Askofu Bagonza aamua kumtetea Prof Kabudi, asema yuko sahihi katoka jalalani

Falsafa kazini.!
Napenda watu wa kunifikirisha.

Muchas gracias padre obispo!!
Estoy muy feliz para tus parablas amables.

Me gustaria las frases cognativas
 
Duuh alafu ndo mnafiki kama huyu anahubiri suala la Kwenda mbinguni...!!
 
Hiyo sentensi ya mwisho ndio imenifurahisha zaidi!
 
"Nami nimeamua kujitoa akili ili kumtetea." hii ndio sentensi iliyobeba maana nzima ya uzi wa Baba Askofu Bagonza kwa sababu bila kujitoa akili huwezi kumtetea propesa kikamilifu na watu wenye afya njema ya akili wakakuelewa hata kidogo!

Hata hivyo naheshimu maoni ya Askofu, yeye ndiye anayejua kwa nini kaamua kujitoa akili kumtetea propesa.
 
Ulichoandika hakina uhusiano na hoja iliyotolewa. Inaelekea una tatizo la akili
 
Ma prof wanahali mbaya Sana kwani wanakaa, kula, kujisaidia na kulala majalalani hii inathibitisha kuwa kazi nzuri ni siasa hata ukistaafu bado unaweza kupaa kwenda ughaibuni kuzurula lakini prof akistaaaf ukisikia yupo ughaibuni ujue ana drip ya maji au damu
 
Kuna uhusiano gani kwa maneno ya baba askofu kuhusu Kabudi na unayoyasema?
Nyoosha maelezo
Kwamba ukiwa na hali mbaya kiuchumi bhasi ndo ukubali kudharauliwa na kutukanwa ili mradi upate kula?? Sasa kama kabudi prof mstaafu anakubali kudhalilishwa hivi kisa tu kula wazee wengine ambao hawakusoma kabisa wafanyaje???
 
Aseme yote lakini hakuna pesa rahisi na tamu kama ya mazabauni.... siku akija huku mtaani kula kwa jasho atapunguza mdomo
 
Mambo mengine ni mpango wa Mungu. Unaweza kuwa mtumishi wa umma na una sifa zote na za ziada lkn teuzi zikipita wala hata kufikiriwa hufikiriwi. Hivyo, kuna bahati mtu kaandikiwa na Mungu.
 
Naona wachache sana wamemuelewa Baba Askofu..
Waziri Kabudi akisoma hii lazima ampigie simu Baba Askofu kumpa sikitiko lake..
Baba Askofu kapiga sehemu inayoumiza...kufafanua ni kufanya uchonganishi.
 
Ametumia falsafa kuwakilisha hoja
Mkuu hakuna cha falsafa wala nini,ukiwa msomi wa ngazi hiyo halafu unakana matamshi yako kuhusu muungano sawa na Dtk Mwakyembe kukataa bandiko lake wasomi wetu bado ni mtihani sana wengi wanaangalia mkate mezani tu.
 
Jf siyo home of great thinker tena, nina mashaka na baadhi ya wachangiaji au ni watoto wadogo, wameshindwa kabisa kuelewa andiko la askofu
 
Kuna wakati unaweza ukadhani unajitafutia heshima kwa watu. Kumbe unajidhalilisha.
Hakuna haja ya sisi kujua kuwa aliokotwa jalalani au alishuka moja kwa moja kutoka mbinguni.
kikubwa apunguze kujipendekeza kwa boss. Akifanya Kazi nzuri itaonekana TU.
 
Mtu mwenye mtazamo hasi juu yake mwenyewe hawezi kuwa kiongozi mzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…