Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Anaandika Baba Askofu Dk Bagonza kutokea Dayosisi ya KKKT Karagwe Kagera.
Dr. BASHIRU NA MATUMIZI YA DOLA.
Duh!! Najua hili limegusa sana. Kila gazeti litaandika na sisi "mashabiki waandamizi" hatukosi cha kuchangia. Dr. Bashiru ni mtu makini, hawezi kukosa ufafanuzi. Anapojiandaa kufanya hivyo, ajue matamshi yake yanaweza kumaanisha moja ya haya au yote kwa pamoja:
1. Wapiga kura hawaamui mshindi, dola ndiyo inaamua ( Wananchi mpige kura, msipige, mtupatie kura au mtunyime, haisaidii lolote).
2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi siyo huru na haina lolote. Dola ndiyo inaamua mshindi.
3. Chama tawala hakina uwezo kuliko dola na hakishiki hatamu. Dola ndiyo imeshika hatamu.
4. Dola haina uhuru wa kujiamulia, bali inaagizwa na chama tawala (inatumiwa).
5. Hata wabunge na madiwani wa upinzani walioshinda, ni kwa fadhila za dola.
6. Tunapoteza raslimali kuendesha uchaguzi uliokwishaamuliwa na dola.
7. Kwa kuwa dola ndiyo inaamua, siku ikiamua vinginevyo, chama tawala kitaondoka madarakani.
Naamini sivyo alivyomaanisha lakini masikioni ndivyo alivyosikika. Kuna haja ya kujisikiliza kabla hujasikilizwa.
Pia soma > Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao