Askari watwangana hadharani

Askari watwangana hadharani

Mwaka 2016 nilikutana na kombania ya askari magereza mjini moshi,walikuwa katika mazoezi ya kutembea km 12.Kwa ajili ya kujiandaa kupanda mlima Kilimanjaro.Walikuwa wako hoi nikapata wasaa wa kuzungumza na afisa kiongozi wao mwenyenye cheo cha ASP(nyota tatu).Katika mazungumzo yetu akanidokeza kuwa hawajawahi kutembea mwendo mrefu kiasi kile,nilishangaa sana.
Wakati kwenye mafunzo ya awali jeshini kutembea (route march) km 40 ni kawaida sana.
Sasa nashangaa wanaosema askari wa jeshi la ulinzi ambaye anafundishwa kuvuka vikwazo anapokuwa vitani eti hana utimamu wa mwili kama askari wa FFU au Magereza.
Mh!! Kuna kipindi nilikuwa mbeya Chuo cha mag nakijua kilipo,kipo bondeni kando ya MTO kiwira nadhani jamaa wanasafiri mwendo mrefu xana kwa mguu,,walikuwa wakipita maeneo ya KK SAA 1 jioni hadi kesho yake asubuhi ndo tunawaona wanarudi tokea Tukuyu na bunduki zao,,,Kiwira- tukuyu km 112 hazipungui kwhy swala la ukakamavu nadhani wako vzr mno
 
Km 112 ni umbali wa Mbeya -Kyela(Km 110)
Kiwira -Tukuyu ni km 18.
 
Maeneo ya Buguruni askari wa JWTZ 3 wametwangana na askari magereza

Walianza kurushiana maneno kati ya wale wanajeshi 3 na askari magereza mmoja ndipo wakaanza kurushiana makonde baada ya askari magereza kuona anataka kuzidiwa akapiga simu ndipo baada ya muda mfupi wakatokea majamaa wawili wamevaa T-shirt za kijani nadhani za magereza,,,duh!!

Sikiuamini kama magereza wanajiamini vile kiufupi wameonesha umahiri,wamewachapa wale mabaka baka hadi mmoja nadhani jicho litakuwa limetolewa maana linaonekana kama limechanwa kabisa.

Wametokea traffic wameamua ugomvi na kumchukua mwanajeshi majeruhi hospitality nadhani

Nimesikitika kwanini askari wetu wadhalilishane mbele za RAIA?? Vijana wa kileo wanaoajiliwa maadili hakuna

Ingekuwa mkoani huku kama Arusha hivi watu tungekuwa tunasubiri CD ya pili ya hiyo movie
 
Katika haya majeshi huwa kuna mafunzo ya kawaida ya kijeshi ambayo yanampa ajira mhusika na baada ya hapo kuna mafunzo ya ziada ta kumuongezea mhusika flani.mwanajeshi awe jw,magereza au polisi wa ffu aliyepata mafunzo maalum ya ziada hawezi kulingana kiuwezo na yule aliyepata Yale ya kawaida ya kumpa hiyo ajira.hivyo magereza aliyepata mafunzo maalum ya ujuzi wa mapigano huwezi kumlinganisha na jw aliyepata mafunzo ya kawaida sababu huyu magereza amebobea ktk shughur hiyo na anafanya mazoez ya Mara kwa Mara,jw pia wako wanajeshi wanaopewa mafunzo maalum ya kimapigano ya ziada hawa ndio wanaitwa makomando nao ni moto wa kuotea mbali na ni mahiri zaidi ya hao wa magereza au ffu sababu hawa wanapikwa kwa uweredi wa kupambana hata na magaidi ila sio rahisi kuwakuta mitaani au kuwajua.kwahyo msishangae hao jwtz kupigwa na hao magereza walioitwa sababu aliyewaita alijua hao ni kikosi maalum ambacho ni mahiri kwa mapigano na hao wakikutana na mwanajeshi wa kawaida lazima watamzidi tu sababu wana mafunzo ya ziada kwa shughuri hiyo.ni sawa na we we raia utake kupigana na bondia mtaani kwa asilimia kubwa utapigwa sababu mwenzako kupigana ni shughur yake rasmi na anaifanyia mazoezi ya mara kwa Mara.kwahyo sio jambo la ajabu lililoshuhudiwa maana mwanajeshi wa kawaida training zake zinabase hasa ktk matumizi ya bunduki na mbinu za kivita na mambo ya ngumi na karate kiasi tu ili asiwe boya jumla,lakini magereza hao walioitwa ni kikosi maalum cha kupigana ili kuzuia vurugu magerezani so wana mafunzo ya ziada na mazoezi ya ziada ktk kupigana.
File wengi nidhamu ndogo
 
Acha kuchezea FFU mjomba,embu tembelea Ukonga pale ujionee.Wale jamaa siyo watu wazuri wapo wengine walienda Jordan na Marekani kupata mafunzo ya juu.Mafunzo hayo(madini) ndio wanawalisha FFU wote nchini.
Mzee acha kuongopea mm nimeishi ukonga acha kufananisha magereza kikosi maalumu (k m) na f f u
 
Mzee acha kuongopea mm nimeishi ukonga acha kufananisha magereza kikosi maalumu (k m) na f f u
'Km' ni maboya tu usifananishe na hao jamaa 'km' wanachojua wao nikujifunza kurusha ngumi tu hakuna cha zaidi,sasa kurusha ngumi hata sisi raia wa kawaida tunaweza.Madini ya ffu(tactics) wameyapatia Jordan ila 'km' madini yao ni ya hapa hapa(Bongo).Ffu ipo juu milele.!!
Unachofanya hapa nikufananisha komando aliyechukua mafunzo ya ukomandoo nchini China na yule aliyepata mafunzo bongo(Ngerengere).
 
Mkuu fika pale km garden uwanjani asubuhi uwone km wanavyo fundishwa na wachina na wakorea alafu nenda kule f f u juu Mombasa near mzambarauni utajua nani mkali aise pale km zamani palikuwa na nyumba kambi za wanajeshi (makomando) f f uu juu kule ni kulenga shaba tu
N:B kikosi maalamu km wakiwa mafunzoni si ruhusa raia au mtu ambae simuhusika kusogea eneo LA mazeozi
 
Back
Top Bottom