Askofu amkaanga Makinda

Askofu amkaanga Makinda

Jangakuu

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Posts
513
Reaction score
221
Naye askofu wa kanisa moja kubwa nchini ambaye aliomba kuhifadhiwa jina ili kuepusha malumbano, alisema kuwa Spika Makinda na Naibu wake, Job Ndugai, wanayumba na wanaliyumbisha Bunge.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu, askofu huyo alisema kuwa viongozi hao wawili wametumwa na wanatumika. Na kwamba wale waliowatuma wanaona kuwa wanafanya vizuri kwani ndilo hasa lengo.

Alisema ni juhudi za wabunge pekee, tena wenye maono ya kizalendo, ndizo zinaweza kuwaondoa madarakani kwani ni vibaraka.
"Ukimlinganisha huyu Spika na wenzake waliowahi kuongoza Bunge, huyu ni balaa. Amevaa itikadi zaidi Lakini tunatafsiri kuwa anatumika na Rais.

"Huwezi kuwa na Bunge imara kama una serikali dhaifu. Ndiyo maana katika nchi yetu sasa, mtu hawezi kuwa Spika kama Rais hajamkubali," alisema.

Alisema hayo tunaweza kujifunza kutokana na kauli ya Makinda ya hivi karibuni alipotoa maoni yake kwenye tume ya kukusanya maoni ya Katiba, pale aliposema kwamba anapendekeza Spika asitokane na chama cha siasa.

Hiyo ina maana anashinikizwa na chama chake kufanya mengi ambayo kama si shinikizo, asingeyafanya. Hata haya yanayotokea ni shinikizo la chama chake.

"Hali ni hiyohiyo hata katika mahakama. Serikali inaingilia sana uhuru wa mahakama. Ndiyo maana hata Jaji Mkuu alipotoa maoni yake katika Tume ya Marekebisho ya Katiba alisema angependa mahakama iwe huru.

"Maana yake anajua kuwa kwa sasa kuna shinikizo kutoka serikalini au chamani katika uendeshaji wa maamuzi ya mahakama nchini. Hii ni hatari," alisema.

Askofu alibainisha kuwa Makinda ni tofauti na Spika aliyepita Samuel Sitta; kwamba Sitta alikuwa na mwelekeo, alisimamia ukweli, japo mwelekeo wake haukupendwa na watawala.

Aliongeza kuwa Sitta alikuwa mpigania haki, mpenda mabadiliko na aliweza kuonyesha kuwa anawajali wanyonge. Hakuliyumbisha Bunge na aliweza kusimamia maamuzi.

"Bunge haliongozwi kitaasisi, bali linaongozwa kwa matashi ya mtu binafsi au kikundi cha watu.

"Sisi tunapaswa kuwa makini katika kuchagua watu wa aina hii na tunapaswa kuwaelimisha Watanzania ili wapambane kuondoa mfumo wa aina hii," alisema.

source: Tanzania daima
 
Naye askofu wa kanisa moja kubwa nchini ambaye aliomba kuhifadhiwa jina ili kuepusha malumbano, alisema kuwa Spika Makinda na Naibu wake, Job Ndugai, wanayumba na wanaliyumbisha Bunge.

source: Tanzania daima

Njia bora ya kuepusha malumbano ni kukaa kimya...
 
Kama hata askofu anaomba jina lihifadhiwe basi ujue hajiamii, maana yake hana tofauti na wanasiasa

keleb...
 
jamani nachukia sana matamko ya maaskofu nyie acheni tu,make hayana tija kwa jamii zaidi ya upotoshaji,kuna askofu 1 aliwahi kutaja hadharani kuwa Jk ni chaguo la mungu lakin badae aligeuka.
 
Mi habari bubu kama hizi huwa zinanikera tu, yaani tujadili jambo lililoongelewa gizani..too low
 
Hapa kosa sio la askofu ni upumbavu wa mwandishi na mhariri wake, kama mtu hataka kutaja jina kwa nini umpe prominence? inamaana hii ni habari ya kutungwa na wakina Ansbert ili kutengeneza story kwanza ni askofu gani Tanzania anayemuogopa rais na hivyo kuogopa kusema ukweli? maaskofu wanamuogopa mungu tu na ndio maana walitoa waraka na kumuuliza huyu bwana juu ya mfumo kristo kwenye serikali yenye asilimia 95 ya viongozi wakiwa waislamu na mpaka leo amefyawa mkia hajajibu, Tanzania Daima acheni usanii wenu mnaboa acheni uvivu nakufanya kazi zenu binafsi wakati na sehemu yakazi
 
jamani nachukia sana matamko ya maaskofu nyie acheni tu,make hayana tija kwa jamii zaidi ya upotoshaji,kuna askofu 1 aliwahi kutaja hadharani kuwa Jk ni chaguo la mungu lakin badae aligeuka.
Ni kweli Kikwete ni chaguo la Mungu ili watanzania mjifunze!!! Wala Askofu Kilaini hakukosea!!!
 
Uandishi wa aina hii ni usanii,inawezekana hata hakuna cha askofu ni hadithi ya kutunga tu,askofu wa ukweli hawezi kuficha Jina,hata kama kweli aliongea na kukataa kuficha Jina kwa mwandishi aliyebobea kwake isingekuwa habari angeitafutia sehemu ikawa kama makala,kama angeiona bado kwake ni muhimu kitu ambacho kwangu hakuna umuhimu sana kwa sababu maoni ya aina hii yameshatolewa sana na watu.
 
Na mimi naomba jina langu lihifadhiwe ila huenda akawa ni askofu wa pale kanisa karibu na bahari sokoine drive
 
ufalme wa mungu utatekwa na wenye nguvu.mungu hatumii watendakazi waoga.tanzania daima limekuwa gazeti la udaku
 
Kanisa kubwa lipi hizi habari zimetoka kwenye gazeti la udaku Tanzania Daima. Wanataka kuwachonganisha Askofu na Makinda.
 
Hapa kosa sio la askofu ni upumbavu wa mwandishi na mhariri wake, kama mtu hataka kutaja jina kwa nini umpe prominence? inamaana hii ni habari ya kutungwa na wakina Ansbert ili kutengeneza story kwanza ni askofu gani Tanzania anayemuogopa rais na hivyo kuogopa kusema ukweli? maaskofu wanamuogopa mungu tu na ndio maana walitoa waraka na kumuuliza huyu bwana juu ya mfumo kristo kwenye serikali yenye asilimia 95 ya viongozi wakiwa waislamu na mpaka leo amefyawa mkia hajajibu, Tanzania Daima acheni usanii wenu mnaboa acheni uvivu nakufanya kazi zenu binafsi wakati na sehemu yakazi

Jomba naona umeamua kula sumu kwa sababu tu umesikia harufu ya ARKI!
Hivi wewe na hao Maaskofu wako munaposema zaidi ya 95 Viongozi wa Serikali ni Waislamu hua munakusudia nini? Mimi ninavyofahamu Serikali haikamiliki kwa Raisi, Spika, Makamo wa Raisi, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu, IGP na au Mkuu wa Majeshi peke yao bali uongozi wa Serikali unajumuisha Mawaziri, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, Gavana wa Benki kuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya na wengineo.
Ili wewe na Maaskofu wako muniridhishe hemu nambieni katika hao Waislamu ni wangapi na wasiokua Waislamu ni wangapi?? Musiishie kutoa takwimu za 95% bali mungetenda haki zaidi iwapo mutatupa orodha ya uwiano wa idadi katika kila taasisi ya serikali! Binafsi TAMKO lile la Maaskofu limeliona ni KITUKO cha mwaka.
 
jamani nachukia sana matamko ya maaskofu nyie acheni tu,make hayana tija kwa jamii zaidi ya upotoshaji,kuna askofu 1 aliwahi kutaja hadharani kuwa Jk ni chaguo la mungu lakin badae aligeuka.

hivi hawajifunzi toka kwa pengo alieachana na matamko ya kisiasa.
 
Ili gazeti toka liandike Tyson kawa mwanamke siku nalinunua nafunguia pweza au ngisi.
 
Back
Top Bottom