Askari wetu wanapewa mzigo mzito kuelekea Uchaguzi Mkuu

Nimeulizia anaye takiwa kutoa taarifa tume ni nani?

Magu kampeni zake anaanza saa 06:00 nakumaliza saa 16:45

Halafu kumbuka JEMEDARI NDO YEYE.
Atasema kwingine alikuwa anahutubia kama jemedari, kampeni kamaliza 17:54hrs.

Kwanini uulizie hicho kitu kidogo cha muda wakati Magufuli amesema kabisa kwamba wananchi wakichagua mpinzani hataendeleza hilo eneo na akatolea mfano ambavyo hakutaka barabara ya lami ijengwe bunda sababu walimchagua mpinzani hivi hayo makosa ni sawa na mtu aliyechelewa kumaliza mkutano.
 
Kwani kanuni na maadili yanasemaje?

Mimi naamini kila mdau wa uchaguzi kwa maana ya wagombea, NEC, Polisi, wapiga kura na wengineo kila mmoja ana wajibu wake wa kikanuni...

Kwa swali lako hili la nani atoe taarifa, jibu lake ni;

Hawezi kuwa Polisi bali ni yule anayedhani ameathiriwa na kuvunjwa kwa kanuni fulani. Polisi kutaka kumshusha mgombea alikuwa anataka kufanya jukumu lisilo lake...

HEBU SOMA HII;

Kuna sehemu moja huku Shinyanga mgombea ubunge wa CCM wa jimbo fulani alikuwa anazindua kampeni zake jana J'5 trh 16/9/2020...

Jana yake gari la matangazo kwa nyakati tofauti tofauti lilipita mitaani kuutangaza mkutano huo....

Mpaka saa 5 usiku lilikuwa linapita mtaa moja baada ya mwingine likitangaza na kesho yake kuamkia J'5 tangazo la mkutano likatangazwa kwa kutumia vipaza sauti vya misikiti karibu yote ya mji ule ile mida ya swala ya asubuhi ya saa 11 alfajiri...

Kumbe kwenye kanuni imeelezwa mpaka muda unaoruhusiwa kikanuni kutangaza mikutano ya kampeni kwa kutumia vipaza sauti....

Kanuni inasema kuwa kwa jioni mwisho ni saa 2usiku na kwa asubuhi ni kuanzia saa 1 ASB....

Kwa hiyo mgombea huyu wa CCM akawa amevunja kanuni na maadili ya uchaguzi wa 2020....!!

Kesho yake haraka haraka na mapema kabisa vyama vya CHADEMA, ACT na vingine vikafikisha malalamiko kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo wakimtaka amchukulie hatua za kisheria mgombea huyu wa CCM....

Haijulikani hatua gani zilichukuliwa....

Pointi hapa ni kuwa, kuhusu masuala kama haya ya uchaguzi, sio Polisi wanaopaswa kulalamika kama kanuni fulani inavunjwa na mgombea fulani isipokuwa wagombea wa upande mwingine ndiye anaweza kulalamika...!

Mwalimu mgombea mwenza wa Urais wa CHADEMA, yuko sahihi. Polisi hana mamlaka kumshusha mgombea fulani kwa kigezo cha kuzidisha muda....

Kama kuna mgombea ameathiriwa na hilo, aende akalalamike kwa tume ili wachukue hatua kama wataweza...!!
Uko sahihi. Na, asipochukuliwa hatua sasa ikatokea ameshinda, hiyo tiyari ni sababu mojawapo ya kupinga ushindi.
 
Wewe unafikiria kama Magufuli akizidisha muda kuna askari wa kumshusha jukwaani kwa kuzidisha muda? Kwa nini kuwe na upendeleo?
.
tapatalk_jpeg_1588860003675.jpg
 
Back
Top Bottom