Askari, wananchiwawili wakabiliwashtaka launyang'anyi Sh78.6milioni

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Dar es Salaam. Serikali inatarajia kuita mashahidi 12 na vielelezo vitano katika kesi ya unyang'anyi wa
kutumia nguvu na kujipatia Sh78.6 milioni, inayowakabili washtakiwa watatu akiwemo askari Polisi.

Hatua hiyo inatokana na upelelezi wa kesi hiyo ya jinai namba 173/2023 kukamilika katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu. Washtakiwa katika kesi hiyo ni Nassoro Mkono (32) maarufu kama Samson, dereva na mkazi wa Mbezi Kimara, Sia Tarimo (26) mkazi wa Ukonga na askari Polisi mwenye namba F 5867 Koplo Khamis (40).

Kwa pamoja washtakiwa hao wanadaiwa kufanya unyang'anyi wa kutumia silaha na kujipatia Sh78.6
milioni, mali ya Zawia Shabani, ambapo kabla ya kujipatia fedha hizo, walitumia nguvu na kumtishia
ili waweze kujipatia fedha hizo bila kikwazo.

Wakili Serikali, Judith Kyamba ameieleza mahakama hiyo leo, Oktoba 26, 2023, Mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Amiri Msumi, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa hoja za awali.

Akiwasomea maelezo yao, wakili Kyamba alidai kuwa Mei Mosi, 2022 katika eneo la Karakata, Ukonga mkoani Dar es Salaanm mshtakiwa wa tatu (Koplo Khamis) akiwa pamoja na watu wengine wawili akiwemo
mshtakiwa namba moja(Mkono), walifika kwa mlalamikaji Zawia Shabani na kujitambulisha kuwa ni askari polisi.

Baada ya utambulisho, Koplo Khamis na wenzake walimuweka Zawia na ndugu zake Amina Shabani, Mariam Salum na mshtakiwa namba mbili (Sia) chini ya ulinzi na kuwaamrisha wakabidhi simu zao na kutopiga kelele kisha wakawatoa nje watoto wawili waliokuwa ndani.

Kyamba aliendelea kudai kuwa, mshtakiwa namba tatu (Koplo Khamisi) na wenzake walimfahamisha mlalamikaji kuwa wanahitaji kufanya upekuzi ndani ya nyumba na kuwa angepewa taarifa wanahitaji kufanya upekuzi ndani yanyumba na kuwa angepewa taarifa ya kinachopelelezwa baadaye, hivyo walianza upekuzi kwa kuingia chumbani kwa Zawia ambako alikuwemo mshtakiwa namba mbili (Sia) na kukuta fedha kiasi Sh8,000,000.Baada ya hapo, mshtakiwa wa pili alitoka nje na kuonana na waliojitambulisha kuwa ni polisi na
kurudi chumbani kisha akapekua begi la mlalamikaji ambapo alikuta Sh70,600,000.

Baada ya kukuta fedha hizo walimfokea mlalamikaji kuwa ni mwizi na kuziweka fedha hizo kwenye mfuko mweupe angavu na kumwambia mlalamikaji awafuate kituo cha polisi Staki Shari kisha wakaingia ndani ya gari na kuondoka.

Mlalamikaji akiongozana na ndugu yake Amina walifika Kituo cha Stakishari ambapo ilibainika kuwa hakukuwa na askari yeyote aliyetumwa kwake kufanya upekuzi wala hakukuwa na mtu aliyefika hapo na fedha hizo, ndipo
alipogundua kuwa ameibiwa, baadaye polisi walichukua maelezo na jalada la kesi likafunguliwa.

Januari 18, 2023, mshtakiwa nambamoja (Mkono) alikamatwa na katikamahojiano alikiri kushirikiana namshtakiwa namba mbili (Sia) ambaye alikuwa msaidizi wa kazi zandani wa mlalamikaji ambayealifahamu zinapohifadhiwa fedhahizo na aliwatafuta mshtakiwanamba tatu (Koplo Khamis) na mtumwingine aitwaye Baraka na kuwapataarifa za kuwepo fedha hizo nakupanga njama za kumuibia mlalamikaji bila yeye kuwepo."Mshtakiwa namba moja (Mkono)pia alikiri kupokea Sh5,000,000 kamamgao wake baada ya tukio hilo naalipokamatwa mshtakiwa nambambili (Sia) alikiri kushirikiana namshtakiwa namba moja," amedaiwakili Kyamba.

Kyamba aliendelea kudai kuwaJanuari 26, 2023 katika Kituo Kikuucha Polisi (Central), Jeshi la Polisililifanyika gwaride la utambuziambapo mlalamikaji alifanikiwakumtambua mnshtakiwa namba tatu(Koplo Khamis) kama mmoja wawaliofika kwake siku ya tukio nakumpora fedha zake.

Aliendelea kudai kuwa Septemba 21,2023 washtakiwa wote watatuwalifikishwa mahakamani nakusomewa shtaka moja yaunyang'anyi wa kutumia nguvu nakujipatia Sh78 milioni.

Upande wa mashtaka baada yakuwasomea maelezo yao,washtakiwa waliakana maelezo hayona kukubali majina yao na sikuwalipofikishwa mahakamani hapo. Hakimu Msumi, baada ya kusikilizamaelezo hayo, aliahirisha kesi hiyohadi Novemba 9, 2023 itakapoitwakwa ajili ya usikilizwaji wamashahidi.

Kesi hiyo inatarajiwa kurudi tenaNovemba 9, 2023 kwa ajili yakusikilizwa.
 
Back
Top Bottom