askari waporwa risasi 60 na bunduki 2


P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
39,844
Likes
8,663
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
39,844 8,663 280
MAJAMBAZI wamewapora polisi bunduki mbili aina ya SMG, risasi 60 na kuwajeruhi mjini Songea.

Askari hao wamelazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma mjini Songea,hali zao bado si nzuri.

Polisi hao waliporwa silaha,jana saa 11.30 alfajiri katika njia ya Mpate, Mtaa wa CCM, wakati askari hao wakitoka lindoni.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda, amesema jana kuwa, askari walioporwa bunduki hizo walijeruhiwa na kulazwa na mwingine hadi jana alasiri alikuwa akifanyiwa upasuaji.

Aliwataja askari hao kuwa ni Konstebo Rajabu na Konstebo Joel Gwamaka ambao walizidiwa nguvu na majambazi hao waliowavamia ghafla na kuwashambulia.

"Askari aliyejeruhiwa zaidi kwa kupigwa kichwani na kitu kizito ni Rajabu na huku Gwamaka akipigwa risasi pajani katika purukushani hiyo," amesema Kamuhanda.

Kamanda alisema askari hao walivamiwa na kundi la majambazi wasiojulikana idadi na kwamba Polisi mkoani hapa inaendesha msako kwa kushirikiana na wananchi.

"Bado hatujakamata mtu kuhusu tukio hili, msako unaendelea kijiji hadi kijiji, nyumba hadi nyumba pia pori hadi pori," alifafanua Kamuhanda na kuongeza kuwa mikoa yote imejulishwa tukio hilo.

Aidha, Polisi hapa ikishirikiana na makao makuu yake Dar es Salaam, imeahidi zawadi ya Sh milioni 5 kwa atakayetoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa majambazi hao.
 
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
4,134
Likes
73
Points
145
Mpaka Kieleweke

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
4,134 73 145
SMG 2 Risasi 60zilikuwa za kazi gani?

Ama walikuwa wanaenda vitani?
 

Forum statistics

Threads 1,235,149
Members 474,353
Posts 29,213,277