawaheshimu maamuzi ya wapiga kura.Ndiyo maana sasa wanaanza kukiri kuwa wanawanunua wapinzani,wameiteka Tume ya Uchaguzi,Polisi na Mahakama hivyo mpige kura au msipige haiwahusu.Wao ni washindi iwe mvua,liwe jua wanashinda kwa 99.9999%.Wanajiona bora kuliko Wananchi, wamelewa mvinyo wa damu za wapinzani wao.
 
Kama mtumishi umemwelewa amesema huwenda akawa anamaanisha vinginevyo Ila masikioni ndivyo alivyosikika, kabla hujamlaumu mtu nivema ukajiuliza wewe mwenyewe ulivyoelewa kwani swala lauelewa nilamtu binafsi hivyo huwezi mlaumu mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bagonza bora atangaze tu nia yake,huko anakoelekea si pazuri anaisakama sana dola
 
Kuna matatu kuhusu Askofu, inawezekana:

1. Hajamuelewa katibu mkuu

2. Kamuelewa lakini kaamua kupotosha

3. Ni kweli Katibu mkuu ameeleweka Kama Askofu alivyomuelewa.

Ili kujua hayo matatu:

1. Katibu mkuu aombwe kutoa ufafanuzi wa kauli hiyo

2. Tusiwe wepesi kutafsiri tusivyoelewa

3.Tukubali kueleweshwa pale tusipojua

Kama Askofu kamuelewa Katibu mkuu na kaamua kupotosha: je, ni Nani anamtuma? Anamtuma kwa lengo gani? Kwa Nini kakubali kutumika hivi? Je Hana Roho wa Mungu wa kumfunulia ili aelewe?
Mbona alitafsiri the same day..!

Kiufupi siyo mtu makini alipotosha waziwazi maana ya dola.

Eti dola ni TRA inapokusanya kodi

Itoshe kumuonesha watanzania si wajinga wanauwezo wa kudadavua mambo kuliko ata yeye na degrii zake za sayansi ya siasa amejiumbua kuongea bila kutafakari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fafanua wew sasa uliye elewa kumzidi Askofu
Kuna matatu kuhusu Askofu, inawezekana:

1. Hajamuelewa katibu mkuu

2. Kamuelewa lakini kaamua kupotosha

3. Ni kweli Katibu mkuu ameeleweka Kama Askofu alivyomuelewa.

Ili kujua hayo matatu:

1. Katibu mkuu aombwe kutoa ufafanuzi wa kauli hiyo

2. Tusiwe wepesi kutafsiri tusivyoelewa

3.Tukubali kueleweshwa pale tusipojua

Kama Askofu kamuelewa Katibu mkuu na kaamua kupotosha: je, ni Nani anamtuma? Anamtuma kwa lengo gani? Kwa Nini kakubali kutumika hivi? Je Hana Roho wa Mungu wa kumfunulia ili aelewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaandika Baba Askofu Dk Bagonza kutokea Dayosisi ya KKKT Karagwe Kagera.

Dr. BASHIRU NA MATUMIZI YA DOLA.

Duh!! Najua hili limegusa sana. Kila gazeti litaandika na sisi "mashabiki waandamizi" hatukosi cha kuchangia. Dr. Bashiru ni mtu makini, hawezi kukosa ufafanuzi. Anapojiandaa kufanya hivyo, ajue matamshi yake yanaweza kumaanisha moja ya haya au yote kwa pamoja:

1. Wapiga kura hawaamui mshindi, dola ndiyo inaamua ( Wananchi mpige kura, msipige, mtupatie kura au mtunyime, haisaidii lolote).

2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi siyo huru na haina lolote. Dola ndiyo inaamua mshindi.

3. Chama tawala hakina uwezo kuliko dola na hakishiki hatamu. Dola ndiyo imeshika hatamu.

4. Dola haina uhuru wa kujiamulia, bali inaagizwa na chama tawala (inatumiwa).

5. Hata wabunge na madiwani wa upinzani walioshinda, ni kwa fadhila za dola.

6. Tunapoteza raslimali kuendesha uchaguzi uliokwishaamuliwa na dola.

7. Kwa kuwa dola ndiyo inaamua, siku ikiamua vinginevyo, chama tawala kitaondoka madarakani.

Naamini sivyo alivyomaanisha lakini masikioni ndivyo alivyosikika. Kuna haja ya kujisikiliza kabla hujasikilizwa.
Tunamshukuru Baba Askofu kwa kutonyamaza. Katika lindi la uvuli wa mauti wa wasiojulikana inakubidi ujikane kufanya afanyayo baba Askofu Bagonza. KUTOA MAWAZO YAKE. Mwenyezi Mungu amlinde. Tunakumbuka yaliyomkuta aliyekuwa anatoa mawazo yake yule mbunge ambaye hata kumtaja ni hatari mbele ya wasiojulikana maana Mwenyezi Mungu amewaumbua ushetani wao unaojulikana na malipo yake hawajayalipa bado
 
Kuna matatu kuhusu Askofu, inawezekana:

1. Hajamuelewa katibu mkuu

2. Kamuelewa lakini kaamua kupotosha

3. Ni kweli Katibu mkuu ameeleweka Kama Askofu alivyomuelewa.

Ili kujua hayo matatu:

1. Katibu mkuu aombwe kutoa ufafanuzi wa kauli hiyo

2. Tusiwe wepesi kutafsiri tusivyoelewa

3.Tukubali kueleweshwa pale tusipojua

Kama Askofu kamuelewa Katibu mkuu na kaamua kupotosha: je, ni Nani anamtuma? Anamtuma kwa lengo gani? Kwa Nini kakubali kutumika hivi? Je Hana Roho wa Mungu wa kumfunulia ili aelewe?
Kwenye debate mawazo yako ni ya wale wanaotaka kuonekana kwamba wanapambanua mambo lakini ndani yake ni pumba tupu
 
Kuna matatu kuhusu Askofu, inawezekana:

1. Hajamuelewa katibu mkuu

2. Kamuelewa lakini kaamua kupotosha

3. Ni kweli Katibu mkuu ameeleweka Kama Askofu alivyomuelewa.

Ili kujua hayo matatu:

1. Katibu mkuu aombwe kutoa ufafanuzi wa kauli hiyo

2. Tusiwe wepesi kutafsiri tusivyoelewa

3.Tukubali kueleweshwa pale tusipojua

Kama Askofu kamuelewa Katibu mkuu na kaamua kupotosha: je, ni Nani anamtuma? Anamtuma kwa lengo gani? Kwa Nini kakubali kutumika hivi? Je Hana Roho wa Mungu wa kumfunulia ili aelewe?
Umesahau Bushiru alivyopindisha kuhusu Azory Agwanda.

Mara zote kauli ya kwanza huwa ya kweli na hakika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom