Askari wa wanyamapori waua mtu Bukombe

Askari wa wanyamapori waua mtu Bukombe

Mshumaaa

Senior Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
156
Reaction score
17
Jamaa ni Fundi seremala alikuwa na vijana wake wanamchania mbao porini.

Askari waliwakuta vijana wakiendelea na kazi waliwapiga sana na baadaye kuamuru wale vijana wampigie simu bosi wao. Alipofika alipokewa kwa kipigo hadi kupoteza fahamu na baadaye wamempeleka Hospitali akafia huko.

Kwenye maelezo yao wanasema baada ya kufika kwenye eneo la tukio alianguka mwenyewe Kwa kupooza ghafla kitu ambacho hakiingii akilini hata kidogo.
 
Siku hizi bora ukutane na simba kuriko binadamu!! R.I.P Fundi.
 
Jamaa ni Fundi seremala alikuwa na vijana wake wanamchania mbao porini.

Askari waliwakuta vijana wakiendelea na kazi waliwapiga sana na baadaye kuamuru wale vijana wampigie simu bosi wao. Alipofika alipokewa kwa kipigo hadi kupoteza fahamu na baadaye wamempeleka Hospitali akafia huko.

Kwenye maelezo yao wanasema baada ya kufika kwenye eneo la tukio alianguka mwenyewe Kwa kupooza ghafla kitu ambacho hakiingii akilini hata kidogo.

Na hii nayo watasema Kagasheki
 
Bukombe-(ushirombo ) geme wa bukombe wahuni fulani hivi niliwahi kuwashuhudia siku moja wakikusanya mbao kutoka kwa mafundi selemara! Karibu na sheli ya rupirya.
 
Jamaa ni Fundi seremala alikuwa na vijana wake wanamchania mbao porini.

Askari waliwakuta vijana wakiendelea na kazi waliwapiga sana na baadaye kuamuru wale vijana wampigie simu bosi wao. Alipofika alipokewa kwa kipigo hadi kupoteza fahamu na baadaye wamempeleka Hospitali akafia huko.

Kwenye maelezo yao wanasema baada ya kufika kwenye eneo la tukio alianguka mwenyewe Kwa kupooza ghafla kitu ambacho hakiingii akilini hata kidogo.

postmortem itajibu maswali yote
 
Askari hana mamlaka ya kuua na pia Fundi hana ruhusa ya kuchana Mbao kwenye hifadhi. Askari alijichukulia Sheria na Fundi naye madaraka.
 
Askari hana mamlaka ya kuua na pia Fundi hana ruhusa ya kuchana Mbao kwenye hifadhi. Askari alijichukulia Sheria na Fundi naye madaraka. Ni sawa na sababu na matokeo. Ni vizuri kutii bila shuruti. Askari nanyi msitafute sifa za kijinga
 
Tatizo watu wenye hasira ni wale wenye njaa kali , kwanini ukose ubinadamu hadi umtoe roho mwenzako. RIP FUNDI.
 
Acheni uzushi; wanachana mbao kwenye national reserve? Hao ni majangili wanaojihami kwa kutoa sabau zisizokuwa na msingi, majangili waache wapigwe tu!!
 
Jamaa ni Fundi seremala alikuwa na vijana wake wanamchania mbao porini.

Askari waliwakuta vijana wakiendelea na kazi waliwapiga sana na baadaye kuamuru wale vijana wampigie simu bosi wao. Alipofika alipokewa kwa kipigo hadi kupoteza fahamu na baadaye wamempeleka Hospitali akafia huko.

Kwenye maelezo yao wanasema baada ya kufika kwenye eneo la tukio alianguka mwenyewe Kwa kupooza ghafla kitu ambacho hakiingii akilini hata kidogo.

Tusiwalaumu Sana Kwani Yawezekana Aliyeuwawa Nae Alikuwa Anafanana Na Wanyama Kama Tembo Na Faru Hivyo Wakajua Labda Angeharibu Mazingira. Usisahau Binadamu Wengine Hatuna Tofauti Na Wanyama Wa Mbugani Kimwonekano Hivyo Inawawia Vigumu WATOTO Wa Nyalandu Kutambua Kiurahisi Lakini Wakishakupiga Tu Risasi Ya M.A.T.A.K.O Na Wewe Ukilia Ndipo Wanajua Kuwa Kumbe Haukuwa Mnyama Bali Ni Binadamu Mwenzao. Pole Yake Huyo Aliyeuwawa.
 
jamani wazima humu?labda tu napenda ieleweke kua si kila afisa maliasili ni afisa wanyamapori.sasa kwa jinsi nimeona hiyo taarifa (ingawa sifahamu undani wake) labda nitumie fursa hii tueleweshane juu ya tofauti ya kiutendaji kati ya idara ya wanyamapori na mamlaka ya huduma za misitu na ofisi ya maliasili na utalii katika halmashauri zetu.
1.idara ya wanyamapori
hii ni idara inayosimamia mapori yote ya akiba yaliyopo nchini ikiwa inatimiza majukumu yake chini ya sheria ya wanyamapori yaani wildlife conservation act no.9 of 2009.hiki ndo chombo kikuu cha usimamizi kilichopo cjhini ya serikali kuu (central government),sasa unapoona mtumishi anafanya kazi akiwa na kombati ndani ya pori lolote la akiba basi anajlikali kama ASKARI WA WANYAMAPORI.
2.huduma ya misitu tanzania(Tanzania Forestry Services Agency)
hii ilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya uwakala cap.245 revised edition 2009),national forest and beekeeping policies adopted on march 1998 lakini ikawa administered kupitia sheria ya misitu no14 ya 2002 na sheria ya ufugaji nyuki no15 ya 2002.hawa wamepewa majukumu mengi lakini kati ya hayo ni pamoja kulinda hifadhi za misitu yetu yote.
NOTE
Askari wanyamapori kwa upande huu nahisi hawahusiki kwa mujibu wa majukumu ambayo kimsingi yanaainishwa na kutofautishwa na sheria hizo nlizozitaja,kwahvo nlikua najaribu kutoa angalizo tu kwa wanaotuma wajaribu kufatilia mambo kwa kina kabla ya kulaumu upande ambao kwa namna moja au nyingine unaweza ukawa offended na kutojua kwa mtoa habari ambae pengine kwa kua aliona mtu amevaa nguo zinazofanana na kada fulani basi aka conclude.ieleweke sijasema kwa ubaya lakini ni katika kuelimishana na pia niwape pole kwa hao waliopatwa na maswahibu haya.
 
jamani wazima humu?labda tu napenda ieleweke kua si kila afisa maliasili ni afisa wanyamapori.sasa kwa jinsi nimeona hiyo taarifa (ingawa sifahamu undani wake) labda nitumie fursa hii tueleweshane juu ya tofauti ya kiutendaji kati ya idara ya wanyamapori na mamlaka ya uwakala wa huduma za misitu.

1.idara ya wanyamapori
hii ni idara inayosimamia mapori yote ya akiba yaliyopo nchini ikiwa inatimiza majukumu yake chini ya sheria ya wanyamapori yaani wildlife conservation act no.9 of 2009.hiki ndo chombo kikuu cha usimamizi kilichopo chini ya serikali kuu (central government),sasa unapoona mtumishi anafanya kazi akiwa na kombati ndani ya pori lolote la akiba basi anajulikana kama afisa wanyamapori au ASKARI WA WANYAMAPORI .

2.huduma ya misitu tanzania(Tanzania Forestry Services Agency)
hii ilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya uwakala (cap.245 revised edition 2009),national forest and beekeeping policies adopted on march 1998 lakini ikawa administered kupitia sheria ya misitu no14 ya 2002 na sheria ya ufugaji nyuki no15 ya 2002.hawa wamepewa majukumu mengi lakini kati ya hayo ni pamoja kulinda hifadhi za misitu yetu yote.

NOTE
Askari wanyamapori kwa upande huu nahisi hawahusiki kwa mujibu wa majukumu ambayo kimsingi yanaainishwa na kutofautishwa na sheria hizo nlizozitaja,badala yake ni maafisa misitu ambao wanafanya doria kushirikiana na maafisa maliasili wa halmashauri waliopo katika halmashauri husika kufanya doria katika sehemu zote zenye mazao ya misitu iwe misitu ya hifadhi au misitu ya wazi.

Kwahvo nlikua najaribu kutoa angalizo tu kwa wanaotuma taarifa kama ya "MSHUMAA" wajaribu kufatilia mambo kwa kina kabla ya kulaumu upande ambao kwa namna moja au nyingine unaweza ukawa offended pasipo kujua kwa mtoa habari ambae pengine kwa kua aliona mtu amevaa nguo zinazofanana na kada fulani basi aka conclude.ieleweke sijasema kwa ubaya lakini ni katika kuelimishana na pia niwape pole kwa hao waliopatwa na maswahibu haya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom