Askari wa kikoloni waliwaua Waafrika na kukusanya fuvu zao kwa ajili ya Makumbusho yao (Museums)

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
13645343_1061325033955916_8857944332286101220_n.png

Askari wa kikoloni wakifaransa waliwaua Waafrika wengi kwa lengo la kukusanya fuvu zao ili kuimarisha Makumbusho yao ya historia (Museums) na walikuwa wakiingiza fedha nyingi sana kwenye hayo makumbusho yao. Na walienda mbali zaidi kwa kuweka picha za vichwa vya waafrika kwenye Stempu Zao kwa ajili ya kutuma Barua. Historia hii haitasahaulika, kwa vizazi hadi vizazi.
 
Binaadamu itabidi tupewe jina jingine...

Ahsante kwa kutujuza.
 
Pia usisahau walichukua mali zetu tena bado wanachukua.
sijui hatima yake nini dah inauma..
 
Lilikuwa koloni gani hilo? Maana makoloni ya wafaransa hapa afrika yanajulikana.inasikitisha sana
 
Mleta mada hii huwezi kupata wachangiaji umeharibu kusema mkoloni mfaransa.
Ungesema mkoloni mwarabu sasa hivi bandiko lako lingesha sheheni wachangiaji mpaka ungesikia raha..
Lakini unawasema wafaransa wazungu umebugi mkuu.
 
Dhambi walizotufanyia hao wakoloni wazungu hazitasameheka na wametengeneza wakoloni weusi wanatutawala mpaka leo jamaani tupiganie ukombozi wetu na wa mtu mweusi
 
Back
Top Bottom