Askari wa usalama barabarani sasa wanakusanya mapato na si kuangalia usalama

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
892
1,709
Inakera na inaudhi kuwa wengi barabarani na kila mmoja ana EFD mashine haisaidii kujenga nidhamu. Nguvu mnayotumia kukusanya mapato kushindana na TRA haisaidiii kuweka nidhamu barabarani.

Baadhi ya sehem mmekuwa chanzo cha kero kwa kusababisha foleni zisizo za lazima na sehemu zingine mmesababisha ajali kwa sababu tu mnajisikia kusimama popote na kusimamisha gari mnalotaka.

Hebu tumieni zile ethics mnazofundishwa darasani na chuoni jamani nchi haiendi hivi. Hebu mjipange jamani sidhani kukusanya pesa kwenu ni sifa bali sifa iwe nidhamu barabarani na ajali kupungua sio mnakuwa chanzo cha kero.
 
Wamepangiwa hesabu mkuu... Wameambiwa wanyonye kadri kubwa iwezekanavyo! Unaposikia mapato TRA yameongezeka ulifikiri pesa inatoka wapi? Kwenye biznes? Huoni frem, godowns na maofisi mengi sikuhizi yako tupu? Hali ni mbaya sana Mkuu.

[HASHTAG]#vyetimubashara[/HASHTAG]
 
I agree mkuu, hivi waziri wa hawa jamaa ni nani? Sidhani kama anaona hili tatizo?! Njia za mbeach adi tegeta ndio wamejaa foleni haziendi hawavuti magari wanaangaika kutafuta makosa kwa madereva, hawa traffic wamekua Kero mno
 
ukimchukua kichwa maji ukamkabidhi ferrari, huchelewi kumkuta anaivuta na mkokoteni.

Ability is nothing without control.

Serikali yetu ina tools lakini inazi-misuse.

Ni ujinga ulioptiliza kwa jeshi la polisi kutumia nguvu inazotumia kuongeza mapato, wakati kuna vingi vya kufanya kwenye usalama, havifanyiki.

A generation later this phase will be painted as the most pathetic our police force has ever been through. Grand kids read about this and wonder what kind of toxic liquor our force was using to have such a twisted mindset.
 
ukiona ripoti ya BOT inaonyesha mapato yasiyo ya kodi tu ndiyo yaliokusanywa kwa kuvuka malengo, ujue watu wameajirwa ili wakusanye mapato tu na sio kusimamia maswala ya usalama. mkikutanisha macho ukiwa umenuna, anakupiga faini.
 
Inakera na inaudhi kua wengi barabarani na kila mmoja ana efd mashine haisaidii kujenga nidham,nguvu mnayotumia kukusanya mapato kushindana na TRA haisaidiii kuweka nidham barabarani,baadhi ya sehem mmekua chanzo cha kero kwa kusababisha foleni zisizo za lazima na sehem zingine mmesababisha ajali kwa sababu tu mnajisikia kusimama popote na kusimamisha gari mnalotaka guys hebu tumieni zile ethics mnazofundishwa darasani na chuoni jamani nchi haiendi hivi kila mtu anaibuka tu na kua kama bashite , hebu mjipange jamani sidhani kukusanya pesa kwenu ni sifa bali sifa iwe nidhamu barabarani na ajali kupungua sio mnakua chanzo cha kero.

Mimi wakinisimamisha wanakagua na baadae kunitakia safari njema. Kwa nini inakuwa hivi? Kwa sababu gari yangu ipo vizuri na huduma zote inapata; halafu na mimi mwenyewe ninajitahidi kufuata sheria za barabarani.

Sasa wakianza kuangalia kama magari yetu yanafanyiwa service kwa ajili ya roadworthiness si wengi wataumia ingawaje sticker za car service zitapata soko sana (forgery).
 
Na siku mgomo wa madereva ukitokea nchini kwa siku nne mfululizo, nchi lazima iyumbe kabisa kimapato, hata watumishi wanaweza wasipate mishahara mwisho wa mwezi. Maana imekuwa kero sasa.
 
Kuna askari wanasimamia sheria na hawakutozi faini kama huna kosa, Ila kuna wachache wanakubambia makosa hawa sijui tuwafanyaje utakuta askari anakupiga torchi kabla ya 50 au hakuoneshi gari yako kwenye kamera unaona kivuli analazimisha faini.Tangu wanibambikie kosa sina urafiki na trafic kabisa tofauti na awali niliwapenda kwa kutimiza majukumu.
 
Wabongo mbona ninyi walalamishi kila siku. Nchi inahitaji mapato! Kama unaona shida kuchangia pato la taifa kwa faini ya kosa la barabarani, basi uza hicho kigari chako mtumba utembee kwa mguu au upande daladala/bodaboda.
 
Inakera na inaudhi kuwa wengi barabarani na kila mmoja ana EFD mashine haisaidii kujenga nidhamu. Nguvu mnayotumia kukusanya mapato kushindana na TRA haisaidiii kuweka nidhamu barabarani.

Baadhi ya sehem mmekuwa chanzo cha kero kwa kusababisha foleni zisizo za lazima na sehemu zingine mmesababisha ajali kwa sababu tu mnajisikia kusimama popote na kusimamisha gari mnalotaka.

Hebu tumieni zile ethics mnazofundishwa darasani na chuoni jamani nchi haiendi hivi. Hebu mjipange jamani sidhani kukusanya pesa kwenu ni sifa bali sifa iwe nidhamu barabarani na ajali kupungua sio mnakuwa chanzo cha kero.

Wananshindwa nini kuiga nchi zilizoendelea ili kuondoa kero kwa watumiaji wa barabara, sijui tutabadilika lini,
 
Labda sasa ingefaa rasmi kitengo cha Traffic kihamishwe kutoka Polisi kihamie TRA.
Wanaimudu vyema kazi ya kukusanya mapato kuliko nyingine za kipolisi.
 
mm nilichangia hapa kuwa jamaa wanajisikia raha sana wanapokaa kwenye media na kutangaza mapato yao ya mwezi itabidi tuanze kuwaita Police Revenue authority
 
Wabongo mbona ninyi walalamishi kila siku. Nchi inahitaji mapato! Kama unaona shida kuchangia pato la taifa kwa faini ya kosa la barabarani, basi uza hicho kigari chako mtumba utembee kwa mguu au upande daladala/bodaboda.
Mkuu inawezekana wewe ni mmoja wao au hujawahi fanyiwa mambo ya hovyo au kutozwa faini isiyo na sababu za msingi. Mimi walivyonibambikia kosa ndio siku hiyo niliwachukia kwa kweli, maana mtu unaweza lipa fine kwa sababu unawahi mambo yenye umuhimu zaidi na si kwamba umekubali kosa, jiulize kama kila kitu kuna fake yake unadhani hawa jamaa hawabambiki makosa fake.
 
Hajui alisemalo huyo jamaa
 
Back
Top Bottom