Maeneo ya Buguruni askari wa JWTZ 3 wametwangana na askari magereza
Walianza kurushiana maneno kati ya wale wanajeshi 3 na askari magereza mmoja ndipo wakaanza kurushiana makonde baada ya askari magereza kuona anataka kuzidiwa akapiga simu ndipo baada ya muda mfupi wakatokea majamaa wawili wamevaa T-shirt za kijani nadhani za magereza,,,duh!!
Sikiuamini kama magereza wanajiamini vile kiufupi wameonesha umahiri,wamewachapa wale mabaka baka hadi mmoja nadhani jicho litakuwa limetolewa maana linaonekana kama limechanwa kabisa.
Wametokea traffic wameamua ugomvi na kumchukua mwanajeshi majeruhi hospitality nadhani
Nimesikitika kwanini askari wetu wadhalilishane mbele za RAIA?? Vijana wa kileo wanaoajiliwa maadili hakuna