Askofu atangaza kugombea ubunge 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu atangaza kugombea ubunge 2015

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Feb 16, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  ASKOFU Edson Mwombeki wa Kanisa la Tanzania Evangalism Field lililoko katika Manispaa ya Shinyanga, ameeleza nia ya kugombea ubunge ifikapo 2015 kwa madai kuwa wabunge walioko sasa hawana utukufu wa Mungu na nia ya kuwatumikia wananchi kwa upendo.

  Askofu Mwombeki alieleza nia hiyo kwa waumini wa kanisa hilo hivi karibuni bila ya kutaja ni chama gani atagombea na kuongeza kuwa yupo katika maombi ya kufunga siku 40. Hata hivyo alisema majimbo atakayowania kiti hicho cha ubunge ni kati ya Shinyanga Mjini na Kishapu.

  "Sasa mimi nimeamua kugombea naweka mambo hadharani, mbona wanaowania urais wanajitaja?” alihoji.

  Mwombeki alisema kuwa yuko katika mfungo wa siku arobaini na waumini wake na kuwataka wachungaji na maaskofu kuungana naye katika maombi hayo ili kuombea nchi neema.

  Alidai baadhi ya wabunge wa sasa hawataki kubadilika na baadhi ya viongozi wa Serikali wanataka urais na kupitapita katika jamii kujionesha.

  “Utabiri uliopo mwaka 2015 tunategemea Tanzania kupata rais mcha Mungu mfano wa Nabii Musa apigiwe kura au asipigiwe, hakuna mgombea atakayeingia madarakani kama hana ufalme wa Mungu,” alisema.

  Alisema kuna baadhi ya Watanzania wanamlaumu Rais Jakaya Kikwete badala ya kutatua changamoto zilizopo kwani yaliyo mazuri mengi yapo aliyoyafanya.

  Alifafanua kuwa nia yake ya kugombea sio mbaya kwa kuwa anaamini watu wanamhitaji kwani amekuwa nao bega kwa bega kwa majimbo yote mawili katika kuleta maendeleo kwa jamii ila chama atapewa na Mungu.

  HABARILEO
   
 2. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  Askofu wa makanisa ya kisanii!
   
 3. Mromboo

  Mromboo JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 728
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Aseme sadaksa imekuwa kidogo hivyo anatumia kigezo cha dini kuongeza POSHO. akadese kwa Lwakatare.
   
 4. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  mku futa kauli yako bwana,makanisa yote ni sawa tu cha muhimu ni kumwomba mungu tu
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Dini haichanganywi na siasa na waliochanganya kimojawapo kiliwashinda. Katika hili waumini wake wajue kuwa akishinda ubunge watakuwa wamemkosa kiongozi wao wa kiroho.
   
 6. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #6
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  wewe ndio ufute kauli yako! siasa na dini wapi na wapi!
   
 7. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Hivi kwanini tusibaki na kanisa katoliki pekee na uislamu iili adabu iwepo?
   
 8. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Nilijua Askofu wa Arusha aliyefulia!
   
 9. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Karibu CHADEMA chama cha Yesu!
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ama kweli pesa mbele,siasa imekua mtaji,

  haya kaungane na mama Lkwakateare na mch. Msigwa kukemea mapepo bungeni.
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,943
  Trophy Points: 280
  wewe kenge Yesu yupo kil sehemu sio chadema tu
   
 12. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkubwa!

  Humu ndani tuna watu mizigo na itabidi twende nao hivyo hivyo Mkubwa wangu!
   
 13. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0


  Baada ya kuchuna ngozi kondoo wa bwana here comes another opportunity ya KUJIONGEZEA MPUNGA - Range rovers sports bei imepanda nn?
   
 14. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,183
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Huyu hafai kuitwa askofu bila kuonyesha CV yake ya masomo ya kiroho,hivyo namshauri kabla ya kuufikiria ubunge basi aende akasomee daraja la uaskofu.kisha afikirie jinsi ya kuwaelimisha watu wake kiroho na kutambua jinsi ya kutumia haki yao ya kikatiba kupiga kura halali bila ya kuomba rushwa wagombea,,,,
   
 15. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #15
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Nadhani wewe upo mbari sana ktk maswala ya siasa na dini,kwani hata vitabu vya mungu vinanena kuwa viongozi ni chaguo la mungu,na viongozi wetu waliowengi wanapatikana ktk mkondo wa siasa,si hivyo tu hata kumchagua kiongozi wa kanisa kura hupigwa ili kumpata kiongozi huyo,sasa unatenganisha vipi siasa na dini?
   
 16. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #16
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ivuga
  kuna watu wao hawataki kubadirika hata uwape elimu ya namna gani,nacho elewa ni kwamba vyama vyote vya siasa hapa Tz vina wanachama na viongozi wa kada tofauti niki maanisha Dini tofauti.

  nakubaliana na wewe kumcha mungu ni mahala popote pale
   
 17. s

  sanjo JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Ni haki yake ya kiraia kuwania nafasi ya kuchaguliwa. Lakini, lazima aelezee atawafanyia nini kama mbunge wananchi wa jimbo la Kishapu au Shinyanga Mjini tofauti na wabunge waliopo (Mbunge Masele na Nchambi).
   
 18. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  huyo atakua mgombea wa CCM maana nimeunganisha dot... Nimeona kamfagili Baba MwanaAsha(JK).. Halafu na chanzo cha Habari ni lile gazeti la HABARILEO
   
 19. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,135
  Likes Received: 6,628
  Trophy Points: 280
  mwacheni akatafute hela ndegu,
  sadaka ameona siyo dili tena.
   
 20. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,703
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
Loading...