Askari wa usalama barabarani Maili Moja,Kibaha

Askari wa usalama barabarani Maili Moja,Kibaha

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,056
Reaction score
10,729
Wakuu nimekuwa msafiri wa mara nyingi hasa nikitokea Dar kwenda Mikoani.

Mara ZOTE tunapofika Kibaha huwa naona makondakta wanashuka na kadi ya TLB ikiwa wameifinya na kati ya Shs 1000 hadi 5000 na kuwapa askari.

Askari huzugazuga kuwa wanasoma kadi hizo na kukagua gari ilihali wakisunda fedha mifukoni.

Aidha miaka ya nyuma palikuwapo na banda la mbao hapo hapo stendi ambalo lililazimika kuondolewa kwa kuhusika sana na rushwa, hali ambayo nadhani haijakoma.

Najiuliza sana, Pesa hizo ni za nini? na ili iweje?

CC:- IGP na Kamanda MPINGA.
 
Kuna wale wa pale Kingolwira Morogoro, ila duh. .....
 
Njia nzima ya kibaha ni vurugu tu toka pale mizani mpaka chalinze,wale wametumwa pesa
 
Hivi kweli hujui hizo pesa ni za nini au unazingua tu?

Kwa kuwa huwa unasafiri mara kwa mara,fanya kuwauliza wahusika wenyewe watakujibu.
 
Kama unasafiri na gari lako binafsi kwenda mikoani hakikisha una kuwa na sh 1000 kama 30 hivi za usumbufu wa traffic.

Rushwa imehalalishwa tanzania.
 
Kama unasafiri na gari lako binafsi kwenda mikoani hakikisha una kuwa na sh 1000 kama 30 hivi za usumbufu wa traffic.

Rushwa imehalalishwa tanzania.

Mimi nasafiri mara kwa mara na gari langu binafsi sijawahi sumbuliwa na hao traffic sababu nafuata sheria zote za barabarani
 
Matajiri wenye mabasi mengi hawahangaiki na traffik vidagaa mikunndu wazi wanaopigwa na jua. Hua wanampa RTO mshiko wa nguvu mara moja kwa mwaka halafu RTO ndio anatoa amri kali kwa vidagaa kwamba mabasi fulani msiyabughudhi lkn hasemi kwamba kuna kitu kapewa. Sasa ole wake kidagaa mkunddu wazi mpigwa na jua mvaa nguo nyeupe alikamate hilo gari..atajuta kuitwa coplo
 
Nimetoka Mwanza jana kuja Arusha , tulivyotoka Babati karibia tunaingia Magugu Trafick alitusimamisha , akiongea kwa lafdhi ya kichaga na huku amelewa , kwa maana ya kulewa .
Dreva wetu alimpa elfu mbili !
Wakati tunaondoka mmojawetu akamuuliza dreva umempa sh ngapi?
"nimempa buku mbili"
"umempa zote hizo za nini ? Kwani umekua mgeni leo njia hii ? Huyu anapewaga buku-buku tu ya viroba!"
 
Mimi nasafiri mara kwa mara na gari langu binafsi sijawahi sumbuliwa na hao traffic sababu nafuata sheria zote za barabarani
Tatizo hao jamaa huwa hawakosi sababu ili mradi wakuchomoe tu!
 
Njaa kali pale Kibaha mpaka Mlandizi. Wanapenda sana rushwa
 
Mbona mijimama yote traffik Tanzania imesheheni nyuma ? ni kudra za allah au hela za rushwa zinanenepesha mitako.
 
Mbona mijimama yote traffik Tanzania imesheheni nyuma ? ni kudra za allah au hela za rushwa zinanenepesha mitako.

Hili swali hujalitendea haki !
Halikuhitajika uliulize via comment!
Liulize via Thrade ! Coz lina elements za ukweli 98% !
 
tatizo hao jamaa huwa hawakosi sababu ili mradi wakuchomoe tu!

halijakukuta. Ipo siku nilishuhudia askari mmoja akiwaonyeshea speed radar 70km/h kila dereva aliyekuwa anapita mbele kidogo ya kibaha kongowe kwenye kituo cha mafuta. Na mimi akanitendea hivyohivyo. Nikashangaa kwani speed yangu ilikuwa 40km/h. Nilivyogundua baada ya kumbambikia wa nyuma yangu haraka akaniruhusu.
 
mfike mahala muache asikari wale hivi vijirushwa jamani,sasa askari kutwa kasimama juani na mshahara mwisho wa mwezi hata ungekuwa wewe mleta mada ungeacha kulamba two thousand?
_kwanini usiandike kihusu rushwa kwenye mikataba na huko mahosupitalini?na kule kwenye ule mjengo wa makinda?
_siwapendi asikari ila mmezidi kuwaandiaka loh
 
waache ndugu zetu wale, sasa buku 2 wewe unakuja kufungua uzi hapa. pambana na rushwa kubwa za bilioni, hizi wacha maisha yaende. siku nyingine ukifika hapo nunua juice na apple uendelee na safari ya askari waachie wenyewe na konda, au kama unataka muondoke hapo saa 4 wasitoe buku 2.
 
Nimetoka Mwanza jana kuja Arusha , tulivyotoka Babati karibia tunaingia Magugu Trafick alitusimamisha , akiongea kwa lafdhi ya kichaga na huku amelewa , kwa maana ya kulewa .
Dreva wetu alimpa elfu mbili !
Wakati tunaondoka mmojawetu akamuuliza dreva umempa sh ngapi?
"nimempa buku mbili"
"umempa zote hizo za nini ? Kwani umekua mgeni leo njia hii ? Huyu anapewaga buku-buku tu ya viroba!"

Wewe mpuuzi mkosa elimu tumbo kubwa unakula mpaka una kunyakunya ovyo
 
Mimi nasafiri mara kwa mara na gari langu binafsi sijawahi sumbuliwa na hao traffic sababu nafuata sheria zote za barabarani

Nakubaliana nawe, miye huwa nikifanya kosa namwambia aniandikie notification faster ili iniumie nisirudie kosa. Tunaendekeza wenyewe haya mambo.
 
Back
Top Bottom